Tafuta

Karibia majengo elfu moja ya kufanyia ibada nchini Angola yamefungwa, kufutia na kuibuka dini ambazo hazina mpangilio Karibia majengo elfu moja ya kufanyia ibada nchini Angola yamefungwa, kufutia na kuibuka dini ambazo hazina mpangilio  

Zaidi ya majengo elfu moja ya ibada yamefungwa nchini Angola!

Mswada wa Sheria nchini Angola umepitishwa wa kufunga majengo ya ibada kufuatia na kuibuka kwa dini hovyo bila mpangilio na sheria ya sasa lazima wawe na kibali na dini yoyote iwe na idadi ya waamini wake laki moja katika wilaya 12 kati ya wilaya 18 za nchi

Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Zaidi ya majengo ya ibada ya kikristo yalifungwa na mamlaka nchini Angola kati ya tarehe 6 Novemba hadi 25 Desemba 2018 kutokana kuibuka kwa dini nyingi kila kikicha, bila mpangilio na haya bila kuwa na kibali. Hatua hiyo imefikia kukubaliwa kwa mswada mpya wa sheria  na kupitishwa ambapo unataka kila aina ya dhehebu ya dini ijiandikisha katika serikali kupata kibali pia angalau waamini wa dhehebu hilo wafikie lakini moja. Kila kikundi cha dini lazima kijiandikishe katika ofisi ya Waziri wa Haki na Utamaduni, japokuwa kabla ya sheria hiyo kupitishwa baadhi ya makanisa hayo yalikuwa tayari  yako nje ya sheria kwa mujibu wa Mkutano wa Mawaziri wa Angola kabla ya kuchukua hatua, kwa ajili ya mchakato wa uundaji na marekebisho ya kufunga majengo hayo.

Taarifa inasema sheria mpya ya sasa nchini Angola, inahitaji kuwa dini zote lazima zijiorodheshe katika Ofisi ya waziri wa Haki na Utamaduni ili  kupata kibali cha haki ya utambulisho wa huduma za ibada. Lengo la kujiandikisha ni pamoja na kuthibiti majengo ambayo yamekuwa hayastahiki kwa mujibu wa sheria mpya.Na zaidi Kanisa hilo liwe na waamini laki moja angalau katika wilaya 12 kati ya wilaya 18 za nchi ya Angola.

Kwa kufuatia vigezo hivyo ni wazi kwamba kuna uthibiti au hakuna ruhusa ya makundi madogo madogo mapya ya kidini yanaweza kujiandikisha ili kupata kibali kama vile makundi anayoibuka ya kiinjili na kiislam nchini Angola. Mkurugenzi kitaifa katika masuala ya kidini kwenye ofisi ya Waziri wa Utamaduni nchini Angola, Bwana Francisco de Castro Maria, anathibitisha kwamba, asilimia 50 ya Makanisa yaliyoko katika nchi yao ni kutoka nje ya nchi yao kwa namna ya pekee kutoka nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Brazil, Nigeria na Senegal. Bwana De Castro Maria anabainisha kwamba kwa kuchukua hatua hii mpya ya kisheria ndiyo itakuwa ni mwisho wa mchakato mrefu wa mapambano dhidhi ya taasisi hizi mpya zilizohibuka nchini Angola tangu mwaka 2013.

Katika kipindi hili, nchi ilikuwa karibu na makanisa mapya laki tisa na kati ya makanisa hayo ni 82 mbili tu ambayo yanatambuliwa rasimi na Ofisi ya waziri wa utamaduni na kukubaliwa kuendelea na shughuli zao. Kwa mujibu wa habari zaidi nchini Angola (Angop), majengo ya ibada yaliyoko katika migogoro yalifungwa katika wilaya tofauti kaskazini kwa namna ya pekee huko Kabinda (900) Bengo (21) Zaire (7) Uinge (79) na mengine 29 yalifungwa kutokana na kinyume na sheria huko Luanda Kusini  mashariki ya nchi. Zaidi ya kufungwa kwa maeneo ya ibada  huko Kabinda, pia  polisi wa taifa waliwakamata wachungaji 11 ambao hawakutii katika makanisa mengine ya kikristo yanayoibuka.

Wachungaji haowalikamatwa kati ya tarehe 16-23 Desemba 2018, kutokana na kukiuka sheria ya kufungua makanisa hayo wakati yamethibitwa kufungwa. Hata hivyo kwa mujibu wa Polisi anathibitisha kuwa kati ya makanisa mengine 58 yaliyokubaliwa na serikali,kufanya kazi yake,  lakini majengo hayo yao hayastahili kwa shughuli ya uendeshaji wa kidini na  majengo 141 hayana vibali vya sheria.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni nchini Angola wanaishi watu milioni 21 ya ambao kwa asilimia 55 ya wakristo ni wakatoliki na asilimia 25 ni  waluteri na makanisa mengine ya kikristo, asilimia inayobaki inaendelea kuamini dini za kiasili. Dini ya kiislam kwa upande wa Angola inahesabuka ni sehemu isiyojulikana kwa mamlaka kwa maana waamini wake ni wachache mbao ni karibu watu 50,000 au 80,000 na kwa mujibu wa sheria mpya wako nje ya mswada wa sheria.

07 January 2019, 13:44