Tafuta

Vatican News
Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Argentina wanawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kutosahau mizizi ya kikristo wakati huu wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Argentina wanawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kutosahau mizizi ya kikristo wakati huu wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana  

Ujumbe wa Noeli wa Maaskofu Argentina:msisahau mizizi ya kikristo

Ni lazima pambania haki, kujenga urafiki kijamii na kuwa na mshikamano kwa masikini zaidi, wakati huo huo bila kusahau mizizi ya kikristo na kuwa na umakini wa kazi na elimu. Ndiyo mbiu ya ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Argentina kwa waamini na watu wenye mapenzi mema, wakiwatakia matashi mema ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mungu aliye jifanya mtu, anatukumbusha ni kwa jinsi gani kila mmoja anajitambua ubinadamu wake. Kwa maana hiyo tunaalikwa wote kupambania haki, kujenga urafiki kijamii na kuwa na mshikamano kwa walio maskini zaidi, wakati huo huo, tusisahau mizizi ya kikristo na kuwa na umakini wa kazi na katika elimu. Ndiyo maneno ya  ujumbe wa  Kamati  ya Baraza ya Maaskofu wa Argentina, katika ujumbe wao kwa waamini wote  na watu wenye mapenzi mema katika  kuelelea Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ambao umetolewa tarehe 11 Desemba 2018, mara baada ya kuhitimisha  Mkutano wao wa mwaka.

Bara la Amerika ya Kusini, nisayari ya ukosefu wa usawa wa kukithiri

Sikukuu ya mwaka huu nchini Argentina maaskofu wanaandika, inakutana na kipindi cha kipeo kikubwa cha uchumi ambapo watu walio wa mwisho katika jamii ndiyo  wanateseka sana kwa sababu ya matatizo ya kila siku wanayoishi. Hao ndiyo walio dhurika hata kwa upande wa usalama kwa sababu hawana rasilimali ya kuweza kujilinda. Zaidi , pia ukosefu wa usawa ni moja ya sababu za vurugu za kudumu katika nchi hiyo na ambapo Barani Amerika ya Kusini wanasema, ni sayari ambayo  kuna ukosefu wa usawa wa kukithiri.

Kadhalika ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Argentina unaendelea kuonesha juu ya  mabadiliko ya utumaduni kwamba: ndoto na mawazo ya vijana, hayaelekezi zaidi katika ulinzi na utetezi wa watu wenye kuhitaji zaidi; au katika matumaini ya kutengeneza familia au hata kuwa na ukaribu kwa masikini, kinyume chake, ni kuelekeza maono yao katika jinsi ya kutumia hovyo bila kikomo, ukiunganisha sambamba hata na  hali ya sintofahamu ya kuishi utofauti na kusahahu ile thamani muhimu za maisha.

Katiba ya Jamhuri ya Argentina iwe makini katika kazi na elimu

Licha ya hayo yote, maaskofu lakini wanasema: Tunaamini ukuu wa roho ya vijana na kwamba wanaweza kukataa misingi ya  mtindo hiyo ya maisha ambayo unaleta huzuni peke yake na kutotosheka. Wanahitimisha katika ujumbe wao, wakisema kwamba, katika miaka hii 35 ya kurudisha hali katiba ya Jamhuri yao, wanapendekeza  demokrasia ambayo haitasahau udhati na unyoofu wa mizizi ya kikristo na utamaduni ambao  unajikita hawali ya yote kuwa makini katika kazi na katika elimu.

12 December 2018, 13:58