Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu mjini Bucarest, Romania Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu mjini Bucarest, Romania 

Ziara ya Papa Romania:Kuna haja ya umoja kati ya familia,Kanisa!

Padre Wilhelm Danca Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Bucarest nchini Romania anaelezea matumaini yake juu ya ziara ya Baba Mtakatifu nchini mwao iliyotangazwa kuanzia tarehe 31 Mei hadi Juni 2, 2019 inaweza kuwa ishara ya imoja kati ya familia, Kanisa na kijamii katika nchi ambayo kwa saa inapitia kipindi kigumu cha maelewano

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Romania itatoa msukumo wa kutafuta sababu mpya ya kuweza kuishi kwa pamoja na umoja. Ndiyo matarajio ya Padre Wilhelm Danca Mkuu wa  Kitivo cha Chuo Kikuu cha Bucarest  nchini Romania kufuatia na kutangazawa rasmi ziara ya Baba Mtakatifu ambayo inatarajiwa kufanyika tarehe 31 Mei hadi tarehe 2 Juni 2019 ambapo  Baba takatifu anatarajia kutembelea miji ya Bucarest Iaşi, Blaj na Madhabahu ya Bikira Maria ya Șumuleu Ciuc.

Akifafanua maana ya sababu kuwa na umoja wa familia, Kanisa na Jamii

Mkuu wa chuo Kikuuu Katoliki nchini Romania padre Wilhelm Danca anathibitisha kuwa  Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko itakuwa ni kutoa msukumo zaidi wa kuweza kupata suluhisho na  sababu mpya za kuweza kuishi hasa kwa sababu za kuunda ule umoja wa familia, katika Kanisa na jamii. Mkuu huyo anathibitisha hayo  kutokana na kwamba nchini Romania kwa kipindi hiki ni mahali ambapo pamekuwa na migawanyiko hasa kwa mtazamo wa kisiasa, na kwa sababu hiyo nchi kwa dhati inahitaji kweli kitulizo na kutiwa moyo ili iweze kubaki na uaminifu wa thamani kuba za kikristo. Ni msukumo kwa ajili ya mchakato mzima hasa wa kiekumene, ambao kwa sasa unapitia kipindi cha ubaridi. Kutokana na hili ni matumaini yake  kwamba ziara ya Baba Mtakatifu Francisko inaweza kweli kuleta hali nzuri kwa ajili ya kutafuta maana ya kuhisi ule upamoja na kuishi zaidi kwa kusali pamoja na maelewano

Kuna haja ya kujenga umoja kati ya kanisa na jamii pia

Kadhalika amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwa na umoja hata katika Kanisa na si tu katika jamii, kipindi hiki cha majaribu ya ushirikishwaji wa Ulaya na ambapo bado umejikita kama hatua muhimu ya maendeleo ya Romania. Yote hayo ni kutokana na kwamba hapakuwapo na kufikiria kuwa kile ambacho kimefikia hatua ya kutokuwa na usawa kati ya watu kwa mfano, kati ya wenye ajira na wale wasiokuwa na ajira, hata wale ambao hawawezi kuendelea mbele katika maisha yao, suala ambalo pia linagusa hata kambi ya elimu na kidini.

Jinsi gani wanaishi watu wa Romania

Akifafanua ni kwa jinsi gani watu wa Romania wanaishi, amesema kuwa kwa sasa idadi ya watu wazima wakatoliki imepungua kwa maana wana jumuiya inayondwa na watotot na wazee wakati watu wazima wamekwenda nchi za nje au katika miji mikubwa ya nchi. Hii ni changamoto inayohitaji kutafuta mwafaka wa umoja, amethibitisha.

Baba Mtakatifu atatembelea madhabahu ya Bikira Maria huko Șumuleu Ciuc

Madhabahu ya Bikira Maria huko Samuleu Ciuc ni eneo la kihistoria ambayo inaelezea mwendelezo na Mtakatifu Yohane Paulo II alipoitembelea nchi ya Romania na kutembelea bustani ya Bikira Maria. Madhabahu ni kielelezo cha wana wa Romania lakini pia nchini Romania kuna mchanganyiko kwa maana inaweza kuitwa Ulaya ndogo, umoja katika utofauti kwa ajili ya lugha na imani.

14 January 2019, 07:36