Tafuta

Mtakatifu Francis wa Assisi na Sultani AL-Kamil wa Misri mwaka 1219 Mtakatifu Francis wa Assisi na Sultani AL-Kamil wa Misri mwaka 1219 

Pakistan:Maadhimisho ya miaka 800 tangu Mt.Francis na Sultani wa Misri

Miaka 800 iliyopita kati ya Mtakatifu Francis wa Assisi na Sultani wa Misri Al-Kamil ni msingi wa mazungumzo ya kidini katika ya waislam na wakristo. Rais wa Baraza la Maaskofu wa Pakistan, Askofu Sebastian Shaw amesema kuwa ni lazima kuwa mabalozi wa amani leo hii

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Ilikuwa mwaka 1219 wakati Mtakatifu Francisko wa Assisi alipoanza safari katika katika kipindi cha ghasia na migogoro na kuamua kutelemka katika kambi ya kuhamasiha amani kwa kupewa baraka na ruhusu ya Papa Onorio III wa wakati ule. Kwa maana hiyo alivuka mifereji miwili ya  bahari ya Meditranea na kufikia huko  Damietta, kilometa chache za na mjini Cairo. Pale alipata kuzungumza na Sultani wa Misri Maliki al Kamil kama vile  kutaka kuthibitisha kwamba Injili iliweza kukutana na Koran

Ni ishara yenye nguvu na ambayo hadi sasa inasubiriwa

Ilikuwa ni ishara isiyosubiriwa na nia yenye nguvu lakini ilibaki kwa muda mfupi na kuukuka kidogo, na zaidi ilifikiriwa zaia kushindwa, Lakini na kumbe ndiyo ilikuwa shauku ya Francis kutelemka kwa waislam bla mfuko akiwa na silaha moja tu ya heshima ambayo inajikita katika mapambano ambayo hata leohii yanapaswa kuanza kutafuta maelewano na umoja kati ya nchi za Mashariki na Magaharibi. Maskini Francis wa Assisi kwa maono yake ya uinjilishaji na matendo uake yanajikita katika mantiki nzima ambayo haijuliskani kwa kipindi na kujieleza kuwa ni msafara ambao kusaidia kitu.

Kufuatia na maadhimisho hayo ya miaka 800 tangu mkutano huo, nchini Pakistan tarehe 15 Januari 2019 wameanzisha Tume ya kitaifa kwa ajili ya mazungumzo ya kidini na kiekumene katika umbu la Baraza la Maaskofu nchini humo pia kuanzisha hata mambo mengi na sherehe ambazo zinajikita kutoa ujumbe wa dunia ule wa kuvumiliana hasa kwa mwaka ambao unajikita katika mazungumzo yanayoendelea katika siku hizi huko Lahore kwa uwepo wa Askofu, Sebastian Shaw, Askofu Mkuu na Rais wa Baraza la Maskofu na Francis Nadeem Msimamizi wa Shirika la ndugu wadogo wa Kapuchini nchini Pakistan na Katibu mtendaji wa Tume. Na kati yao walikuwapo na idadi kubwa ya wafransikani watawa, mapadre, walei hata wasomi wa kiislam walifika katika fursa hiyo hata kutoka  Sialkot, Gujranwala e Islamabad.

Kwa upande wa mazungumzo na picha ya viongozi maarufu

Viongozi hawa wakuu wawili Francis na Al-Kamil walipokutana walikiwa wakitaka kuhamasisha amani na uvumilivu kati ya hali halisi ya vita na migogoro wakati wa misafara ya wakati ule. Hawa ni watu wa kuigwa mfano wa kweli wa mazungumzo ya kidini na uelewa wa pamoja amesema Padre Nadeem. Picha inayoonesha mkutano kati ya Mtakatifu Francis wa Assisi na Al- Kamil ilioneshwa katika Mkutano huo, wakati huo  njiwa mbili nyeupe zilifunguliwa na kuachiwa huru ikiwa ni ishara ya matumaini ya kusambaza ujumbe wa amani nchini Pakistan na katika maeneo yote mahali wanapoishi na migogoro ya kidini na kisiasa.

Naye Mkapuchini Frateli Shahzad Khokher, akifafanua juu ya picha hiyo ameonesha mantiki ya kihistoria na maana ya mkutano huo wakati akisimulia historia ya kitubu kinachoitwa “Benedikto XVI na Mtakatifu Francis” na ambacho kinaraka kufafanya utafiti wa kitaalimungu, katekesi na kisaufi ya Papa mstaafu huyo juu ya maskini Mtakatifu Francisko , historia inayojikita juu ya kuongeza juhudi ya mazungumzo ya kidini, mada ambayo ni pendevu kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye alichukua jina la mtakatifu huo.

Wawe mabalozi wa amani nchini Pakistan

Askofu Mkuu Shaw aliwatia moyo washiriki wote ili wawe mabalozi wa amani , kwa kuiga mfano mkuu sana wa viongoiz hawa wawili wa wakati ule lakiniambao hadi sasa wanazungumza juu ya amani, na ambayo hadi leo hii utafikiri iko mbali sana. Kwa upande wa Padre Nadeem, pia alitangaza kuwa katika mwaka huu 2019 utaathimisha tukio hili nchi nzima ya Pakistan kwa kujikita katika shughuli mbalimbali, hususani semina kwa watoto, vijana wanafunzi wa vyuo vikuu, na kuwahusisha kwa namna ya pekee wakristo na waislam. Hiyo ni kwa lengo kutaka kudumisha uelewano na asilimia 30% ya viongoz wa dini yakiislam ambao wamekuwa wagumu  dhidi ya wakristo. Kama Mtakatifu Francis ambaye hakuwa na hofu kwa mdaaa wa waslam ambao wako karibu nao wanatamani wakutane nao ili kuhamasisha amani na maelewano nchini Pakistan.

 

16 January 2019, 16:00