Kila mtu anahusika na kile anachoandika na kuchapisha. Usitumie meneno na lugha ya ghafla katika vyombo vya habari kijamii. Ni lazima kutunza maadili na kuhepuka habari za kughushi Kila mtu anahusika na kile anachoandika na kuchapisha. Usitumie meneno na lugha ya ghafla katika vyombo vya habari kijamii. Ni lazima kutunza maadili na kuhepuka habari za kughushi 

Pakistan:Warsha juu ya kuhamasisha ukweli na kupambana na habari za kughushi!

Kila mtu anahusika na kile anachoandika na kuchapisha hivyo usitumie meneno na lugha ya ghafla katika vyombo vya habari kijamii. Hayo yamesemwa na Padre Qaisar Feroz, ndugu mdogo mkapuchini ( OFM Kap), ni Katibu Mkurugenzi wa Tume ya Baraza la Maaskofu ya Mawasiliano nchini Pakistan katika warsha ya wahusika wa vyombo vya habari Katoliki

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Usitumie maneno na lugha ya ghafla katika vyombo vya habari kijamii. Ni lazima tuendelee kutunza maadili kijamii na maadili kwa umma kwa kile tunacho andika na kuchapisha.  Kila mtu anahusika na kile anachoandika na kuchapisha. Hayo yamesema na Padre Qaisar Feroz, Ndugu mdogo mfranciskani mkapuchini ( OFM Cap), ambaye ni Katibu Mkurugenzi wa Tume ya Baraza la Maaskofu yaa Mawasiliano nchini Pakistani, wakati akitoa hotuba yake katika warsha kuhusu vyombo vya habari vya Kikristo, iliyoandaliwa siku za hivi karibuni na Tume ya Mawasiliano kijamii kwa jimbo Kuu la  Karachi kwa kushirikiana na Caritas, Signis ya Pakistan na Huduma ya Radio Veritas -Asia ya  Kiurdu.

Kukuza amani na huduma ya ukweli katika jamii

Warsha hiyo ilikuwa na lengo la kuongeza uelewa kati ya wahudumu wa vyombo vya habari ili kuweza kufanya kazi kwa amani. Na kwa maana hiyo, Padre Feroz amesema kuwa, kambi za vyombo vya habari  kijamii vina ushawishi mkubwa sana na vimeenea. Ni jukumu lao wote kama wana habari kuweza kuvitumia  kama zana za kueneza na kukuza maadili ya amani kijamii na ya kidini na maelewano kijamii kupitia vyombo vya habari kijamii; kuvitumia vyombo hivyo kwa ajili kujenga mahusiano mazuri na watu na kuunda vikundi ambavyo vinaweza kusaidia kuendeleza amani katika maisha ya mtu binafsi, katika miji na katika jamii. Kadhalika ameongeza kusema wote kama wadau na waandishi wanapaswa kukuza heshima ya maisha; kuhudumia ukweli na kukuza ushirikiano kati ya wanadamu, badala ya kukuza habari za kughushi, kueneza ujumbe usiofaa au picha zinazoharibu  amani katika jamii.

Kwenda kinyume na utamaduni wa kulaghai

Katibu Mkurugenzi wa Mawasiliano pia amethibitisha kwamba, kumezuka hata uhuru wa nguvu za vikosi vya kisiasa katika kulinda na kukuza ubinadamu, kuheshimu thamani ya kimaadili na kufanya kazi kwa kuboresha jamii. Warsha hiyo umechangia kuimarisha na kuhamasisha ujuzi, kuboresha ujuzi wa uandishi wa habari na kutafakari juu ya mantiki nzuri na athari mbaya za vyombo vya habari kijamii katika jamii. Na hatimaye padre Feroz amekazia juu ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko alio utoa wakati wa kuadhimisha Siku ya Mawasiliano Dunia 2018, iliyoongozwa na mada: “Habari za kughushi na uandishi wa amani”; kwa maana hiyo Padre Feroz amewaalika washiriki wa warsha hiyo kupambana na habari za kughushi na pia kupinga utamaduni wa ulaghai.

Wakristo ni wahamasishaji wa ukweli

Amehitimisha kwa kusema: “Ukweli huongoza katika kufikia amani, hivyo tunapaswa kuwa wahamasishaji wa ukweli kwa njia ya maandishi yetu na kutuma. Kama Wakristo ni wajibu wa kila mtu kuendeleza uhamasishaji na kusaidia kukuza utume wa Kristo na Injili yake ya amani na udugu”.

14 December 2018, 14:58