Migogoro ya kanda ya Sahel bado ipo ambayo pia inachangiwa uhaba wa chakula,mabadiliko ya tabianchi na mafuriko Migogoro ya kanda ya Sahel bado ipo ambayo pia inachangiwa uhaba wa chakula,mabadiliko ya tabianchi na mafuriko 

Mkutano wa Caritas huko Senegal kwa ajili ya kusaidia kanda ya Sahel!

Maamuzi ya matendo ya dhati katika mkutano wa Caritas uliofanyika kuanzia tarehe 31 Januari hadi 1 Februari 2019 nchini Senegal umetazama baa la njaa,mafuriko na wimbi la wahamiaji,kwa mujibu wa maelezo ya Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis ambaye ameshiriki mkutano hai katika mji wa Saly

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuanzia Mali, Niger, kuelekea Italia,Uhispania,Ubelgiji,Danimarca,Austria na nchi nyingine ambapo ni wawakilishi wa Caritas 20 za Afrika na Ulaya  na zaidi moja inayowakilishwa na Marekani ambao tarehe 31 Januari hadi 1 Februari 2019 wamekutana nchini Senegal kwa ajili ya Mkutano wao wa mwaka wa Kikundi cha kusaidia Sahel. Hiki ni kikundi kilichoundwa ndani ya Caritas Intenationalis. Ukanda wa Sahel ni sehemu kubwa ya Afrika chini ya Jangwa la Sahara ambapo kwa kipindi kirefu imekumbwa na kipeo kibaya cha ukosefu wa msimamo wa kukithiri kisiasa pia hata kuongezeka kwa kipeo cha vyakula, kukumbwa na mafuriko na mabadiliko ya tabia nchi.

Kusaidia Sahel ili kupambana na uhamiaji na baa la njaa

Naye Moira Monacelli Mwakilishi wa Caritas ya Italia katika Caritas Internationalis ambaye ameshiriki mkutano huo amefafanua kwa kifupi juu ya mkutano ulivyofanyika kwamba wameunganika katika mji wa Saly nchini Sengal na kujikita hasa katika kutazama matatizo makuu mawili. Kwanza ni mabadiliko ya tabia nchi yanayo sababisha baa la njaa na uhamiaji. Kwa maana hiyo ni lazima kutafuta suluhisho ili kuwezesha jumuiya mahalia kuvumilia mabadiliko haya. Na tatizo la pili ni uhamiaji. Ukanda ya Sahel unajulikana kwa uzoefu mkubwa wa mzunguko wa mtu na hivyo anaongeza kusema kuwa ni changamoto kubwa ya kibinadamu.

Mpango wa matendo ya dhati ni kuanzia mipango ya chini kabisa

Baada ya mkutano huo watatoa uamuzi wa dhati ambapo Bi Moira anayo matumaini. Mpango wa kwanza wa matendo anasema unatazamiwa kudumu kwa miaka miwili na pia kusisitiza juu ya  kuweka umakini juu ya ulinzi wa vyakula na uhamiaji. Jumuiya mahalia itaalikwa kuwakilisha mpango wao ambao utasaidia katika matendo ya dhati kuanzia ya chini, kwa maana hiyo wanaweza kutoa chachu ya kujiendeleza  na ambayo ni lazima, amehitimisha Bi Moira.

05 February 2019, 13:11