Jumuiya ya wamonaki wa Taize hata mwaka huu wamekaribisha vijana wa Ulaya kusali na kutafakari kuanzia tarehe 28 hadi Mosi Januari 2019 jijini Madrid Jumuiya ya wamonaki wa Taize hata mwaka huu wamekaribisha vijana wa Ulaya kusali na kutafakari kuanzia tarehe 28 hadi Mosi Januari 2019 jijini Madrid 

Taizé:Ustaarabu wa makaribisho unawezekana!

Usisahau makaribisho ndiyo mada iliyochaguliwa na Jumuiya ya Taize kuongoza mkutano wa 41 wa vijana Ulaya utakaoanza tarehe 28 hadi Mosi Januari 2019 katika mji wa Madrid nchini Uhispania

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuanzia tarehe 28 hadi Mosi Januari 2019, vijana 15,000 wataunganika pamoja kufuatia mwaliko wa Jumuiya ya Taize huko Madrid nchini Uhispania katika Mkutano wa 41 wa vijana ULaya ambao mwaka huu unaongozwa na mada “tusisahau kukaribisha. Mkuu wa Jumuiya ya Taize, Frateli Alois akihojiana na shirika la habari la Sir amefafanua juu lengo la Mkutano huo, kwamba “ tunaishi nyakati ambazo hofu ndiyo inazidi kuongezeka,mipaka inafungwa. Lakini hakuna jamii yoyote inaweza kuishi bila imani na katika hija yetu ya matumaini katika ardhi hii inatakiwa kuwa  watu rahisi ishara ya matumaini. Na matumaini yenye ustaarabu wa makaribishouinawezekana”.

Ni matarajio ya kuwapokea vijana 15,000 katika mji mkuu wa Uhispania. Maparokia 170 na maelfu ya familia watafungua milango yao katika roho ya kukaribisha ili vijana hao katika siku hizo ili waweza kufanya uzoefu wa sala, ukimya na urafiki zadi ya mipaka. Makanisa mengi yaliyoko katikati ya mji wataweza kukaribisha vijana katika sala ya saa sita na baadaye jioni watakuwa wanakusanyika pamoja katika ukumbi mkubwa  wa maonyesho mjini Madrid kuendelea na uzoefu wa pamoja wa tafakari.

Kila mwaka Jumuiya ya Taize wanafanya uzoefu huo wa makaribisho

Frateli Alois akiendelea kufafanua anasema, kila mwaka wanafanya uzoefu huo wa kukaribisha katika fursa ya mikutano ya Vijana  Ulaya. Vijana wengi kwa kawaida ukaribishwa na familia kila mwaka ambapo familia hizo hufanya uzoefu wa furaha kubwa. Na kuhusu mada inayoongoza mkutano mwaka huu, Frateli Alois amethibitisha kuwa katika nyakati hizi hofu inazidi kuongezeka na wakati huo huo, mipaka inafungwa kwa maana hiyo wao wanataka kuwakumbusha kuwa kukaribisha ni mada msingi  na kiini cha Injili, Mungu anakaribisha daima, bila kujali hali. Kristo anabisha hodi mlangoni; anajiwakilisha kwetu sisi kama maskini, halazimishi bali anaomba akaribishwe; Yesu anaimarisha imani na anataka imani hiyo iweze kweli kuiishi hata katika maisha yetu na kuifafanua kwa matumaini kwa watu wengine. Hakuna jamii yoyote inaweza kuishi bila imani , kwa maana hiyo anasisitiza na kusema matumaini ambayo ni ustaarabu wa kukaribisha unawezekana.

Iwapo tunamfungulia mwingine kwa matumaini mara baada ya kushinda hofu ni kitu gani kinatukia?  

Frateli anathibitisha kuwa “Mara nyingi kuna ugunduzi wa kushangaza wa ukaribu wa watu ambao tulikuwa hatuwafahamu kabisa. Mfano kuna familia nyingi zitafungua milango ya nyumba zao. Hapo si kujali  lugha ya vijana watakao wakaribisha, lakini kwa hakika ni uzoefu wa kina wa kuweza kuwa zawadi ya mmoja na mwingine na kuweza kupokea chochota kilicho kizuri bila kutarajia. Ni kugundua kuwa wote tunahitaji mwingine; ndiyo uzoefu wa kina ambao unajitokeza hasa unaposhinda hofu.  Kwa hakika imani siyo ya kijinga, bali inayojikita juu ya ndoto kuu. Imani inaishi pamoja na kufanya uchaguzi wa wema dhidi ya ubaya na wakati huo huo imani inajua namna ya kuthubutu hata hatari ya kukaribisha mwingine, hata kama ni toafuati na mimi.

Maelfu na maelfu ya vijana wanafanya kila mwaka uzoefu huo wakati wa ufunguzi wa mwaka mpya wanatafuta nini

Maneno mawili ni ufunguo, kwanza ni sala na pili ni urafiki. Hapa vijana watagundua uzuri wa sala ya pamoja na hata maisha ya kina. Vijana 15,000 wataungana kwa pamoja katika karamu kwenye ukumbi wa maonyesho mjini Madridi. Ndiyo maana yake. kutakuwa na vipindi virefu vya ukimya wa pamoja. Katika hatua hiyo inakupelekea kujitafiti nafsi na kuungana na Kristo, kusikiliza Neno la Mungu, kuimba na kusifu kwa pamoja. Hiki ni kipindi mwafaka kinachotanguliwa na upatanisho ambao Yesu anatupatia, ni mpatano ya kikristo kati ya watu. Na ndiyo hiyo inapelekea urafiki, urafiki ambao unatambua kuvuka mipaka.

Frateli Alois alipata kuudhuria Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana, katika mwanga wa uzoefu huo, atawaleze nini vijana ambao watakusanyika Madrid?

Sinodi ilikuwa yenye uzoefu wa nguvu kwa upande wake. Kuna shauku ya kina ndani ya mpyo wake na wajumuiya nzima ya Taize mara baada ya Sinodi na kwa maana hiyo inazidi kuwa yenye nguvu zaidi, ili vijana nao waweze kugundua Kanisa kama mahali pa kujenga urafiki  kwa maana nyingine kama familia ya pili na hiyo iweze kutimilizika.

Ni lazima vijana waweze kukutana na watu ambao wawasikilize

Mapadre watawa na hata pia walei, wanaume na wanawake, watu ambao wanaishi kweli na uhai wa imani na wanatambua kuwasikiliza vijana, kuwa na utambuzi, bila kuwahukumu na kuwakatisha tamaa. Frateli Aloiz anafikiri kwamba, katika Sinodi wameweza kuonesha safari ya upyaisho ambayo lazima iwekwe katika matendo kuanzia sasa na kuendelea.

Ujumbe wa Mkutano huko Madridi ambao uanataka kuutua mwaka huu kwa Ulaya

 Frateli Alois akizungumzia juu ya ujumbe wa kutoa kwa Ulaya anasema,Kanisa linaweza kuwa sehemu ya ulimwengu mzima na ambayo kama wakristo tunao uwezekano, kuwajibika na kutafuta umoja wa dunia katika sura ya binadamu. Mkutano wa Madrid kwa vijana ikiwa vijana wanaoudhuria ni idadi kubwa, unaonesha kwamba vijana wanataka kwa dhati na wanatafuta umoja huo. Yote hayo yanahitaji kutembea kwa pamoja, kutambua mambo mengine ya kipekee ambayo yamo kwa kila watu, hata katika makanisa mengine tofauti. Mkutano wa Madrid unataka kuambia Ulaya kwamba inawezekana kabisa kutambuana jambo la kipekee na wakati huo huo ni katika  kufanya pamoja uzoefu wa kuishi  katika ulimwengu kwa pamoja.

 

27 December 2018, 13:00