Tafuta

Askofu Leuzzi katika barua kwa vijana mwezi Januari 2019 anawaomba wamwamini Yesu kwa maana watafutwa na kupendwa na marafiki zao Askofu Leuzzi katika barua kwa vijana mwezi Januari 2019 anawaomba wamwamini Yesu kwa maana watafutwa na kupendwa na marafiki zao 

Umaarufu hautokani na nafasi uliyo nayo ni katika kujitoa zawadi kwa ndugu!

Kuwa mtu maarufu haina maana ya kuwa na cheo au nafasi uliyo nayo ya juu katika jamii, badala yake ni kujitoa zawadi kwa ndugu. Amethibitisha hayo Askofu Lorenzo Leuzzi wa Jimbo Katoliki la Teramo- Atri nchini Italia katika barua yake kwa vijana katika mwezi Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo hii tunaishi katika jamii ambayo tunasukumwa kutembea bila kuwa na utambuzi. Unakwenda mbele, lakini hujui ni kwa nini. Iwapo unataka kuwa na utambuzi ni kitu gani unajenga katika maisha yake,unatakiwa kuamini yule Mtoto katika Pango la Bethlehemu, anakutazama na kutabasamu katika ishara ya kukuhakikishia kuwa usiwe na hofu na kwamba nipo mimi! Ni katika barua ya Askofu Lorenzo Leuzzi wa Jimbo Katoliki Termo - Atri  nchini Italia, waraka wake kwa vijana wa jimbo lake katika mwezi wa Januari 2019.

Uzoefu wa kukatishwa tamaa hayupo kaburini

Mbali na vijana wa Jimbo lake, lakini ujumbe huu ni muhimu kwa vijana wote, kwani, Akiwa anarudi kutoka katika Hija ya Nchi Takatifu, Askofu Leuzzi anaonesha kuwa kama ilivyo watole mitume wawili wa Emau (Lk 24,13-53), hata yeye amefanya uzoefu kama ule wa kukata tamaa, ambapo mara baada ya kusikia kuwa kaburi lilikuwa wazi na Yeye lakini alikuwa wapi? Akiwa huko Emau alitambua na kuhisi kuwa anapaswa kuanza safari kwa upya. Kutokana na hilo anathibitisha kwamba  huo ndiyo uzoefu wa kila mmoja katika usiku ule wa Noeli, usiku ambao Mtoto alikuwa amelala holini kati ya Maria na Yosefu, ambayo ni ishara ya uaminifu kwa Mungu.

Kaa karibu na mfufuka na kufungua macho yako utaona njia yako imejaa furaha

Askofu Leuzzi anaandika kwamba,Mungu aliamua kukaa nasi daima kwa maana hiyo, sisi sote tunaweza kabisa kuanza upya safari, lakini je ya kutufikisha wapi? Anauliza Askofu. Katika kutoa jibu anasema. “ Wengi wanapendelea kufumba macho yao na kutambea bila kujua wanakwenda wapi. Wengine wanachanganya mambo mengi kati ya mipango yao binafsi ya kutimiza na ile mipango ya Mungu. Lakini kwa hakika yote hayo ni rahisi iwapo utajikita kukaa na mfufuka karibu. Fungua macho yako na utaona kuwa njia yako imejaa furaha kubwa”. Askofu Leuzzi akiendelea kuandika anasema, unaweza kupanga kwa dhati lakini ikiwa  michakato ya mipango yako tayari umeielekeza katika safari iliyo jaa furaha. Kwa kufanya hivyo hautakuwa na uchovu kamwe katika safari yako. Usiwe na hofu ya kujiuliza maswali juu ya maisha yako. Rudi katika akili yako, dhamiri yak na moyo wako katika Pango la Bethlehemu. Muulize mtoto  Yesu iwapo anafurahi kwa ajili ya maisha yako.

Yesu na maisha ya kila mmoja, kwa kumtegemea yeye anakuwezesha mengi

Yesu anatualika kugundua ukuu wake wa maisha yako, anaongeza Askofu Leuzzi, na kusema, mwamnini Yeye! Unaweza kufikiria makuu lakini Yeye atakusaidia, usifikiri kama abunuasi , atakuwa karibu nawe ili upate kushinda hatua ndogo ndogo au kubwa za maisha yako kila siku. Utakuwa daima na furaha muhimu kwa ajili yake kwa sababu ili uweze kuwa muhumu kwa ajili yake ndiyo siri ya kuishi binafsi maisha yako! Na ndiyo ujana wa kweli Askofu anabainisha. Kila siku utakuwa na utambuzi ya kuwa na ili uweze kuwa mtu muhimu haina maana ya kuwa na cheo fulani au nafasi iliyo ya juu katika jamii, badala yake ni wewe mwenyewe kuwa zawadi kwa ajili ya ndugu kwa maana walio wengi katika jamii hii wanajihisi ni muhimu sana! Lakini wanajidanganya na mara nyingi wanawatendea vibaya ndugu wengi. Kwa maana hiyo wewe mwamini Yeye na kwa kufanya hivyo utatafutwa na kupendwa na marafiki zako.

VIJANA EMAU
08 January 2019, 13:54