Tafuta

Vatican News
Askofu Olivier Schmitthaeusler, Msimamizi wa Kitume huko Phnom Penh, nchini Cambodia anahimiza familia zote kuwa wazi na mapokezi katika waraka wake wa kitume Askofu Olivier Schmitthaeusler, Msimamizi wa Kitume huko Phnom Penh, nchini Cambodia anahimiza familia zote kuwa wazi na mapokezi katika waraka wake wa kitume  (ANSA)

Cambodia:Familia ni ishara ya upendo wa jamii!

Kanisa la Cambodia limetangaza mwaka 2019 kuwa ni mwaka wa familia ambapo wanajikita kutazama kwa kina familia kama ishara ya upendo wakati wa kijiandaa katika Mwezi Maalum wa Kimisionari, kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko,mwezi Oktoba 2019

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kipindi chote hiki cha mwaka 2019 ni kitu gani tutafanya ili kuona mambo mazuri na mapya? Ndiyo tunaingia mwaka mpya  ambao umetolewa kwa ajili ya familia na mwezi Juni 2019 tutakuwa na mkusanyiko mkubwa wa familia kijimbo. Mwezi Oktoba utakuwa ni mwezi Maalum wa kimisionari, uliopendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko, mahali ambamo tutakuwa na tafakari kuhusu familia zetu zinaishi namna gani na zinawezaje kuwa ishara ya upendo wa Mungu kwa ajili ya jamii yetu. Ndiyo  mawazo ya Askofu Olivier Schmitthaeusler, Msimamizi wa Kitume huko Phnom Penh, nchini Cambodia aliyothibitisha katika barua yake ya kichungaji na kutangazwa na Shirika la habari za Kimisonari Fides. Katika waraka wake askofu anakumbusha uzoefu wanaouishi wanajumuiya wa Cambodia katika maono ya shughuli zao za kichungaji kwa mwaka 2019.

Uzoefu wa Noeli kwa kubatiza watoto, ishara ya dhati ya mtoto holini

Katika barua yake ya kichungaji inasema, katika mkesha wa Noeli waliadhimisha na kuwabatiza baadhi ya watoto ambao ni ishara nzuri na inayofanana na mtoto huyo aliyeko katika holi la wanyama. Familia ni jumuiya na Kanisa ndogo ya nyumbani. Wote wanaalikwa kukua katika familia kwa kutazama mfano wa Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu.

Familia lazima iwe na uaminifu, upendo wa kujitoa bila kubakiza, matumaini, maisha na hadhi

Kati ya mambo mengi ambayo amejikita kufafanua katika waraka wake na ambayo yanaelezea kwa jinsi gani maisha ya kila jumuiya ya wabatizwa inapaswa kujikita ameyataja mojawapo kuwa ni uaminifu, upendo wa kujitoa bila kubakiza, matumaini, maisha na hadhi. Kwa kusisitizia mifano hiyo, Askofu ametaja mifano mingine hai iliyopo katika maeneo mahalia kama vile watoto yatima ambao wanaachwa pembezoni mwa njia, watoto wasio kuwa na familia bila kuwa na upendo. Katika hilo, anawashukuru Shirika Wamisionari wa Upendo la Mama Teresa wa Kalkuta, ambapo watoto hao wamepata nyumba yenye joto na upendo mkamilifu. Kadhalika Askofu anaongeza kusema kuwa, “hii ndiyo nyumba yetu yaani familia kubwa”.

Uzoefu wa makaribisho ya wazee

Na kwa upande mwingine anasema: “kuna hata haja ya kufanya kumbukumbu kwasababu  katika siku ya Noeli, jumuiya nyingi zilikusanya wazee wengi pamoja ili kushirikishana furaha na kuwapa kidogo amani na utulivu”. Askofu anasisitiza, “ni jambo la kujenga zaidi kwa kutazama vijana wanahudumia wazee wanakaa nao na kuwasikiliza”. Kutokana na ushuhuda huo Askofu anaandika, “ mwaka huu ambao unangazia familia katika jimbo letu, kuna haja ya kutoa kipaumbele cha wazee wetu na kuwapa nafasi muhimu, kwa namna ya kwamba mizizi yao iweze kugeuka daima sehemu msingi ya historia na ambapo kizazi kipate kuwasikiliza, kuwalewa na kuwaliwaza”!

Matashi mema kutoka kwa waislam na wabudha na matarajio mema ya uwazi na makaribisho

Kadhalika Askofu pia hakukosa kuonesha mbegu njema ya kuishi kati ya dini na hata matashi mema ya amani ambapo anaandika kwamba, waislam na wabudha walikwenda kumtembelea kwa ajili ya kumtakia matashi mema ya Heri na sikukuu ya Noeli na kwa ajili ya jumuiya nzima. Hii ni kuthibitisha kuwa Noeli inatoa mwaliko wa amani na kutokana na hilo  anatoa wito wa kutazana maisha mapya katika kufanya hivi ndipo dunia inaweza kubadilika. Kwa mwaka 2019 ni matarajio ya Msimamizi wa Kitume kwa ajili ya Kanisa mahalia la Cambodia ya kwamna jumuiya inaweza kuwa wazi yaanui kufungua milango yake na kutoa matunda mema na watu wote watakuwa wenye furaha ya kukutana na kuwa familia kubwa yenye upendo na wenye makaribisho!

KANISA LA CAMBODIA
11 January 2019, 09:41