Tafuta

Wafungwa wanaweza kujifunza wakiwa ndani ya magereza,baadaye wapate kushiriki maisha ya kijamii Wafungwa wanaweza kujifunza wakiwa ndani ya magereza,baadaye wapate kushiriki maisha ya kijamii 

Mpango wa Caritas Zambia pamoja na kituo cha utume wa walei Italia!

Wafungwa nchini Zambia wanakabiliana na hali mbaya ndani ya magereza,kwa maana hiyo mpango wa Caritas na Kituo cha kitume cha walei wa Italia wanatoa msaada ili wafungwa waweze kujikimu maisha yao mara baada ya kumaliza muda wao jela.Msaada huo unatazama afya,lishe na mafunzo kwa wafungwa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mfumo wa ndani ya magerenza nchini Zambia kwa kipindi ulikuwa unaelekea kudidimia na kuwa dharura ambayo inayotazama hasa afya,lishe na mafunzo kwa wafungwa. Kutokana na  dharura hii ni wazi kwamba kuna haja ya kuweza kuwasaidia wafungwa ili waweze kuishi na pia watakapo maliza muda wao kifungoni waweze kushiriki kimalifu katika jamii. Katika mtazamo huo tangu mwaka 2016 Kituo cha walei nchini Italia kwa ajili ya utume (Celim) ni Shirika lisilo la serikali  likiwa na makao makuu yake Milano ambacho kinashirikiana na Caritas nchini Zambia na taasisi nyingine kwa malengo ya kuingilia kati katika suara hili la dharura ili kuhamasisha na kukuza heshima ya haki za kibinadamu kwa wafungwa nchini Zambia. Dharura hii inajikita hata katika mtazamo wa kuwasaidia  wafungwa ili waweze kuunganika na kuaminiwa na kushirikshwa katika jamii. Lakini lengo kuu msingi ni kuboresha hali za maisha ya wafungwa katika magereza saba wanazohudumia Caritas kwa namna ya pekee hasa umakini wa wanawake na watoto waliofungwa nao.

Wafungwa wanakufa kwa sababu ya kukosa chakula, maji na matibabu

Mkurugenzi wa mpango kwa ajili ya Afrika wa Celim ameelezea katika Shirika la Habari za kimisionari Fides kwamba katika magereza nchini Zambia, wafungwa wanakufa kwa sababu ya kukosa chakula, maji na matibabu. Ukosefu wa huduma msingi za afya, hali ya majengo  na ambayo hayatoshi au ni ya kizamani na madawa yanayokosekana ni masuala ya dharura na ya kuingilia kati. Kwa namna ya pekee mahitaji ya wanawake na watoto hayashughulikiwi vya kutosha.Wanawake wajawazito hawapati hata matibabu yanayositahili,na watoto wa wafungwa wanaalazimika kushiriki chakula na mama zao. Wafungwa wanalazimika kuishi wamebanana katika vyumba vidogo sana, ambapo  katika eneo wanalipaswa kusihi wafungwa 8000, wanaishi wafungwa 25,000!

Mafunzo maalum kwa ajili ya kushirikishwa katika jamii

Kwa sasa mfumo wa Magareza nchini Zambia umeanza kujitahidi kubadili namna ya uendeshaji na utekelezaji wake kwa kutazama zaidi ya kuwasaidia wafungwa badala ya kujali sana adhabu kwao. Ili kuweza kufanya mabadiliko hayo ni kwa jia ya kujikita katika mpango wa mafunzo. Katika magereza saba ambayo Caritas ya Zambia inatoa huduma, wameandaa kozi maalum za utaalam kwa ajili ya wafungwa, kwa mfano kujifunza ufundi  umeme, useremala na ufundi mbalimbali na  kuwasaidia wafanye hata mitihani inayostahili ya kitaaluma.

Mipango miwili msingi kwa mwaka 2019 juu ya wafungwa

Bi Vigani akiendelea kufafanua suala hili, amesea wazo kuu la msingi  katika mipango yao ni lile la kujenga kwa pamoja uwezo ambao wanaweza kujiwezesha pindi tu wanapo toka katika magereza. Mpango wa mwaka 2019 una malengo mawili muhimu yanayotazamiwa hasa kujikita katika kuwashirikisha kiuchumi kijamii na kuunda vituo ambavyo vinaweza kuwasaidia mara tu wanapo maliza kutumikia jela. Hawa wafungwa  wanaweza kufanya kazi pamoja na kutoa mchango katika  raia wenzano kwa kutoa huduma ndogo ndogo ya useremala. Sehemu ya pili ya mpango ni ile ya kufanya mchakato wa mapatano, kwa kuhamasisha makutano ya wafungwa na familia zao pamoja na waathirika na kutoa huduma ya ushauri. Bi Vigano anathibitisha matumaini yake makubwa ya kwamba kuwashirikisha inawezekana, pia ni wajibu wa kufanya hivyo.

05 February 2019, 14:25