Tafuta

Vatican News
Katika mchakato wa Sinodi inayoendelea katika Kanisa kila mmoja atambue kuwa anao utume na uwajibu wake wa kupeleka mbele na ambao unaweza kujikita katika wema Katika mchakato wa Sinodi inayoendelea katika Kanisa kila mmoja atambue kuwa anao utume na uwajibu wake wa kupeleka mbele na ambao unaweza kujikita katika wema  (Vatican Media)

Sinodi 2018:Sinodi imetoa tafakari juu Kanisa linavyotakiwa kuwa leo hii!

Askofu Msaidizi Anselmi wa Jimbo Kuu Katoliki la Genova Italia, amethibitisha kuwa Sinodi ya Vijana ya mwaka 2018 imetoa tafakari kuu kuhusu Kanisa linavyo takiwa kuwa leo hii. Amesema hayo wakati wa Mkutano na vijana walioshiriki uliofanyika tarehe 5 Januari 2019 mjini Roma kwa kuandaliwa na Ofisi ya Kichungaji kwa ajili ya miito ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kilichotimishwa hivi karibuni, ilikuwa ni Sinodi ya Kanisa na siyo kwa vijana tu, kwa maana ilikuwa ni tafakari ya namna gani Kanisa linatakiwa kuwa leo hii. Haya ni maneno yaliyosemwa na Askofu msaidizi Nicolò Anselmi wa Jimbo Kuu Katoliki la  Genova Italia wakati akiwa pamoja na walioshiriki Sinodi ya mwisho ya Maaskofu kuhusu vijana iliyoongzwa Vijana imani na mang’amuzi ya miito kuanzaia tarehe 3-28 Oktoba 2018, katika Mkutano hivi karibuni wa Kitaifa kuhusu miito na ambao ulioongozwa na kauli mbiu: “ni kama vile waliona kisichoonekana”.

Ni mkutano ilioandaliwa huko Roma tarehe 5 Januari 2019 na Ofisi ya Taifa ya huduma ya Utume wa Miito wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia. Katika hotuba yake, Askofu Anselmi amesema kuwa Baba Mtakatifu Francisko anapendelea Kanisa kutembea pamoja kama ilivyokuwa katika Sinodi na kwa maana hiyo  vijana na maskini wanahitimishwa kama kieleleza cha kuwa, sisi sote tunayo maana ya kweli iwapo tunaweza kutembea kwa pamoja na wote. Wakati wa sasa na endelevu ni lazima uwe na rangi ya kimisionari ya Sinodi amesisitiza Askofu!

Bado tupo katika mchakato wa Sinodi

Askofu Anselmi akisisitiza juu ya maana ya kutembea pamoja kama Sinodi, amethibitisha kwamba, kwa sasa ina maana ya kuwa bado tupo katika mchakato wa Sinodi, na ambapo kwa kukumbushwa na Mtaguso wa Pili wa Vatican ambao ulituachia urithi wa namna ya dhati ya Kanisa yaani ya kuishi pamoja na hali ya kuwa pamoja  ambayo inahitajika na lazima kuhisi kwa kina. Lakini zaidi hali hii inaweza kufanyika kwa vijana zaidi kama vile walivyothibitisha hata maaskofu wa Amerika ya Kusini kuwa hali hii si vijana tu bali na masikini pia!

Kadhalika akitazama juu ya Sinodi iliyopita na ambayo lazima iendelezwe katika matendo, Askofu Anselmi amethibitish kwamba mkutano huo wa Sinodo ni jambo muhimu ambalo hatuwezi kufikiri kwamba limefika mwisho. Na ili kuweza kukabiliana na Sinodi inayotakiwa kuwa endelevu, Askofu alionesha hatimaye hatua inayotakiwa kuchukuliwa akionesha umuhimu wa kushirikiana. Sifa ya kwanza ya Sinodi amesema ni umisionari,kwa maana ya uzoefu mbalimbali wa vijana katika kushirikiana kwa pamoja unatoa mvutio na kuwaalika marafiki na wanafunzi wengine, lakini ikiwa jambo hili litaandaliwa na watu wengine bila kuwahusisha na kuwashirikisha wahusika, halisi basi haitaleta mvuto na ushiriki wa kweli.

Padre Gianola (Cei) anasema baada ya Sinodi shughuli nzima ya kichungaji igeuke kuwa wito

Naye Padre Michele Gianola Mkurugenzi wa Ofisi ya Kitaifa kwa ajili ya shughuli za Kichungaji kwa ajili ya miito wa Baraza la Maskofu Italia ( Cei), wakati wa kutoa hotuba yake anasema wakati wa kusikiliza hotuba mbalimbali zilizotolewa,amekuwa na hisia ya suala la kuwasiliana na hali halisi, ile hali ya kudumbukia ndani ya historia yetu Kanisa letu na dunia, kwa maana hiyo ni katika  kujikita ndani ya hali halisi! Majadiliano yameweka bayana hata kwa baadhi ya ugumu, majeraha na mateso ya mwili wa Kanisa.  Padre aasisitiza kuwa,kutazama ndiyo kazi ya kwanza ya kufanya mang’amuzi. Kutazama  ndiyo wajibu wetu wa kwanza katika kutoa huduma ambayo tunaweza kufanya mara baada ya Sinodi hiyo na ili  shughuli ya kichungaji na kwa pamoja ziweze kugeuke kuwa wito.

Majadiliano ya Sinodi yageuke kuwa maisha na mapinduzi ya Kanisa 

Kadhalika Padre Gianola amebainisha ya kuwa walipendelea kupanua muda wa siku mbili wa Mkutano ili kutoa nafasi kubwa kwa sauti mbalimbali. Anaamini ya kwamba katika shughuli ya kichungaji kwa ajili ya miito na uchungaji kwa ujumla wake. unaweza kutoa nchango mkubwa wa maisha. KWA maana hiyo waamini wote, vijana  wote wanaalika kila mmoja atambue kuwa anao utume, anao uwajibu wa kupeleka mbele ambao unaweza kujikita katika mchakato wa kutenda wema. Padre Gianola amethibitisha kuwa shughuli ya Sinodi imehitimishwa kwa kutoa Hati ambayo inapaswa kuhaririwa na kufungwa vizuri na baadaye kuwekwa katika maduka ya vitabu, lakini majadiliano ambayo yamefanyika yanaweza kwa dhati kugeuka maisha na mapinduzi ya Kanisa letu.

SINODI VIJANA
08 January 2019, 15:03