Cerca

Vatican News
Askofu Msaidizi Benjamin Phiri wa Jimbo Katoliki la Chipata nchini Zambia anawashukuru jumuiya ndogo ndogo, vigango, makatekista na wanaparokia katika shughuli zao za kichungaji Askofu Msaidizi Benjamin Phiri wa Jimbo Katoliki la Chipata nchini Zambia anawashukuru jumuiya ndogo ndogo, vigango, makatekista na wanaparokia katika shughuli zao za kichungaji 

ZAMBIA:Faida za kuwa na Askofu msadizi Jimboni Chipata

Askofu Msaidizi Benjamin Phiri wa Jimbo Katoliki la Chipata nchini Zambia anawashukuru wanajumuiya ndogo ndogo, vigango, makatekista na wanaparokia kwa ujumla kwa sababu ya kuonesha jinsi gani wanavyokwenda pamoja kusaidiana katika shughuli za kichungaji jimboni humo

Sr Angela Rwezaula - Vatican

Jimbo Katoliki la Chipata ni moja ya majimbo nchini Zambia yenye kuwa na maaskofu wawili na wakristo wanayo fursa ya kuona maskofu wao mara kwa mara angalau mara moja kwa mwaka kupata huduma ya kichungaji kutoka kwa maaskofu wao. Badala ya kufanya ziara ya kuchungaji katika maparokia baada ya mwaka mmoja, miwili au mitatu. Maaskofu hao wanaweza kuwatembelea mara moja, mbili au tatu kwa mwaka, ambapo ziara hizo zinajikita katika fursa ya kutoa Sakramento ya Kipaimara au shughuli maalum ya vyama vya kitume vya kilei ambavyo vimebarikiwa ba Askofu.

Hayo yamefafanuliwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Chipata lililoko Mashariki ya nchi ya Zambia ambapo linachukua upana wa kilometa za mraba 6969,000 km. Licha ya wakazi kuwa wachache kwa mujibu wa Askofu msaidizi Benjamin Phiri, wakazi wake wannakaribia milioni mbili katka eneo ambalo linapakana na nchi ya Malawi. Kadhalika katika Jimbo la Chipata ni moja ya jimbo mahali ambapo kuna mbuga ya taifa Zambia, inayoitwa Luangwa South National Park. Watu wake wanategemea uchumi wao kutokana na ufugaji na kilimo, kwa maana hiyo hata Kanisa mahalia linategemea kilimo.

Iwapo kuna mavuno mengi pia ni wema wa Kanisa mahalia

Askofu msaidizi wa Chipata akizungumzia juu ya uvunaji wa mazao anasema, iwapo watu wanavuma mazoa mazuri, ina maana kwamba Kanisa mahalia wanakuwa na uchumi mzuri wa kuwasaidia, na iwapo mambo yanakuwenda kinyume na matarajio kama vile ukosefu wa mvua au mvua kunyesha sana, na kukiasa haya masoko ya mazao yao, matokeo hayo yanasikika hata katika Kanisa moja kwa moja na  kuathirika. Akiongeza Askofu Phiri anasema, hata hivyo ufugaji  wakati mwingina katika jimbo unaongeza nguvu kutokana na maendeleo na kwa sababu kilimo ndiyo msingi endelevu katika kuongeza nguvu muhimu ya masoko  Aidha  anaongeza kusema, wakazi wakatoliki, idadi yao ni karibia 400,000 katika karatasi. Anasema katika karatasi kwa sababu wakatoliki kwa hakika ambao ni wadau kusaidia Kanisa ni wachache kulinganisha na majimbo mengine.

Siri ya kukua kwa ukristo katika jimbo

Jumuiya ndogo ndogo za kikristo, vigango na makatekista wamechangia  kwa ajabu sana katika kukua wa ukristo,kwa namna ya pekee ukatoliki katika jimbo la Chipata. Kwa mujibu wa Askofu Benjamin ,anathibitisha kuwa, Jimbo la Chipata , linakumbwa na changamoto ya uchumi, japokuwa siyo jambo hasi linalohusika zaidi katika kukua kwa Kanisa katoliki, na kwa maana hiyo anapongeza sana Jumuiya ndogo ndogo, vigango vya paroki na nguvu za makatekista ambao kutokana na wao, ka dhati Kanisa linaendelea kukua kwa haraka. Jimbo linazidi kufuatilia na kuongoza Jumuiya ndogo ndogo za wakristo kama ilivyo hata majengo ya vigango. Na kila  kigango yupo kateksta wa kidumu na siyo wa kujitolea.

Kituo cha mafunzo ya makatekista wa kudumu, Chipata

Tangu mwaka 1954 huko Chipata kumekuwapo na kutuo cha mafunzo ya makateksita wa kudumu. Mafunzo hayo yanatakiwa  kujikita  kwa kipindi cha miaka miwili kufanya kozi ikiwa ni wanaume na wake zao pamoja na familia nzima. Kwa namna nyingine Askofu anathibitisha wote wawili mme na mke ni makatekista japokuwa ni mara chache, wanawake kuwa makatekista, walio wengi ni wanaume. Hata hivyo Askofu amebainisha kusema kuwa makatekista wanao uwezo wa kuongoza shughuli za Jumuiya ndogo ndogo  kama ilivyo pia kigangona kwa maana hiyo wao ni kama macho, masikio na mikono ya Paroko wa Parokia.

Kukua kwa Kanisa katika jimbo ka Chipata ndiyo ushuhuda kwa maana kwamba katika maparokia wanapoamua kujenga hili kuwakaribisha wote, leo hii kabla ya kuanza kulitumia, wanagundua kuwa tayari ni dogo na hivyo kanza kuwa na mpango wa kujenga Kanisa jipya.  Maparokia kwa sasa bado ni machache na mahali ambapi wanapokwenda kuadhimisha misa, mara nyingi jingo halitosho na hasa katika maadhimisho ya Ekaristi ya Askofu, mara nyingi misa zinafanyika nje ya Kanisa.

Mapadre wa jimbo

Jimbo Katoliki la Chipata kuna mapadre wa jimbo 70, na kati yao, 10-15 ni wamisionari, ambao wengi wanatoka katika Shirika la wamisionari wa Comboni, Wamisionari wa Marian Hill na ambao wanaendesha Kituo cha Kituo  cha kiroho cha Jimbo la Chipata. Kutokana na hiyo, mfumo wa jumuiya ndogo ndogo na vigano vimeweza kusaidia sana undelezaji wa shughuli za kichungaji. Kwa hiyo mfumo wa jumuiya ndogo ndogho na vigano vinasaidia sana uendeshaji katika jimbo ambamo linaunganisha karibia maparokia 34 amethibitisha Askofu Msaidizi wa Jimbo la Chipata nchini Zambia.

Wanaprokia kusaidiana na maaskofu katika shughuli za kichungaji

Akiendelea na ufafanuzi wake anasema, Askofu anapokwenda kutembelea parokia yoyote, kwa kawaida parokia inachangia ununuzi wa mafuta ya petroli na kwa namna hiyo anawashukuru sana wanaparokia kwa sababu wanaonesha jinsi gani wanavyokwenda mmoja ili kusaidiana, na kutokana na hilo, askofu anaamini kwamba iwapo watu wanaweza kuwezeshwa nguvu katika uchumi na iwapo wanaweza kuondokana  na tegemezi, jimbo linaweza kuamka, kuwa mbele, lakini iwapo watu wanahangaika kiuchumi na jimbo vilevile linapata taabu amesisitiza Askofu Phiri.

11 December 2018, 15:43