Tafuta

Vatican News
Maaskofu Afrika ya Kusini wanapongeza taifa kwa kuongeza kiwango cha chini cha mshahara wa watu maskini Maaskofu Afrika ya Kusini wanapongeza taifa kwa kuongeza kiwango cha chini cha mshahara wa watu maskini  (ANSA)

Afrika ya Kusini:Kanisa linapongeza viongozi kuongeza kiwango cha chini cha mshahara!

Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini wanapongeza Rais na kabineti yake kuongeza kiwango cha chini cha mshahara kwa wafanyazi masikini uliotangazwa tarehe 1 Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tunatoa pongezi kwa rais na kabineti yake kwa sababu ya kutimiza hatua ya kwanza ya kuondoa utofauti mkubwa wa mishahara na kukabiliana na hali nyingi za matatizo ya wafanyakazi masikini. Ndiyo uthibitisho katika ujumbe wa Askofu Abel Gabuza wa Jimbo Katoliki la Kimberly na Rais wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kisini (SACBC) ujumbe uliofuatia mara baada ya kutangazwa kwa mswada mpya wa sheria tarehe 1 Januari 2019 unaohusu kiwango cha chini cha mshahara katika nchi ya Afrika ya Kusini.

Kulinda na kuheshimu sheria

Askofu Gabuza katika ujumbe wake anasisitiza kwapa licha ya ongezeko hilo, lakini vitivo vya kazi, lazima viendelee kujikita katika usimamizi na kulinda, ili sheria hiyo iweze kuheshimiwa na wote. Rais wa Haki na Amani wa Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini, pia anaonesha kuwa kiwango cha chini cha mshahara kitaifa, kinatazamia wafanyazi walio wadhaifu wapate Rand 3500 ( zenye thamani ya dola 242, kwa mwezi. Na ili mfanyakazi aweze kupata Rand 3500 anatakiwa kufanya kazi masaa 40 kwa wiki. Asilimia kubwa ya wafanyazi maskini wanafanya kazi masaa machache zchi ya 40 kwa wiki na hivyo hawapati kiasi ambacho kimekubaliwa na sheria.

Suluhisho na malumbano kati ya watoa ajira na wafanyakazi

Kwa mujibu wa Askofu Gabuza anaonesha kwamba Tume iliyokabidhiwa kudhibiti  kusuluhisho la malumbano kati ya watoa ajira na wafanyazi (Commission for Conciliation, Mediation and Arbitration - CCMA)  hawana uwezo wa kuridhisha maombi mengi ya huduma, ikiwemo hata maombi ya ajira za chini kitaifa. Na zaidi, uwezakano wa fedha katika ofisi za Tume ya Suluhisho na Kitivo cha ajira yanazidi kuwa matatizo hasa kwa wafanyakazi masikini wa wilaya za vijijini.

Hukosefu wa sheria yenye uhakika

Matatizo yaliyoongezeka ni kwamba sheria haikuzingatia kipimo kinachostahili kwa kutoa adhabu ya watoa ajira ambao wanatenda vibaya na kuendelea kuwanyonya watu zaidi walio maskini. Katika sekta nyingine, anathibitisha, watoa ajira wamewatangazia wafanyazi kuwa wanataka kupunguza masaa ya kazi kwa kiwango cha chini ya masaa 40 kwa wiki. Na wengine kama makampuni kwa namna ya kipekee wakulima wametangaza kuwa mwaka 2019 wataongeza kiwango cha kulipia umeme, maji na mikopo mingine. Mambo yote hayo mawili ni kutaka kupunguza kiwango hivho cha chi kitaifa cha mshahara

Ustawi katika mshahara

Mwisho kwa mujibu wa Tume ya Haki na amani wanathibitisha kuwa majadiliano juu ya kiwango cha chini cha mshahara kitaifa, unasaidia kuwa na umakini  na muhimu juu ya ustawi katika mshahara. Ustawi wa mshahara, uliotolewa wa  kiwango cha chini cha sheria kwa namna ya dhati unatoa fursa kwa mahitaji msingi ya wafanyakazi maskini na gharama kuu ya maisha ya chini na siyo katika mahitaji ya soko la kazi. Ustawi katika mshahara inahakikisha kuwa wafanyakazi masikini waweza kupata chochote hata kidogo kwa ajili ya kufanikisha maisha ya kawaida na yenye hadhi.

04 January 2019, 14:57