Kardinali Tagle Askofu Mkuu wa Manila nchini Ufillipini anasema maandamano kwa ajili ya maisha yanaweza kujenga jamii yenye makaribisho kama tumbo la uzazi wa mama Kardinali Tagle Askofu Mkuu wa Manila nchini Ufillipini anasema maandamano kwa ajili ya maisha yanaweza kujenga jamii yenye makaribisho kama tumbo la uzazi wa mama 

Ufillipini:Katika uchaguzi ni kuiweka nchi katika mikono mizuri!

Maono ya Kardinali Luis Antonio Tagle, Askofu Mkuu wa Jimbo la Manila anasema katika uchaguzi ni kuiweka nchi katika mikono mizuri na hivyo inahitaji ukarimu na mshikamano. Amesema hayo katika fursa ya maandamano kuhusu utetezi wa maisha na katika mtazamo wa upigaji kura unaotarajiwa Mwezi Mei mwaka huu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Inahitaji kuiweka nchi katika mikono mizuri, mikono ambayo ina ukarimu na mshikamano kwa sababu ya jamii ya ufillipini iweze kuwa bora katika kukaribisha kama umbu la mama linalotunza maisha. Ni maono ya Kardinali Luis Antonio Tagle, Askofu Mkuu wa Jimbo la Manila kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari za kimisonari la Fides, akielezea juu ya  hali halisi ya nchi yake katika matazamio ya nchi katika uchaguzi  wa kati, utakaofanyika mwezi Mei. Askofu Mkuu Tagle anasema, kura zitasaidia katika uchaguzi wa wawakilishi wabunge na waseneti 12, pia kupyaisha majukumu yote ya utawala wa mikoa, wilaya na tarafa. Hata hivyo amepata fursa ya kuzungumza hayo katika tukio la Mandamano makuu ya utetezi wa maisha.

Kuwa na shauku ya kugeuka tumbo la uzazi ambamo kuna maelewano

Kardinali Tagle amezungumza wakati wa Misa Takatifu wakati wa fursa ya maandamano kuhusu utetezi wa maisha, ambayo ni maandamamo makubwa katika nchi nyingi lakini pia sana hata katika nchi ya Ufillipini, yaliyofanyika tarehe 16 Februari 2019. Katika mahubiri yake anaonesha matarajio kwamba, maandamano kwa ajili ya maisha yanaweza kujenga jamii yenye makaribisho zaidi kama tumbo la uzazi wa mama ambapo kina nafasi kubwa ya kushirikishana, maelewano  na watu, jumuiya  na viongozi. Ni shauku yake kwamba jamii yao inaeza kugeuka kuwa kizazi cha maisha kwa sababu ya kuwa na mikono ya wale wanaoishi kwa ukarimu na siyo wachoyo.

Kardhalika Askofu  Mkuu Tagle akitafakari maneno ya Yesu ameonesha mantiki ya kutoa hasa kwa mantiki ya matendo ya ukaribu na upendo ambao unatakiwa kuwa na ukarimu na jitihada za mshikamano na wengine. Aanasema kiasi kidogo cha mkate iwapo kitapitia katika mikono mizuri, kinaweza kuongezek, kwa mujibu wa Injili inayohusu Yesu na mkate. Lakini akaonya kuwa , kwa upande wa mikate 7000 itagawanywa na watu wachoyo, haitatosha kwa watu hata wanne, kwa maana ni mikono ambayo inaua. Na hiyo ni hasara kubwa kwa ajili ya jamii, na wakati huo huo  katika kazi ya uumbaji inazidi kutoa kwa ukarimu na kutakiwa kutunzwa na wote.

Vijana wengi waliudhuria maandamano kuhusu  maisha

Katika tukio hilo, kulikuwa na vijana wengi walioudhiria maandano hayo. Maandamao ya kwa ajili ya maisha katika  Kanisa la Ufilippini linapendekeza kila mwaka kwa ajili ya maisha na hadhi yake ya kuwa mwanadamu. Maandamano ya mwaka huu yamefanyika katika miji ya Dagupan, Tarlac, Cebu, Ormoc e Cagayan de Oro, hata mji wa  Palo na Palompon.

Watu wawe makini kuchagua wagombe wanaoaminika na kuzuia ufisadi 

Katika suala  juu ya uchaguzi wa  mwezi Mei, hata Askofu Mkuu  Crispin Varquez, wa Jimbo Kuu Katoliki la Borongan, amewaalika waamini wapige kura kwa uwajibikaji ili kusahihisha thamani zilizopinda na ambazo zimeonekana katika uchaguzi uliopita. Kwa mujibu wa Askofu mkuu Varquez, watu watapiga kura kwa wanasiasa ambao wanaonekana kuwa wema katika serikali. Na hii ni kwa sababu imefikia wakati sasa wa kutaka madiliko halisi wakikumbuka fursa iliyopita ya uchaguzi, katika wilaya masikini zilipata matukio ya kuuza na kununua kura. Mfumo wa ufisadi wa namna hii,  anasema unahatarisha zaidi kuwa na wagombea wasio aminika. Kwa maana hiyo ni lazima kutimiza uwajibu wa haki katika mang’amuzi na kuchangua mgombea ambaye anajali ustawi wa pamoja, kama msingi wa kusimamia (Fides 19/2/2019).

21 February 2019, 11:22