Wakati wa Misa Takatifu Yerusalemu  tarehe 1 Januari 2019, Askofu Mkuu Pizzaballa amesisitizia juu ya Ujumbe wa 52 wa maadhimisho ya kuombea amani duniani Wakati wa Misa Takatifu Yerusalemu tarehe 1 Januari 2019, Askofu Mkuu Pizzaballa amesisitizia juu ya Ujumbe wa 52 wa maadhimisho ya kuombea amani duniani 

Nchi Takatifu:tunaitwa kufanya siasa safi ikiwa na maana ya kulinda amani!

Kufuatia ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya 52 ya Maadhimisho ya kuombea Amani duniani, Askofu Mkuu Pizzaballa, msimamizi wa nchi Takatifu Yerusalemu, kwa kuongozwa na ujumbe huo wakati wa mahubiri yake tarehe 1 Januari 2019 amesema kuwa, kufanya siasa safi ina maana kuu zaidi kwani ni kulinda amani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tunapaswa kuzungumza wazi na kwa huru, katika kulinda hali na amani, ili kuifikia mioyo ya wahusika wakuu wa miji yetu na kukuza ndani ya moyo wa kila mzalendo ule utashi na upendo au labda ile shauku ya ufalme wa Mungu. Matendo mema ya amani lazima yasindikizwe na tangazo la dhati na uwajibu wake wa kweli. Ndiyo mbiu ya maneno ya Askofu Mkuu Piebarbattista Pizzaballa Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Kilatino nchi Takatifu Yerusalemu, wakati wa mahubiri ya  maadhimisho ya Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na Siku 52 ya maadhimisho ya kuombea Amani duniani. Askofu Mkuu Pizzaballa akitafakari katika mahubiri kwa kuongozwa mwanga wa ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa siku ya Amani duniani amesema, wote wanaalikwa kujikita katika  siasa safi ikiwa na maana ya neno kuu yaani ya kulinda amani mbele ya hatari ambazo daima zinaitishia. Na ameonesha juu ya mahusiano yaliyopo kati ya Ufalme wa Mungu na matendo ya kisiasa.

Matatizo ni kama litania isiyoisha

Katika mantiki maalum wanayojikuta nayo, hasa katika majimbo yao na yale yanayo wazunguka, Askofu Mkuu amesema kila kitu utafikiri haiwezekani na yote yako mbali na amani kwa miaka mingi na kwa mwanga ambao kwa hali halisi wanaouishi. Katika maeneo yao wanaendelea kuona kuona hatari na kuanguka kwa mahusiano kwa ngazi zote za kijamii, mahusiano ya kisiasa na imani kijamii. Kwa miaka sasa mikataba imeshindwa; mipango ya amani iliyokuwa imetangazwa imeshindikana na kamwe haijawahi kutimizwa, mipango mingi ya kijamii iliyokuwa imeanzishwa, haijawahi kukamilisha, uchumi umeanguka… na mambo mengine ambayo yanaweza kuorodheshwa na ikafananishwa  na litania ya matatizo yasiyo pata suluhisho.

Kutia moyo katika kuendelea na siasa safi

Akiendelea na mahubiri, Askofu Mkuu Pizzaballa anabainisha kuwa matatizo yamegeuka kuwa sehemu yao ya mfumo wa maisha na namna ya kuishi na kufikiria. Katika mzunguko na kupanga kwa kila kitu na kwa kila kitu wanachokifanya. Hii ni hali ambayo inaendelea hasa katika kipindi hiki na kuwafanya kubaki kuamini hasa katika mji wao wa Yerusalemu, mji Mtakatifu, ambao kwa hakika yeye anathibitisha kuwa bado upo uwezekano wa kujenga Ufalme. Askofu Mkuu anatoa ushauri wa kufuata ujumbe wa Baba Mtakatifu hasa kwa wanasiasa wa kweli, yaani wasanii na wajenzi chanya wa mji wao, lakini ni lazima kuanzia na wadhaifu, watu walio wa mwisho, katika nyumba zao na katika jumuiya zao.  Aidha amesisitiza kuwa upo utashi wa kuendelea kuamini katika binadamu, japokuwa na matatizo yaliyopo ya kutokufanikiwa. Ni lazima kujifunza kwa kuwatia moyo wale wote wanaojikita katika kutengeza siasa safi.

Wanasiasa wanaweza kufanya kitu kidogo tu iwapo hawahusishi wengine

Kadhalika amethibitisha kwa jinsi gani ilivyo na haja ya kuwa na siasa safi hawa kwa watu ambao wanataka kujikita maisha yao katika miji  na  wenye uwezo wa kuungana na kuendeleza, japokuwa anaongeza kusema, Askofu Mkuu, wahusika wa kisiasa wanawewzakufanya kidogo iwapo watu wote na wenye mapenzi mema wasipoungana nao kujihusisha kwa ari na katika sera za kisiasa.Yote hayo lazima yafanyike kwa pamoja na si kufanya pekee. Wote wanayo haja ya kuinua mtazamo wao, kutazama mtoto wa Betlehemu, kwa sababu ni nguvu na jasiri wa kuweza kuwageuza kuwa wajenzi wa mji wao na ambao wanaweza kwa dhati kutafakari yule mtoto mdhaifu wa Betlehemu na ambaye ni upendo kwa walio wadogo.

02 January 2019, 17:00