Tafuta

Vatican News
Lengo la Maombi kwa ajili ya umoja wa Wakristo ni kwamba  wote wawe wamoja Lengo la Maombi kwa ajili ya umoja wa Wakristo ni kwamba wote wawe wamoja  

Askofu Mkuu wa Kiorthodox wa Italia na Malta:Ukosefu wa kuungana ni kushindwa kiroho,kimaadilini na kijamii

Ujumbe wa Askofu Mkuu wa Kiorthodox wa Italia na Malta katika fursa ya Wiki ya kuombea umoja wa wakristo. Askofu Mkuu Gennadios anasema kuwa mbele yetu ipo wiki maalum kwa wahusika na jitihada hizo. Kwa dhati ni zawadi ya Mungu ambaye anataka kufikia lengo lake kuu,"ili wote wawe wamoja". Ukosefu wa muungano maana yake ni kushindwa kiroho, kimaadili na kijamii

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya Wiki ya kuombea umoja wa Wakristo tarehe 18-25 Januari 2019 siku ambayo inakwenda sambamba na Siku kuu ya uongofu wa Mtakatifu Paulo Mtume wa watu, Askofu Mkuu Gennadios wa Kiorthodox wa Italia na Malta ameandika ujumbe wake kwa wote.  Katika ujumbe huo anasema kuwa wote wanatambua ya kuwa kunzia tare 18-25 Januari duniani kote ni maadhimisho ya Maombi kwa ajili ya umoja wa Wakristo ikiwa na leongo kuu la kusaidia kiroho ili kuufikia utashi wa Mwokozi wetu Yesu Kristo: ili wote wawe wamoja ( Yh 17,21). Mbele yetu kuna wiki maalum, wiki iliyo jaa neema, furaha na matumaini, mbele yetu ipo wiki maalum kwa wahusika na jitihada hizo. Kwa hakika ni zawadi ya Mungu ambaye anataka kufikia lengo lake kuu la wote wawe wamoja (Gv. 17,21).

Inawezekana kushona dunia inayosumbuliwa na migawanyiko,mteso, mienendo mibaya, unafiki na masengenyo

Katika ujumbe huo ,anaangalia mada inayoongaza wiki isemayo tafuteni kuwa na haki ya kweli na mada ambayo inaangazia mwaka huu, jumuiya ya wakristo wa Indonesia. Katika Kitabu caha Kumbukumbu la Toarti sura ya 16, 16, tunakutana na mada ya Wiki ya kuombea umoja wa Wakristo. Hata ni maombi ya kiekumene ambayo mwaka huu yanaweka kiini cha Haki. Kwa mtazamo wa kitabu cha cha Kumbulkumbu la Torati kinamulika kwa dhati  kwa namna ya pekee katika nyakati hizi tunazoishi, katika dunia ambayo imejaa matatizo na ghasia ,katika jamii ambayo imkuwa na mitindo wa uadui na malumbano makubwa, ushindani na kashfa, vita na ukosefu wa heshima na upendo. Kitabu cha kutokana kinawakumbusha wote kuishi kama ndugu, watu wa Mungu, kuishi kwa umoja katika ushuhuda wa mshikamano na huruma ili kupata kushuhudia kuwa haki inaweza kweli kuwa nyenzo ya neema ya Mungu katika jambo dogo au kubwa la jamii inayoteseka, ambayo inasumbuliwa na migawanyiko, mteso, mienendo mibaya, unafiki na masengenyo.

Kiukweli haiwezekani kutojadili na kuhamasisha umoja, ambao ni wa lazima na wenye thamani, lakini hatua hii hawezekani ifanyike kwa wakristo tu, bali ni kwa ajili ya binadamu wote. Katika kutembea wakristo kati yao pekee, inawakilisha Yesu aliyegawanyika, ambapo inaondoa maana halisi ya mapenzi ya makuu ya Mungu kuwa: “ ili wote wawe wamoja” (Rej, Yh 17,21) na ni kashfa kwa waamini kuacha neno lisiweze kuwa na maana na kuligeuza kuwa dhaifu,na lisilokuwa na uwezo wa kuokoa na kumbe kinyume chake, Neno hilo ni haki na lenye nguvu, linatoa chachu ya upendo, ukweli na imani kwa ajili ya kushuhudia ukristo unaoaminiwa na kupendwa zaidi. Wakristo nchini Indonesia wameweza kupata mwanga na pendekezo la Neno kutoka Kitabu cha Kumbukumbu la Torati  ni  kutafuta kuwa kweli wenye haki na matumaini na kuzungumzwa kwa namna ya kweli hali yao na mahitaji yao. Wakristo wa nchi hiyo wanatafuta kugundua  roho hiyo maadhimisho ya mshikamano kati ya jumuiya za kikristo: “nawe utafurahi katika sikukuu yako, wewe, na wanao na binti zako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na mlawi, mgeni, na yatima, na mjane, anayeishi katika mji wako” (Rej Kumb. 16,14).

Wana wapendwa katika Kristo wanaalikwa wote 

Ukosefu wa muungano maana yake ni kushindwa kiroho, kimaadili na kijamii; aidha ni suala la kushindwa kuwa ishara ya upendo wa Mungu, nguzo ya watu wake. Inajulikana sana kuwa licha ya utofauti uliopo wa makabala, lugha na dini nchini Indonesia wameishi kwa mujibu wa msingi wa mshikamano na ushirikiano. Hivi karibuni, Askofu Mkuu wa Kirothodox anabainisha. Tumeadhimisha Siku Kuu ya Epifania ambayo imetujza roho zetu mwanga na neema kubwa ya manenosho halisi ya Utatu Mtakatifu.

 Pangoni Bethlehemu kimekuwa ni kutovu cha dunia, katika kuendeza amani na haki duniani. Inaunganisha yote na kutamani, kuhisi kuwa wote wanaweza kuishi kama ndugu. Amani na umoja ndiyo njia pekee ambayo tunaweza kukimbilia pamoja na yeye. Maombi ya kiekuemea ni ukweli wa daraja thabiti na thamani kwa ajili ya wakristo; Aidha anaelezea uzoefu wake wa neema aliyoipta kutokana na kuwa na fursa ya shuhudia wa matukio ya kihistoria ambayo yanajenga mnyororo wa kushangaza, uliopambwa na upendo na amani ya Bwana na Mungu.

 

 

18 January 2019, 16:23