Cerca

Vatican News
Vijana wa Papua Guinea walitembelea alipozaliwa Mwenye heri Peter ToRot, katekista wa Papua Guinea ambaye alikufa akiwa anatetea  imani yake, pia mtetezi wa ndoa Vijana wa Papua Guinea walitembelea alipozaliwa Mwenye heri Peter ToRot, katekista wa Papua Guinea ambaye alikufa akiwa anatetea imani yake, pia mtetezi wa ndoa 

Papua Guinea:tumeitwa katika utimilifu wa maisha na upendo!

Vijana 260 wameunganika kutoka katika majimbo katoliki nchini Papua Guine mpya ili kushiriki siku ya sala, tafakari na makuzi katika imani. Mkutano wa vijana ulianza tarehe 8-12 Desemba na ambao umeongozwa na mada:tunaitwa katika utimilifu wa maisha na katika upendo

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Mkutano wa kitaifa wa vijana uliofunguliwa tarehe 8-12 Desemba 2018 huko Vunapope katika Wilaya ya Britannia nchini Papaua New Guinea, wameongozwa na mada “tunaitwa katika utimilifu wa maisha na katika upendo. Na Vijana 260 wameunganika kutoka katika majimbo katoliki, ili kushiriki siku ya sala, tafakari na makuzi katika imani.

Shirika la habari katoliki za kimisionari Fides, linaripoti kuwa, Mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Maaskofu kwa ushirikiano na Jimbo Kuu la Rabaul katika mkutano ulifunguliwa rasmi kwa maandhimisho makuu ya Misa katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu huko Vunapope mjini Rabaul.  Katika siku za tafakari ni pamoja na mikutano na katekesi kuhusu maadhimisho ya maisha kwa njia ya Ekaristi na Sakramenti ya kutubio, lakini pia hata kujikita katika mafunzi ya maandalizi ya vijana katika sakramenti ya ndoa.

Naye Askofu Rolando Santos, CM, wa jimbo la Alotau – Sideia akiliambia shirika la habari za kimisionari Fides kuhusu mkutano huo, anathibitisha kwamba vijana wamepata tafakari juu ya imani, wito, maisha na upendo, kwa kushirikishana  historia za wito na  pia yeye binafsi  amewatia moyo ili  wasali na wasiwe na hofu ya kushuhudia Kristo. Pia vijana wametembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mtakatifu Maria ya Vunapope na kuonesha furaha yao katika kushirikisha na ambapo imekuwa ni sadaka yao.

Katika ya shughuli mbalimbali ambazo zimeanzishwa mapema wakati wa kuandaa mkutano huo, ni pamoja na kushiriki hija huko Rakunai , ambapo wote wameweza kutembea eneo alipozaliwa mfiadini, Mwenye heri Peter ToRot, katekista wa Papua Guinea ambaye alikufa akiwa anatetea  imani yake kwa Mungu na mtetezi wa ndoa. Askofu Rochus Tatamai, wa jimbo katoliki la Kavieng akizungumza na vijana, amewasimulia juu ya maisha ya mwenye heri na kumtafsiri kuwa ni kama mtu mnyenyekevu na mtakatifu tangu akiwa mtoto. Mkutano wa vijana umalizika tarehe 12 Desemba 2018 kwa Misa Takatifu ya kushukuru.

12 December 2018, 14:03