Tafuta

Vatican News
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia wanaomba jumuiya ya kimaifa kuingilia kati suala la kipeo cha wakimbizi wa Rohingya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia wanaomba jumuiya ya kimaifa kuingilia kati suala la kipeo cha wakimbizi wa Rohingya  (ANSA)

ASIA:Ni dharura kukabiliana na kipeo cha Warohingya!

Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia wanaomba Jumuiya ya kimataifa kukabiliana kwa dhati kipeo cha wakimbizi wa Rohingya

Na Sr. Angela Rwezaula

Ni dharura kwa jumuiya ya kimataifa  kutafuta  suluisho la kidiplomasia kwa ajili ya kipeo cha wakimbizi wa Rohingya waliokimbia kutoka Myanmar kwenda Bangladesh. Ndiyo maombi ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Barani Asia (FABC) baada ya wajumbe 40 wawakilishi wa Kanisa Katoliki kutoka nchi 11 barani Asia hivi karibuni kutembelea makambi ya wakimbizi wa Rohingya huko Bangladesh na Myanmar, katika sehemu ya Cox’s Bazar karibu na Chattogram mpakani mwa Bangladesh na Myanmar.

Wakimbizi na nguvu zilizopyaishwa

Ziara yao imefanyika ndani ya Mkutano wa kimataifa uliojikita katika mada kuu msingi. Mojawapo ya mada hizi  ni masuala ya wakimbizi na ile ya kupyaisha nguvu  iliyo tathiminiwa katika mantiki ya bara la Asia. Shughuli hiyo fanyika tarehe 11-14 Februari 2019 huko Cox’s Bazar  na Ofisi kwa ajili ya maendeleo ya binadamu (OHD) ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asa (FABC) kwa ushirikiano na Tume ya Baraza la Maaskofu ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu la Bangladesh (CBCB) na Mtandao kwa ajili ya haki na amani katika Bara la Asia na Pasifiki (APJPWN).

Inahitajika kuunganisha sauti ya pamoja katika kutafuta suluhisho la kipeo

Wakati wa mkutano, wawakilishi hao walipata fursa ya kutembelea mrundiko wa  Warohingya ambao ni wageni katika maeneo ya Kutupalong, Ukhia, Cox's Bazar na waliweza kuzungumza na kubadilishana mawazo na baadhi yao, kuwasikiliza matatizo yao na wasiwasi wao. Kutokana na hiyo Askofu Msaidizi Allwyn D'Silva, wa  Jimbo la Bombay na Katibu Mkuu katika ofisi ya  maendeleo ya binadamu na madiliko ya Tabianchi ya FABC amesema kuwa, Jumuiya ya Kimataifa inaalikwa kuunganisha sauti moja tu ili kusaidia wakimbiai wa Rohingya na kutafuta suluhisho la kipeo hicho.

Kuungana kiroho na Baba Mtakatifu

Kwa kuungana na Baba Mtakatifu Francisko ambaye tarehe 1 Desemba 2017 alikutana na wawakilishi 16 wa Jumuiya ya Warohingya, maaskofu wanathibitisha kwamba walisikitishwasana na historia yao na wamekumbuka kwa kile alichosema Baba Mtakatifu ya kwamba:tusifunge miyo yetu, tusigeukie upande mwingine. Uwepo wa Mungu leo hii ni wito kwa Rohingya, amekumbushwa Askofu D’Silva. Na ameongeza kusema: “ziara yetu hii imetufanya kutambua tabia na makaribisho ya watu na Serikali ya Bangladesha ambayo imefungua milango na mioyo kwa ajili ya Warohingya. Tunawapongeza kwa ushirikiano  na watu wengi wenye mapemzi mema ambao wanatoa jibu kwa ajili ya mahitaji ya haraka ya watu waliorundikana.

Wasiwasi kwa ajili ya wanawake na watoto

Hata hivyo  Askofu D'Silva amesisitiza kwamba, wanatazama kwa shukrani zaidi ya kusaidiwa kwa ukamu na utaalaam ulitolewa kwa Wakimbi wa Rohingya kwa upande wa Kanisa Katoliki la Bangladesh kwa njia ya Caritas, kwa msaada wa mtandao wa Kimataia wa Caritas pamoja na mashirika mengine ya dini, Mashirikia ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya Kiserikali. Vilevile amesema, hata hivyo sasa tumeweza kutambua matatizo na vizingiti vya mfumo  wa kuwandalia makazi ya  muda mfupi uliotolewa kwa wimbi la wakimbizi wa Rohingya, wakati huohuo ni  pamoja na changamoto zilizopo kwa mamlaka kwa ajili ya kuweza kujibu kwa utayari na mwafaka wa mahitaji ya kibinadamu, ambayo yametokana na wimbi la watu. Wasiwasi wetu mkubwa  kwa namna ya pekee ni kwa upande wa waathirika wengi wanawake na watoto wakati tukitambua juu ya matatizo mengi yanayoiukumba jumuiya iliyo wakaribisha.

Takwimu ya wakimbizi  Warohingya      

“Hatuwezi kuacha uelezea mshikamano wa wakimbizi wa Warohingya. Jumuiya ya Kimataifa inapaswa iunganishe kwa pamoja ili kuwasaidia, ameongozea Padre Charles Irudayam, mwakilishi kutoka India. Zaidi ya Warohingya 740,000 wamekimbia kutoka Myanmar karibu na Bangladesh baada ya vurugu zilizorekodiwa na Serikali ya Birmania huko Rakhine mahali ambapo walikuwa wanaishi kunako 2016-2017. (Shirika la habari Fides).

Hata hivyo kuna haja ya  kuwatafutia wakimbizi nchi ya tatu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mwaka jana 2018 mahitaji ya kuwapatia wakimbizi nchi ya tatu ya hifadhi yalikuwa ni chini ya asilimia 5 licha ya kwamba mwaka huo ulivunja rekodi ya idadi ya kubwa ya wakimbizi waliosaka hifadhi ya nchi ya tatu.  Takwimu za UNHCR zilizotolewa leo huko mjini Geneva, Uswis zinafafanua kuwa takribani wakimbizi milioni 1.2 waliohitaji kuhamishiwa nchi nyingine kwa mwaka 2018, ni wakimbizi 55,692 pekee ambao walipatiwa makazi mapya. Idadi kubwa zaidi ya wakimbizi hao waliokuwa awanatafuta hifadhi nchi ya tatu kwa msaada wa UNHCR ni waliotoka nchi zenye wakimbizi wengi zaidi ikiwemo Lebanon wakimbizi 9,800, Uturuki wakimbizi 9,000, Yordan wakimbizi 5,100 na Uganda wakimbizi 4,000. Akifafanua zaidi, Shabia Mantoo ambaye ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Uswisi amesema: "Asilimia 68 ya majina yaliyowasilishwa mwaka jana walikuwa manusura wa vurugu na mateso, wale wanaohitaji kulindwa kisheria  na wanawake na wasichana waliko hatarini.

Zaidi ya nusu yaani asilimia 52 ya maombi ya kutafutiwa nchi ya tatu walikuwa watoto”. Kwa mujibu wa UNHCR, katika mwaka huu wa 2019, inakadiriwa kuwa wakimbizi milioni 1.4 ambao wanaishi katika nchi 65 duniani kote watahitaji kuhamishiwa katika nchi ya tatu. Bi. Mantoo amesema wakimbizi wengi ambao wanatakiwa kuhamishwa ni pamoja na wakimbizi wa Syria ambao kwa sasa wanahifadhiwa katika nchi mbalimbali za mashariki ya kati na Uturuki kwa hiyo, “Mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbi unatoa wito kwa mataifa mbalimbali kutoa nafasi zaidi za kuwapokea wakimbizi kwa kupanua programu zilizoko hivi sasa au kwa kuanzisha programu mpya”.

20 February 2019, 12:59