Vatican News
Vijana 14 katoliki wa Pakistan wakiwa tayari na hati zao za kusafiria wamekataliwa katika uwanja wa ndege ili kuudhuria Siku ya Vijana huko Panama Vijana 14 katoliki wa Pakistan wakiwa tayari na hati zao za kusafiria wamekataliwa katika uwanja wa ndege ili kuudhuria Siku ya Vijana huko Panama  (Vatican Media)

Pakistan:Vijana katoliki wamezuiwa katika uwanja wa ndege,Lahore kwenda Panama!

Vijana 14 katoliki waliokuwa tayari kusafiri wakiwa na visa na hati zote kamili za kusafiki wamezuiwa kuondoka wakiwa uwanja wa ndege wa Iqbal,Lahore Pakistan ili kuudhuria siku ya Vijana duniani huko Panama inayoendelea.Vijana hao wanaonesha masikitiko makubwa

Na Sr.Angela Rwezaula -Vatican

Katika ofisi ya uhamiaji kwenye uwanja wa ndege wa Iqbal, Lahore, wamesimamishwa vijana katoliki kuendelea na safari kati ya tarehe 23 na 24 Januari 2019 ambapo  tayari walikuwa wanaelekea katika Siku ya vijana duniani inayoendelea huko Panama kuungana na wenzao katika maadhimisho haya makubwa kwa vijana. Kama ilivyoripotiwa na mwakilishi Katoliki nchini Pakistan kwenye Shirika la habari za kimisionari Fides anathibitisha kwamba, wamezuiwa vijana 14 wakiwa tayari na visa na hati zote za kusafiria, ila ni mseminari mmoja tu wa Kijesuit aliyeruhusiwa kuondoka.

Ukatishwaji tamaa wa vijana

Paul Mohan Mratibu wa Tume ya vijana katoliki wa jimbo la Hyderabad, anasimulia kwa masikitiko makubwa shirika la habari za kimisionari Fides juu ya kukatishwa tamaa sana kutokana na kukatishwa kwa safari hii, kwa maana ilikuwa tarehe 23 Januari wakiwa tayari wamesha pita kukaguliwa uwanja wa ndege na tayari wameshapewa tiketi za kuingia ukumbi wa kusubiri waondoke, lakini kufika mbele ya ofisi ya uhamiaji, walisimamishwa zaidi ya saa moja na kuwakatalia ruhusa ya kuendelea mbele. Imekuwa ni jambo la kusikitisha sana kwa kundi lote la vijana anasema!

Aidha anasema kwamba walitafuta njia zote kuzungumza na wajumbe wa ofisi ya wahamiaji  na hata wakuu wa ndege waliyokuwa wanaondoka nayo, lakini wapi, bila kupata mwafaka wowote! Ilibidi walibadili tarehe ya kuondoka kesho yake yaani tarehe 24 Januari 2019 kwa kulipa gharama, wakiwa na matumaini ya kufanikiwa. Siku ya pili yake, Ofisi ilithibitisha kwa upya yale yale kwamba hata kama wana visa na barua ya kusindikizwa na maaskofu, wasingeweza kuwaruhusu.

Tiketi ya ndege ni gharama na hati zao za kusafiri zilikuwa sawa lakini hazikutosheleza 

Tiketi ya moja ya ndege waliyokuwa wamekata iligharimu Rupia za Pakistan 300,000 ambazo ni karibia Euro 1,800. Kwa upande wa Atif Sharif Mratibu wa chama cha Vijana wa Jimbo Kuu Karach anathibitisha ni kwa jinsi gani ya kuona kweli hii ni leseni ya ubaguzi. Iwapo unaweza kutosheka na mantiki hiyo,ikiwa na maana ya  hati zote na vitambulisho vyote vilivyotolewa na Mabalozi wa nchi za nje, hata kupata visa, mzalendo lazima awe na uhuru kusafiri. Vile vile anathibitisha, kuna hata uwekezaji mkubwa wa safari ya kuelekea nchi za nje,japokuwa leo hii serikali yao inawabagua!

Haki ya kuzunguka, haki msingi

Haki ya kuzunguka ikijumuishwa haki ya kusafiri ni haki msingi wa kila mzalendo. Baadhi ya kesi za serikali zinaweza kuongeza majina ya raia wake katika orodha maalum ya kukagua wakati wa kwenda nje na kuweka vizingiti vya kuzuia kwenda. Lakini kama siyo hiyo, kitengo cha serikali hakiwezi kuzuia watu wasisafiri iwapo hati zotwa walizo nazo hazina kasoro. Hayo yamethibitishwa na Padre Bonnie Mendes wa Faisalabad, pia kutokana na hiyo ni lazima kupambana na siasa na sheria ili kutetea haki hiyo.

Suala hili, lazima litazamwe na Tume ya haki na amani au Tume ya haki za Binadamu

Ni suala ambalo linapaswa kukabiliwa na Tume ya Haki na Amani au Tume ya Haki  za Binadamu.  Hii siyo kwa mara ya kwanza wakristo wa Pakistan kukataliwa haki ya kusafiri. Ilikuwa ni mwaka 2018, Serikali ya Ireland iliwanyima visa  wakristo wa  Pakistan kwenda kuudhuria Mkutano wa Familia duniani. Na mwaka mwaka 2011 Serikali ya Uhispania iliwanyima visa vijana wa Pakistan na Bangladesh kuudhuria Siku ya Vijana duniani. Na kwa mara nyingine tena kizingiti kinatoka katika serikali yenyewe ya Pakistan kuwakatalia raia wake.  

 

 

 

25 January 2019, 15:29