Cerca

Vatican News
Mahakimu wawili  ambao ni Roydah Kaona na Ammesie Banda Bobo,na jaji mmoja, Sylvia Munyinya ni wanawake watatu nchini Zambia wanaharakati wa kupambania haki za binadamu Mahakimu wawili ambao ni Roydah Kaona na Ammesie Banda Bobo,na jaji mmoja, Sylvia Munyinya ni wanawake watatu nchini Zambia wanaharakati wa kupambania haki za binadamu 

Zambia:Wanawake watatu wako mstari wa mbele kupambania haki za binadamu!

Wanawake watatu wakiwa mstari wa mbele katika mapambano ya haki za binadamu nchini Zambia na zaidi kupambana na aibu ya biashara ya binadamu, wamependelea kukutana na Baba Mtakatifu Francisko ili kushirikisha juhudi zao. Wamekutana naye wakati wa Katekesi ya tarehe 12 Desemba 2018

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wanawake watatu wakiwa mstari wa mbele, katika mapambano ya haki za binadamu ncini Zambia na zaidi kupambana na aibu ya biashara ya binadamu, wametaka kwa nguvu zote kukutana na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, ili kuweza kushirikisha utume wao wakiwa ni kama mahakimu wawili ambao ni Roydah Kaona na Ammesie Banda Bobo, pamoja na jaji mmoja, Sylvia Munyinya na ambao katika  kwa siku hizi wameshiriki mkutano Mjini Roma  kwa ajili ya kuleta mchango wao wa wanawake mahakimu wa Zambezi katika Jukwaa la Mahakimu wa Afrika juu ya mada ya  Biashara ya Binadamu na uhalifu wa kupangwa.

Sanamu ya kuchongwa inayowakilisha mtoto aliyekufa kwa bomu la atomiki

Imekuwa pia fursa mwafaka kwa namna ya pekee katika Ukumbi wa Paulo VI , wametoa zawadi ya sanamu ya mti wa kuchongwa inayowakilisha ujumbe wa historia ya picha iliyopigwa kunako mwaka 1945 na Joseph Roger Donnel, ambapo Baba Mtakatifu ameita  kuwa ni “ tunda la vita, kwa sababu inaonesha mtoto wa Japan amebeba mdogo wake aliyekufa, kufuatia na bomu la atomiki.   Msanii Nocola Gioba kwa ushirikiano na Shirika la Daraja la tatu  la Mtakatifu Francis wa Assis, walipendelea kutengeneza picha inayowakilisha “ roho ya mtoto mwathirika wa bomu la atomiki na ili kumpatia maisha”.

Baba Mtakatifu kubariki Sanamu  zinazoelekea huko Panama

Baba Mtakatifu Francisko, baadaye amebariki hata sanamu ambazo zinalekea huko Panama kwa ajili ya hija ya Siku ya vijana duniani. Kwanza ni picha ya Mtakatifu Maria wa Antiqua,  ambayo inapendwa na kufanyiwa ibada na watu wa Panama na kama ile ya Salus populi Romani ( yaani Maria Afya ya waroma). Ni ishara ya maana kubwa inayohamasisha maandalizi ya kiroho, lakini pia hata namna ya kutenda katika matazamo wa siku hiyo maalumu ya Kanisa, inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 22-27 Januari 2019.

Wasanii kuonjesha furaha itakayokuwapo huko Panama katika Siku ya Vijana duniani

Kadhalika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI, kulikuwapo na vijana karibia 50 wanamuziki ambao wanajihusisha zaidi na mambo ya kiutamaduni na usanii, wameweza kuonesha utangulizi wa hali  ambayo itakuwapo huko Panama katika Siku ya vijana duniani na ambao wametumbuiza wimbo uliotungwa kwa ajili ya siku ya vijana duniani.

ZAMBIA:WANAWAKE WATATU WATETEZI WA HAKI
13 December 2018, 15:27