Cerca

Vatican News
Askofu Maronta ameandika barua ya wazi akiomba Maduri aleze nini maana ya matendo na maneno yake,kuzuia misaada ya kibinadamu na azuie umwagaji damu Askofu Maronta ameandika barua ya wazi akiomba Maduri aleze nini maana ya matendo na maneno yake,kuzuia misaada ya kibinadamu na azuie umwagaji damu 

Venezuela:Barua ya Askofu Maronta kwa Rais Maduro!

Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Venezuela Askofu Maronta ameandika barua iliyo wazi kwa rais Maduro akimwomba atoa sababu za matendo yake,maneno yake na vizuizi vya msaada wa kibinadamu,lakini zaidi anaomba azuie umwagaji damu na kusilikiza kilio cha watu wanaoteseka kwa njaa na madawa

Na Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Barua yake inayochota maneno ya shairi la mtunzi Simón Bolívar, Askofu Mario Maronta wa Jimbo Katoliki la Mtakatifu San Cristóbal na Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu Venezuela, baada ya kutoka katika mafungo huko Equador,ili aweze kuandika kwa moyo wa kibinadamu kwa Rais wa Venezuela Nicolás Maduro. Askofu anamwomba Rais atoa sababu gani za matendo yake, maneno yake vizingiti vya msaada wa kibinadamu:anaomba pia kuzuia umwagaji damu na kusikiliza kilio cha watu. Anasimulia mateso ya watu ambayo wanakabiliana naye leo hii, hasa  katika kipeo kikubwa cha kisiasa, uchumi, kijamii, kimaadili na ambacho anathibitisha hakijawahi kusikika namna hii katika nchi hiyo. Kukataa kwake, anaongeza ni kama kufunika jua kwa kidole kimoja.

Suala la njaa kwa kukosa chakula cha kutosha na ukosefu wa madawa 

Aidha Askofu Maronta anashutumu suala la njaa itokanayo na ukosefu wa chakula cha kutosha na madawa. Anathibitisha kuwa ni rahisi kukana kwa kutumia maneno makali,dharau na vitisho akidai kuwa kila fursa kwamba sababu ni vita ya kiuchumi. Hiyo ni ndiyo kuna vita ya uchumi lakini siyo ile dhidi ya Serkali au Taasisi ya Serikali bali ni ile dhidi ya watu Askofu anaandika. Kwa kusititiza anasema,“ninapaswa kusema ukweli kama alivyoshauri Mshairi Bolívar kwamba: “mtu wa watu amechoka kwa sababu ya kuendelea kudharauliwa”. Sehemu kubwa ya watu,wanateseka na kipeo cha aina ya kibinadamu na ninaweza kushuhudia. Mimi siyo kama yule anayebaki amefunga milango yake ya ofisi, bali ninatembea kati ya jumuiya na kukutana na wote bila kubagua”.

Watu wanaomba kusikilizwa hali, sauti zao na zaidi mabadiliko ya kisiasa

Askofu Maronta anagusia aidha maombi ya mazungumzo kwa upande wa Maduro na ukosefu wa kusikiliza hali halisi zilizo wekwa mbele, miaka miwili iliyopita kwa upande wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kwamba : “Kama angeweza kusikiliza watu na kilio chao, kiukweli ingewezekana kutimiza hatua za kufungua milango ya kuleta suluhisha kipeo”.  Na watu wanaomba kusikiliza mateso yao, wanaomba kuheshimiwa hali zao, hadhi zao na haki zao, zaidi wanaomba mabadiliko ya kisiasa. Hata hivyo Askofu Maronta pia amendika barua ya pili ya wazi kwa wale ambao wanashika nafasi ya nguvu za kijeshi akiwaomba walinde watu na siyo kuzuia kupita kwa msaada wa kibinadamu (kutoka Shirika Sir).

20 February 2019, 14:28