Hii ni sanamu maarufu ya Huruma ya Michelangelo (La Pietà)iliyopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,mjini Vatican Hii ni sanamu maarufu ya Huruma ya Michelangelo (La Pietà)iliyopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,mjini Vatican 

Michelangelo katika ubora wa picha zenye ukuu kitasaufi!

Tarehe 18 Februari 1564 ni mwaka alipofariki mjini Roma Michelangelo Buonarroti akiwa na umri wa miaka 89 mwana sanaa maarufu wa Firenze Italia ambaye aliweza kutengeneza kazi nzuri sana ya sanamu ya( Huruma, Musa na Daudi),katika mchoro mkubwa wa Volta na Hukumu ya Ulimwengu katika Kanisa la Sisitina Vatican

Na Sr. Angela Rwezaula

Tarehe 18 Februari 1564 ni mwaka alipofariki mjini Roma Michelangelo Buonarroti mwana sanaa maarufu wa Firenze, Italia ambaye aliweza kutengeneza kazi nzuri sana ya sanamu ya (Huruma, Musa na Daudi), katika mchoro mkubwa wa Volta na Hukumu ya ulimwengu katika Kanisa la Sisitina) Vatican na katika usanii wa mchoro kwenye paa la Mtakatifu Petro. Alikuwa ni mtu mwenye akili na mnyenyekevu, ambaye alikuwa kuchota nguvu ya usanii wake kutokana na imani yake. Michelangelo Buonarroti msanii alifariki mjini Roma siku chache kabla ya kufanya sikukuu ya kutimiza miaka 89, siku ya kuzaliwa kwake ni tarehe 6 Machi. Katika siku zake za mwisho alitafakari maisha yake na mawazo yake ya mwisho yalikuwa ni katika sanamu ya Huruma iitwayo Rondanini, sanaa ambayo hadi leo inatunzwa katika Jumba la Makumbusho ya kifalme Sforzesco huko Milano nchini Italia.

Kazi ya sanaa ya Huruma “Rondanini” na homa kali

Mwanafunzi wake Daniele da Volterra anaandika kwamba, alikuwa karibu naye hadi kifo chake na alipewa majukumu ya kufunika picha ya Huruma ya ulimwengu kwa kile kiitwacho maarufu kama braghe (ndiyo maana waliipa jina Braghettone). Michelangelo alifanya kazi Jumamosi nzima siku kabla ya Jumapili na kabla ya kuanza kipindi cha kwaresima. Jumatatu aliiugua; lakini wakati huo alifanya kazi kwa akiwa amesimama na kutafakari juu ya mwili wa sanamu ya  huruma. Homa kali ilimpelekea kifo akiwa katika nyumba rahisi ya Macel de Corvi mtaa wa Fornari Roma.

Kifo chake siku ya Ijumaa ya kwanza ya kwaresima 1564

Baada ya kusimama kwa muda mrefu alikubali kukaa katika sofa, akiwa anahudumiwa na Tommaso de Cavalier, kijana tajiri wa Roma na madaktari wawili na ambao waliwaomba waende kumwita mpwa wake Leonardo aliyekuwa anaishi Firenze. Jumatatu tarehe 14 Februari, kabla ya kwaresima Daniele da Volterra, alimwandikia mpwa wake akimbie kwa haraka kumwona Michelangelo, ambaye taratibu alianza kupoteza fahamu hasa siku ya Jumatano ya majivu. Baada ya kuwekwa kitanda cha chuma, akiwa na fahamu kidogo alimwomba Antonio amsomee sehemu ya Mateso ya Kristo. Baadaye aliandika wosia wake na kuaga dunia jioni ya siku ya Ijumaa ya kwaresima. Leonardo mpwa wake aliweza kufika tarehe 24 Februari, wakati mwili wa Michelangelo tayari unapumzika katika Kanisa la Watakatifu Mitume, akiwa amevalishwa nguo kama msafiri!

Mwili ulipelekwa Firenze na kuzikwa katika Kanisa la Msalaba Mtakatifu

Sehemu ya kwanza ya mazishi mjini Roma haikuwa ya mwisho kwa msanii huyo mkuu maana ilifuatia hatua nyingine za mizinguko. Kwanza mamlaka ya Vatican walipendelea Michelangelo azikwe katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, lakini mpwa wake Leonardo akafanya maandalizi kisiri na kusafirisha sanduku la marehemu usiku hadi Firenze mahali ambapo alifika tarehe 11 Machi. Tarehe 12 walizika, lakini baadaye tarehe 14 Julai ikafuatia mazishi makuu katika Kanisa la Mtakatifu Lorenzo. Masalia ya Michelangelo yalihamishiwa tena katika Katika la Msalaba Mtakatifu mwaka 1570  hadi leo hii.

 Kukumbuka ya Michelangelo katika Kanisa la Sistina

Katika kukumbuka msanii maarufu Michelangelo ni kukutana na Guido Cornini, mkurugenzi wa kitivo cha sana ya karne ya XV na VXI katika Jumba la Makumbusho Vaticana. Katika Kanisa dogo la Sisitina ambalo analifafanua kama mchoro Mtakati wa kweli wa Michelangelo ambaye aliweza kuingia mara mbili katika Kanisa hilo: mara ya kwanza aliwa na miaka 30 alipochora picha ya Volta na baadaye alikuwa na miaka 60 hivi alipochora picha wa Hukumu ya mwisho. Ndiyo vielelezo vikuu vya Michelangelo, msaniii maarufu ambaye lakini alikuwa tayari amechora  hasa kama msanii wa kuchonga sanamu, anaandika Cornini na kwamba katika hisotria ya Michalengelo anajilikana kuwa akiwa kijana mdogo alikuwa anaudhuria vipindi katika bustani ya Mtakatifu Marco, kwa madaktari, mahali ambapo alijifunza na mwanafunzi wa kuchonga Bertoldo Di Giovanni na ambaye alikuwa amejifunza sana kuwa na utambuzi wa kuchonga sanaa za kale  hadi kufikia kuchonga sanaa maarufu sana ya Huruma kwa ajili ya Kanisa la Mtakatifu Petro, kunako 1489-99 ambaye hadi leo hii ni moja ya shughuli msingi za usanii wa kisasa wa  kuchonga nchini Italia.

 

19 February 2019, 13:33