Tafuta

Wakati Maaskofu nchini Marekani wanahamasisha mapokezi ya wahamiaji na wakimbizi, huku kiongozi mkuu anaendeleza nia ya ujenzi wa ukuta katika mpaka ili  kuzuia wageni Wakati Maaskofu nchini Marekani wanahamasisha mapokezi ya wahamiaji na wakimbizi, huku kiongozi mkuu anaendeleza nia ya ujenzi wa ukuta katika mpaka ili kuzuia wageni  

Marekani:Kujenga jumuiya ya mapokezi ni mada ya Wiki Kitaifa kwa ajili ya wahamiaji!

Kanisa Katoliki nchini Marekani limekuwa na utamaduni wa kufanya Wiki Kitaifa kwa ajili ya wahamiaji ambayo uanza siku ya Sikukuu ya Epifania hadi tarehe 12 Januari. Kwa mwaka 2019 wiki hii inaongozwa na kauli mbiu:“kujenga jumuiya ya mapokezi"; wakati huo huo naye Rais Trump nchini huo bado anaonesha nia ya kujenga ukuta mpakani wa kuzuia wahamiaji na wakimbizi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Juma la Kitaifa ka ajili ya wahamiaji nchini Marekani ambayo uanza siku ya Epifania hadi tarehe 12 Januari , yak ila mwaka ambapo kwa mwaka huu, Kanisa la Katoliki nchini Marekani, wananaungana katika sala na tafakari ya kina wakati huo huo wakiwa katika juhudi za kuimarisha mipango ambayo inatazama wahamiaji, wakimbizi na waathirika wengine wengi dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Mwa mwakaja 2019 juhudu hii ya wiki kwa ajili ya wahamiaji 2019 inaongozwa na kauli mbiu “ kujenga jumuiya ya mapokezi”. Hili ni lengo kuu la kuhamasisha wakatoliki waweze kukaribisha kwa dhati wageni wapya na kuwasindikiza katika kuanza maisha yao mapya yaliyojaa changamoto nyingi.

Kanisa linahitaji kujivika roho ya kweli ya makaribisho

Naye Askofu Joe Vásquez, Rais wa Tume kwa ajili ya wahamiaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, akifafanua juu ya siku hizi za Wiki kwa ajili ya wahamiaji amethibitisha kwamba, katika kipindi hiki maalum kwa  Kanisa ni muhimu kujikita kwa kina na kuvaa kweli roho ya mapokezi mema hasa kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi ambao tayari wamo ndani ya nchi yao. Maandalizi ambayo yamefanyika katika kusindikiza Juma Kitaifa kwa ajili ya wahamiaji Inawayaka kwa dhati jumuiya nzima kujihusisha katika kuudhuria kila anzisho lolote, kusikiliza mahubiri na sala,kufanya mikutano na wahamiaji, kufuata mitindo mbalimbali na kutuma hata barua pepe kwa wakurugenzi wa makundi mbalimbali ya maandalizi na kuhamasisha wengiil  waweze kusimulia matukio mbalimbali ambayo yanatokea katika nchi yao.

Mapendekezo yaliyotolewa yanasindikizwa na historia za kweli

Hata hivyo mapendekezo  yaliyotolewa yamesindikizwa na historia za kweli na maelezo muhimu juu ya mapinduzi ya wahamiaji na juu ya ulinzi wa kibinadamu, biashara haramu ya binadamu, mifumo mbalimbali ya mapokezi ambayo yapo, hasa mbele ya wale wadogo( watoto wadogo) ambao hawana wa kuwasindikiza na kwa hata familia ambazo zinatoka Amerika ya Kati. Mada zote hizo zimesindikizwa na idadi kubwa ya utafiti uliofanywa na vyombo maalum vya Serikali, lakini pia hata mashirika binafsi yasiyo ya kiserikali.

Nia ya Trump ya kujenga ukuta wa kuzuia wahamiaji na wakimbizi

Wakati Kanisa likihamasisha juu ya mapokezi ya wahamiaji na wakimbizi nchini  Marekani, naye Rais wa Marekani, Donald Trump amesema hali iliyopo katika mpaka wa Marekani na Mexico inazidi kuwa mbaya na imegeuka kuwa mzozo wa kibinaadamu. Rais wa Marekani. Amezungumza hayo wakati akihitubia taifa tarehe 8 Januari 2019 usiku  katika Ikulu mjini Washington, amesisitiza kuwa hatua ya kushindwa kuwadhibiti wahamiaji haramu, inawaumiza mamilioni ya wananchi wa Marekani na kwamba mzozo wa kibinaadamu na kiusalama unaongezeka katika mpaka huo uliopo kusini mwa Marekani.

Nia ya kujenga kuta za utengenishi badala ya madaraja ya makaribisho

Akiendelea Bwana Trump amesema wahamiaji haramu ndiyo chanzo cha kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kinachoingizwa nchini humo pamoja na uhalifu, huku akiendelea kuitetea sera yake ya kuujenga ukuta kwenye mpaka huo. Kadhalika amesema kuwa siku maafisa wa forodha na walinzi wa mpakani wanakabiliana na maelfu ya wahamiaji haramu wanaojaribu kuingia nchini Marekani. ''Kwa miaka mingi maelfu ya Wamarekani wameuawa kikatili na watu walioingia kinyume cha sheria nchini kwetu na maelfu ya maisha yatapotea tusipochukua hatua sasa. Huu ni mzozo wa kibinaadamu. Mwezi uliopita watoto wahamiaji 20,000 waliletwa kinyume cha sheria nchini Marekani, hilo ni ongezeko kubwa. Watoto hawa wanatumiwa na makundi katili ya uhalifu”,alisisitiza  BwanaTrump.

Kadhalika Bwana Trump amewataka wabunge wa chama cha Democratic kuridhia kiasi cha Dola bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika mpaka. Amewaalika Wanachama wa chama hicho kurejea tena Ikulu tarehe 9 Januari 2019 kwa lengo la kukutana naye,na kwamba ni vibaya kwa wanasiasa kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote. Bwana Trump amerudia wito wake wa kujengwa ukuta huo, akisema ni muhimu kwa ajili ya usalama. Katika mtazamo huo wa Bwana Trump juhudi za Maskofu wa Marekani, zinakabiliwa na changamoto kubwa, kwa maana kiongozi mkuu haoneshi utashi wa kuunganisha madaraja badala yake ni kujenga ukuta katika mipakani mwa nchi ili kuwazuia wageni, na zaidi anafunga masikio na kfumba macho juu ya dharura ya namna hiyo ya kibinadamu.

 

09 January 2019, 15:07