Papa Francisko akiwa na Mfalme wa Abu Dhabi,Mohammed bin Zayed Al-Nahyan wakati wa sherehe fupi kabla ya kuondoka nchini humo Papa Francisko akiwa na Mfalme wa Abu Dhabi,Mohammed bin Zayed Al-Nahyan wakati wa sherehe fupi kabla ya kuondoka nchini humo 

Abu Dhabi:Baada ya ziara ya Papa ni kuendeleza utume wa ujenzi wa maelewano na umoja kati ya dini

Baada ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu katika Nchi za Falme za Kiarabu (abu Dhabi),ushuhuda wa wengi unaonesha kuonja hali halisi ya utulivu,sikukuu,umoja na urafiki kati ya watu wote kwa siku hizo,hivyo ni muhimu kukuza utume wa kujenga maelewano na kuishi pamoja kati ya dini zote zilizomo ndani ya nchi hizo!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ilikuwa ni mwafaka wa furaha kubwa kukutana na Baba Mtakatifu! Ilikuwa ni baraka kubwa ya Mungu kwa ajili ya wote ambao wanaishi katika Falme za nchi za Kiarabu. Ndiyo maneno ya Nadeem Lal Bhatti Mkatoliki kutoka Pakistan anayeishi Falme za nchi za kiarabu kwa miaka 7 hivi, akijikita katika kikundi cha huduma ya kiliturujia kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu huko Abu Dhabi. Amesema hayo kwa kukumbuka ziara ya Baba Mtakatiu Francisko katika Falme za Uarabuni iliyofanyika tarehe 3-5 Frebruari 2019.

Shirika la habari za kimisionari Fides, kwa mujibu wa Bhatti anathibitisha kuwa ni ziara itakayobaki katika mioyo na  akili zao, kwa kumbukumbu ya kuishi kirafiki na watu wa mataifa mbalimbali kwa siku zile. Wote walionja kwa dhati hali ya utulivu, sikukuu na urafiki hasa wasio wakristo! Aidha kwa kusisitiza  zaidi anasema, watendelea katika jitihada za kujenga madaraja ya maelewanao na mshikamano. Baba Mtakatifu aliwapatia watu wote na jamii nzima ya Uarabuni, ujumbe wa amani, matumani na kuishi udugu. Baada ya ziara hiyo wote wamehisi na kutambua kuwa mada ya kuvumiliana na kuishi kati ya waamini wa dini tofauti ni ya lazima na ni kujibidisha kila siku ili kuongeza nguvu. Hata hivyo amekumbusha kuwa Falme za nchi za kiarabau (UAE) kwa mwaka 2019 wanaadhimisha mwaka wa kuvumiliana. Falme za nchi za kiarabu, zimeakaribisha watu zaidi ya mataifa 200 kutoka mabara tofauti. Japokuwa uislam ndiyo dini rasmi, lakini inajulikana katika kuheshimu na hadhi ya kila imani.

Naye kijana Adonis Panen kutoka nchini Uffilippini ambaye ni mhudumu maalumu wa kutoa ekaristi Takatifu na ambaye alihudumia liturujia wakati wa Misa ya Baba Mtakatifu, amethibitisha kwamba Ziara ya Baba Mtakatifu katika Taifa hilo, imeacha urithi mkubwa wa furaha kati ya wakatoliki na wasiyo kuwa wakatoliki. Hali ya furaha ilikuwa ikionekana kati ya watu wooe walioudhuria misa na kuongeza nguvu ya umoja, amani na maelewano katika Falme za nchi za Uarabuni. Hadi sasa bado wanahisi na kushi katika mwangwi wa furaha hiyo! Kadhalika ushuhuda mwingine ni wa John kutoka India anayeishi huko miaka 20 na ambaye alitoa huduma ya kujitolea katika siku hizo, anathibitisha kuwa: walifanya kazi kwa kina kwa miezi miwili katika maandalizi ya mantiki zote za ziara yake. Ilikuwa ni ndoto ya kila mbatizwa kuudhuria Misa ya Baba Mtakatifu. Kwa upande wao wanaoishi na kufanya kazi katika nchi za Falme za Kiarabu. ilikuwa ni moja ya baraka maalum. Mungu amewawezesha kupata fursa hiyo na ambayo wataipeleka daima kama sanduku lililojaa tasaufi na ubinadamu,  (Fides 21/2/2019).

22 February 2019, 13:37