Tafuta

Vatican News
AMECEA pamoja na Serikali za Ethiopia, Kenya, Uganda na Sudan wametoa mchango wa pamoja katika kufikia hatua ya kutia sahini ya makubaliano ya amani kati ya Sudan na viongozi wapinzani AMECEA pamoja na Serikali za Ethiopia, Kenya, Uganda na Sudan wametoa mchango wa pamoja katika kufikia hatua ya kutia sahini ya makubaliano ya amani kati ya Sudan na viongozi wapinzani  (AFP or licensors)

Sudan Kusini:Maaskofu wanaendelea kusali kwa ajili ya amani!

Kwa sasa inabidi kusali ili amani iweze kudumu katika nchi ya Sudan ya Kusini. Hayo yamethibitishwa na Askofu Erkolan Lodu Tombe wa jimbo la Yei na ambapo anawaalika wote kuanzia walei na makleri ili wasali bila kuchoka kwa ajili ya nchi hiyo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Mashariki  (AMECEA) pamoja na Serikali za Ethiopia na Kenya, Uganda na Sudan wametoa mchango wa pamoja katika kufikia hatua ya kutia sahini ya makubaliano ya amani kati ya Sudan na viongozi wapinzani. Kwa sasa inabidi kusali ili amani iweze kudumu, kwa mujibu wa Askofu Erkolan Lodu Tombe, wa jimbo la Yei akiwaalika wote kuanzia walei na macleri wote waendelee kusali bila kuchoka.

Tuendelee kusali ili kusitisha umwagaji damu na kujenga amani ya kudumu

Tunahitaji kusali na ni matumaini ya kwamba sala zinawezeka kusitisha umwagaji wa damu na kuunda amani ya kudumu kwa watu ambao wanateseka huko Sudan Kusini, anathibitisha Askofu katika vyombo vya habari za kimisionari Fides. Kwa mujibu wa Askofu Tombe, anasema, baada ya kutia sahini ya makubaliano ya amani kati ya serikali na viongozi wa upinzani iliyotiwa mwezi Agosti mwaka huu, hali kwa kiasi chake kuna  utulivu sehemu nyingi za nchi na hiyo imewajaza imani na matumaini kwa watu wengi, lakini hata hivyo Askofu PIA anabainisha kuwa bado kuna hali ambayo siyo nzuri ya wanamgambo ambao hawakutia sahini katika makubaliano hayo.

Katika baadhi ya maeneo, mara nyingi makubaliano hayo yanakiukwa na vurugu zinaendelea: lakini hiyo ni matukio ambayo yanaweza kutokae katika baadhi ya sehemu zote duniani. Ni lazima kukubali kwamba hakuna makubaliano ambayo ni makamilifu. Licha ya hayo yote, Askofu  Tombe anaonesha juu ya imani yake kwamba vita na vurugu vinaweza kusistishwa kabisa na kutoa fursa ya watu ili waweze kujenga maisha yao.

Viongozi kuomba ruhusa kwa maandishi ya kukutana na wanamgambo wapinzani

Pamoja na viongozi wengine wa dini wa Yei, Maaskofu wa AMECEA wamomba ruhusa ya kwa mandishi kwa upand ewa Serikali wa kuwaruhusu wao waende kukutana na wanamgambo ambao bado wanakataa mkataba huo na ili kuweza kuwahusisha katika mazungumzo na kuwasikiliza hoja zao na mara baada ya mazungumzo wataweza kueleza serikali na watu wake. Hadi sasa lakini bado hawajapata ruhus hiyo, kwa maana wao waliwajibu kuwa wako huru kwenda, lakini jambo hili kwa upande wa viongozi wa dini haikuwa inatosha. Maana wanahitaji uthibitisho wa maandishi, ni kwa njia hiyo tu, inaweza kuwahakikishia usalama kwa yule ambaye atajikita katika utume huo wa mazungumzo ya amani, amehitimisha Askofu Tombe.

12 December 2018, 15:12