Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni vyombo na wajenzi wa amani duniani! Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni vyombo na wajenzi wa amani duniani!  (Vatican Media)

Italia:Chama cha Vijana wakatoliki Roma wanataka amani!

Tarehe 3 Februari 2019 mjini Roma umefanyika msafara wa amani ulioandaliwa na Chama cha Vijana Wakatoliki Jimbo Kuu la Roma.Msafara umeishia katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa kushiriki sala ya Malaika wa Bwana na kusoma ujumbe wao mbele ya Baba Mtakatifu wakionesha hamu ya kutaka amani duniani

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 3 Februari mjini Roma umefanyika msafara wa amani ulioandaliwa na Chama Vijana wakatoliki Jimbo Kuu la Roma. Mada iliyoongoza msafara wa mwaka 2019 ni “radha ya amani”. Saa mbili na nusu  walianza na liturujia ya misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu Misaidizi wa Jimbo la Roma Mashariki, Askofu Giampiero Palmieri katika Kanisa la Maria wa Vallicella na baadaye washiriki wote walianza msafara hadi katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Baada ya kufika uwanja wa Mtakatifu Petro, Rais wa Chama Cha vijana Katoliki Rosa Calabria na wahusika wa kitaifa wa chama cha vijana walisalimia washiriki wote. Saa 6.00 walishiriki sala ya Malaika wa Bwana na Baba Mtakatifu akiwa na vijana wawili wa Chama cha Vijana Watoliki kwa niaba ya yao walisoma ujumbe wao mbele ya Baba Mtakatifu Francisko.

Jitihada za chama cha vijana Wakatoliki kwa ajili ya amani

Ujumbe wa vijana unasema kuwa, hata mwaka huu,vijana wakatoliki kwa pamoja na marafiki, mapadre na wakuu wao,wamerudi tena kwake ili kumwambia kwa nguvu kuwa wanataka amani. Aidha wapo pamoja katika  kuadhimisha uzinduzi wa miaka 150 wa kuanzisha kwa chama cha vijana Wakatoliki Roma na miaka 50 ya kuzaliwa kwa Chama chama cha vijanawadogo wakatoliki (ACR). Ujumbe wao unasema iwapo hawajaeleweka, wanataka amani kwa maana wameelewa kuwa amani ni jambo jema la kipekee  na tamu na ambalo linatoa radha ya mahusiano yao na kuwafanya roho zao zigeuke kuwa safi na bora zaidi.

Mchakato wa mafundisho yao ya mwaka huu ni mapishi jikoni

Vile vile Vijana Wakatoliki katika ujumbe wao, wanaonesha mchakato wa mafundisho yao mwaka huu yanayotazama jiko yaani mapishi na ndiyo maana wamechagua Siku hii kwa kauli mbiu “radha ya amani”. Amani kidogo ni kama chumvi, wanasema na kwamba iwapo hakuna chumvi katika chakula, kinapoteza radha na inatosha kidogo kuweka usawa wa radha katika sahani. Leo hii iwapo wanaona kuwa na  hali ngumu kati yao na duniani hawapaswi lakini kukata tamaa au kugeukia sehemu nyingine, badala yake ni kujikita katika matendo ya amani japokuwa hawezi kusuluhisha kila tatizo, lakini kwa hakika ni kutoa radha katika dunia hii wanathibitisha!

Matendo ya dhati

Vijana wakatoliki Roma pia wamemwakikishia Baba Mtakatifu Francisko juu ya kutaka kushiriki kwa dhati katika matendo yao ya ukaribu na hivyo fedha walizokusanya wanataka kusaidia mpango wa tabasamu kwa ajili ya kanda zilizo maskini duniani kwa kuhakikisha thamani ya chakula na haki kwa wale wanaozalisha ili wote waweza kuwa na haki inayostahili ya kazi na kuishi kwa hadhi. Kadhalika wamonesha uwepo wao katika siku hiyo kwamba ni kutazama mambo mawili muhimu kwanza ya Chama cha Vijana Wakatoliki Roma wanatimiza miaka 150  na kwa maana hiyo wanawaomba Papa na maaskofu sala zao ili wasichoke kutangaza Injili! Pili hata Chama cha Vijana wadogo Wakatoliki, wanatimiza miaka 50 na kwa maana hiyo ni nusu karne vijana wadogo wakatoliki wanatafuta kutajirisha chama chao kwa njia ya uwepo wao na juhudi ya kusimulia ni kwa jinsi gani ilivyo vema kukutana na Yesu! Wanamwomba Baba Mtakatifu Francisko awaombee katika sala zake!

Wamehitimisha ujumbe wao kwa Baba Mtakatifu Francisko, wakimshukuru kwa jitihada kubwa sana ya kusimulia Yesu na  jinsi gani ya kumfuata katika maisha yao. Wanasema: “Inaonekana kuwa huchoki kamwe na hivyo hata sisi hatutachoka kusema tunapenda amani ! ndiyo!”  “Na chama cha Vijana wakatoliki Roma wanakutakia mema” .Baada ya kusoma ujumbe wao, wameachia maputo yakapaa angani. "N ishara ya sala za wote kwa ajili ya amani duniani", kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko! Maelezo zaidi soma: http://is.gd/carovanadellapace2

 

 

04 February 2019, 15:42