Maaskofu wa Burundi wametoa wito kwa viongoz wa serikali ya nchi kujikita kutafuta amani na mapatano Maaskofu wa Burundi wametoa wito kwa viongoz wa serikali ya nchi kujikita kutafuta amani na mapatano  

Burundi:Maaskofu wa Burundi wametoa wito wa amani na mapatano kwa 2019!

Katika Sikukuu ya Noel ina fursa ya kufungua mwaka mpya 2019, maaskofu wa Burundi wametoa ujumbe kwa ajili ya amano na mapatano katika nchi ambayo imeona vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 1993

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mwaka 2019 uwe wa amani na mapatano ndiyo matashi mema ya Maaskofu Katoliki wa Burundi katika ujumbe wao kwa waamini wakati wa sikukuu za Noeli na Mwaka Mpya 2019. Nchi ya Burundi bado inaendelea kupitia kipindi kigumu sana licha ya matumaini yalikuwa yameanza kuchanua mara baada ya kusaini mkataba wa Arusha mwaka 2000 ambao ulikuwa unataka kusitisha umwagaji damu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza kunako mwaka 1993.

Mkataba wa Arusha

Makubaliano yaliyokwema katika mkataba wa Arusha kwa namna ya pekee uliokuwa unarhusu kuunda kwa upya mahusiano na mshikamano wa utawala wa kidemokrasi na kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Mapatano, ulikuwa umeanza kuleta matumaini katika mioyo ya watu, ikiwa ni pamoja na wanasiasa na wazalendo wa kawaida. Katika ujumbe unasema, lakini mivutano iliyofuata mara baada ya hawamu ya tatu ya Rais Pierre Nkurunziza mwaka 2015, kwa ukiukwaji wa Katiba na hata Mkataba huo wa Arusha umesababisha kunyesha kwa vurugu na uchungu nchini Burundi.

Matarajio ya maaskofu kwa viongozi wa serikali kujibu wito wa amani na mapatano

Hisia za maaskofu wa Burundi wni kuomba  waamini wafikiri kama kweli kuna imani ya kutosha kati ya wanasiasa kukaa pamoja na kujadiliana ili kutafuta suluhisho la matatizo ambayo yanaikumba nchini? Na kama hili haliwezekani, ni wazi kwamba ni vigumu kuwahakikishia hata watu wa Burundi hasa wale ambao kwa miaka ya mwisho wamelazimika kukumbilia nchi za nje kutafuta makazi. Na hata ndani ya nchi, Maaskofu wanaandikia, hakuna wale ambao wanaishi kwa hofu na hawataki hata kusema kwa sababu wanaogopana hata wao kwa wao?

Swali jingine 

Je Tume yenyewe kwa ajili ya Ukweli na Upatanisho inabaki na uaminifu katika utume wake msingi wa kutafuta mapatano ya watu wote wa Burundi? Kutokana na maswali hayo, ndipo matumaini ya maaskofu wa Burundi ni kwamba  viongozi wa kisiasa na utawala mzima wanaweza kweli kujibu wito wa amani na mapatano kwa kufungua njia za majadiliano katika sekta mbalimbali za kijamii na wanahitimisha na ujumbe wao kwa kuomba Baraka ya Mfalme wa Amani iwashukie wote.

04 January 2019, 15:24