Ghana:Kanisa linataka kuunganisha mazingira na ajira kwa vijana!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Tatizo kubwa zaidi linalotishia ushirikiano wa kijamii, utawala wa kidemokrasia na usalama wa taifa nchini Ghana na katika sehemu nyingi za dunia ni ukosefu wa ajira wa vijana. Ni uthibitisho wa Askofu Mkuu Philip Naameh, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tamale, nchini Ghana wakati wa kutoa hotuba katika Warsha la Usimamizi wa mazingira, ambao ni mpango mkubwa wa usimamizi wa Jimbo Kuu la Ghana ambalo kwa kiasi kikubwa wanataka kuthibiti takataka za kielektroniki ambazo anasema kuwa hutoka duniani kote kuingia Barani Afrika kila mwaka.
Kwa kuonesha hatari hiyo kubwa Askofu Mkuu Naameh anathibtisha kwamba, kuna zaidi ya tani 215,000 ambamo kati ya tani hizi ni ni viyoyozi vya hewa, friji, televisheni, mashine za kuosha, kompyuta, mashine ya kupuliza taka, simu za mkononi na balbu za mwanga, ambazo sehemu nyingi hutokea bara la Ulaya. Lengo kuanzisha mpango huu ni kutaka kubadili maafa ya mazingira katika fursa za ya kazi kwa vijana wa Ghana. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Naameh kwamba, kama ukusanyaji na uangalizi wa taka za umeme ungekuwa umepangiliwa vizuri, ungeweza kuunda nafasi za kazi kwa vijana.
Kadhalika Askofu Mkuu amesisitiza kuwa, Kanisa linataka kupitisha mbinu ya ubunifu juu ya suala hilo kwa kujifunza kuunganisha mifano ya biashara katika usimamizi wa taka za elektroniki. Katika suala hili, amekazia kuwa Kanisa linajaribu kutafuta ushirikiano ambao hutoa mtaji wa uwekezaji katika mpango wa biashara,ambao haujihusishi na faida bali kujihusisha zaidi katika uendelevu.
Naye Samweli Zan Akologo, mkurugenzi mtendaji wa Caritas nchini Ghana amethibitsha kuwa kuwa warsha hiyo inaonyesha mwanzo wa upanuzi wa mradi wa Kuthibiti Taka wa Caritas zaidi ya mji mkuu, wa Accra, na kuongeza kuwa hautaangalia tu juu ya hukusanyaji wa taka za umeme, lakini pia kuunda sehemu ya kuwezesha mvunjo vunjo wa taka hizo ambao unaweza kutoa fursa ya nafasi za ajira kwa vijana. Mradi huo wa Caritas ulianzishwa mnamo Oktoba 2017, katika kujibu au kuenzi Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato Si.