Tafuta

Vatican News
Kuna umuhimu wa mafunzo kwa makatekista katika kuboresha njia za uinjilishaji Kuna umuhimu wa mafunzo kwa makatekista katika kuboresha njia za uinjilishaji  (AFP or licensors)

Camerun:Kipaumbele cha mafundisho kwa makatekista!

Uinjilishaji ni mdogo kutokana na ukosefu wa makatekista.Katika Mkutano wa 42 wa Maaskofu katoliki nchini Camerun wamekabiliana na matatizo ya katekesi katika jamii,ya nchi ambayo imekumbwa na kipeo hasa kanda ya wanaozungumza kingereza.Askofu Kleda anawashauri kuwa na mazungumzo ya pamoja ili kuweza kuishi kwa amani na umoja

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Inahitaji kutazama kwa upya mitindo na zana za kusaidia kutekesi na ulazima wa kufanya utafiti na kugundua njia mpya kama zile za dunia ya kidigitali, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Hayo ndiyo yamejitokeza hivi karibuni mjini Yaounde katika Mkutano Mkuu wa 42 ya Baraza la Maaskofu Katoliki, kwa kuongozwa na mada ya Katekesi katika Kanisa la Cameruni:jambo la kujiuliza. Maaskofu Katoliki wameonesha ulazima kuwa na  jihudi kwawaamini wote  katika kutangaza Injili na ulazima wa kujifungulia neema ya Roho Mtakatifu.

Makatekista ni sehemu fungamani ya utume wa uinjilishaji

Katekesi ni sehemu fungamani ya utume wa uinjilishaji, wanasisitiza na utume ambao Kristo aliwakabidhi mitume wake, ambapo leo hii maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na walei lazima wajikite kwa dhati kuendeleza utume huo kwa watu wote wenye mapenzi mema. Licha ya juhudi hizo lakini, bado makatekista wanapungua daima na wale ambao wako tayari wanakosa zana muhimu za kufundishia. Wakatekumeni hawapati maandalizi ya kutosha, kwa maana hiyo hawana uthabiti wa kujua Mafundisho ya Meneno matakatikatifu ya Mungu. Makatekista wakati huo huo pia wanalalamika kwa maana wanahisi kuacha peke yao na mapadre kwa sababu ya kukosa mafunzo zaidi ili waweze nao kutangaza au kuhubiri Injili inavyotakiwa katika familia.

makatekista wanahitaji mafundisho yanayokwenda na wakati ili kuboresha njia za uinjilishaji

Naye Askofu Samueli Kleda, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Camerun amesema kuwa, juhudi za Katekesi kwa sasa zinazidi kudhoofisha mwaka hadi mwaka umuhimu wake ambao ni msingi,hasa kwa wakameruni ambao kwa sasa ni kipindi cha kisitisha kuuwana katika njia za kutafuta Amani. Katekesi lazima imfanye mtu atambue kuwa ni shule na mafundisho nyenye nguvu na uhai katika nyakati za mawazo ya kisasa na ili kuweza kutafuta namna moja ya kuishi kwa pamoja. Na zaidi, rais wa Baraza la Maaskofu wa Kamerun anasisitizia juu ya kusitisha kwa ghasia na kurudi katika mchakato  wa amani ili kujenga haki, mapatano, ushirikiano na mshikamano, mambo muhimu katika siasa ya huduma ya amani.

Wakati huo huo naye  Askofu Mkuu Jaen Mbarga wa Jimbo Kuu la Yaounde amesisitizia juu y anafasi ya Kanisa ambayo inapaswa kujikita kwa njia ya uinjilishaji pia kelezea nafasi iliyo nayo katekesi katika jamii ya sasa. Askofu ameonesha kwamba ni lazima kuzingatia hasa kipeo cha kanda ya wanaozungumza Kingereza katika nchi kwa maana nyingine ni kisema kuwa ni lazima kutambua namna ya kuishi kwa pamoja katika utofauti. Kwa mujibu wa Askofu Mbarga anabainisha kwamba kuna ulazima wa kufanya katekesi mpya ambayo inakwenda na wakati wa sasa.

Mkutano wa wa maaskofu mwaka 2020

Nje ya mada msingi ya mkutano huo wa mwaka, maaskofu pia wamejikita  kuzungumzia juu ya Sinodi ya vijana iliyomalizika mwezi Oktoba 2018 mjini Vatican, Siku ya kitaifa ya vijana iliyofanyika huko Garoua Camerun , shughuli za kichungaji kwa ajili ya familia na mwisho wametazama saula la uchaguzi mkuu wa Rais wa Camerun unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 Oktoba 2019, na pia kutangaza  tarehe ya Mkutano 43  ujao ambao utafanyika katika Jimbo la Obala 2020.

22 January 2019, 15:55