Tafuta

Chama cha Wanawake Wakatoliki nchini Australia kinapenda kuwahamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa! Chama cha Wanawake Wakatoliki nchini Australia kinapenda kuwahamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa! 

Chama cha Wanawake Australia: Utume wao ndani ya Kanisa!

Chama cha Wanawake Wakatoliki nchini Australia kuanzia tarehe 22-24 Februari 2019 kinakutana huko Adelaide ili kujadili jinsi ya kuwajengea wanawake uwezo, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kupanga, kuamua na kutekeleza maamuzi mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa. Hii ni nafasi ya kutafakari kuhusu mchango wa wanawake katika maisha na utume wa Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake ya kitume nchini Perù alionesha masikitiko yake makubwa kutokana na nyanyaso na dhuluma ambazo wanawake wanakumbana nazo katika maisha na utume wao, kutokana na utamaduni wa mfumo dume ambao umepitwa na wakati! Hawa ni wanawake ambao wameendelea kujizatiti katika kulinda na kuzitegemeza familia zao katika huduma ya elimu, afya na ustawi katika ujumla wake. Wanawake bado wanabaguliwa hata katika maeneo ya kazi na kwamba, hawa ndio waathirika wakuu wa balaa la umaskini, mauaji ya wanawake pamoja na nyanyaso ambazo zinakwenda kinyume kabisa cha utu na heshima yao.

Ni kutokana na changamoto hizi, Chama cha Wanawake Wakatoliki nchini Australia kuanzia tarehe 22-24 Februari 2019 kinakutana huko Adelaide ili kujadili jinsi ya kuwajengea wanawake uwezo, ili hatimaye, waweze kushiriki kikamilifu katika kupanga, kuamua na kutekeleza maamuzi mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa. Hii ni nafasi ya kutafakari kuhusu mchango wa wanawake katika maisha na utume wa Kanisa. Tafiti mbali mbali zilizofanywa katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita zilionesha kwamba, ushiriki wa wanawake katika maisha na utume wa Kanisa ulikuwa mdogo sana.

Chama cha Wanawake Wakatoliki nchini Australia kikawaomba Maaskofu kuangalia uwezekano wa kurekebisha hali hii, ili kuwapatia wanawake nafasi ya kushiriki katika uongozi wa Kanisa kwa kuzingatia taaluma zao. Baraza la Maaskofu Katoliki Australia linasema, hi ni sehemu ya mchakato wa mageuzi, unaopania kuwashirikisha zaidi wanawake katika maisha na utume wa Kanisa!

Wanawake

 

19 February 2019, 10:56