Cerca

Vatican News
Maaskofu wa Nigeria wanahukumu vikali, makuhani au watawa kujiingiza katika masuala ya siasa wakati wa uchaguzi, kwa mujibu wa Kanuni ya Sheria ya Kanisa Maaskofu wa Nigeria wanahukumu vikali, makuhani au watawa kujiingiza katika masuala ya siasa wakati wa uchaguzi, kwa mujibu wa Kanuni ya Sheria ya Kanisa 

Nigeria:Kanisa Katoliki halifanyi kazi ya kampeni ya uchaguzi!

Kwa mujibu wa Maaskofu wa Nigeria, mara baada ya kutokea ugonvi katika kituo cha kuabudu cha Enugu Nigeria kati wa mwanzilishi wa kituo hicho Padre Ejike Mbaka na Peter Obi mgombea kiti chaurais i kwa bendera ya Chama cha kidemokrasia (PDP) wanahukumu tendo hili vikali na kuonya makuhani na watu wote wenye wakfu kutokuwa upande wowote wa kisiasa

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa Waraka uliopewa jina la “Uchaguzi Mkuu 2019:Kanisa Katoliki linabaki bila kujihusisha na upande wowote wa chama cha kisiasa. Kwa mujibu wa Maaskofu wa Nigeria, mara baada ya kutokea ugonvi katika kituo cha kuabudu cha Enugu Nigeria kati wa mwanzilishi wa kituo hicho, Padre Ejike Mbaka na Peter Obi mgombea kiti cha urais kwa bendera ya Chama cha kidemokrasi (PDP).

Makuhani na watawa hawawezi kushiriki katika kampeni za uchaguzi

Kwa mujibu wa Kanuni ya Sheria, makuhani na watawa hawawezi kushiriki katika kampeni za uchaguzi kwa ajili ya hili au mwanasiasa. Hayo yameelezwa na Maaskofu wa Nigeria, kwa saini iliyotiwa na Padre Ralph Madu, Katibu Mkuu wa Sekretarieti Katoliki ya Nigeria (CSN) waraka uliopewa jina:“Uchaguzi Mkuu 2019: Kanisa Katoliki linabaki bila kujihusisha na ubande wowote wa chama cha kisiasa.

Kuhukumu vikali vurugu zilizotokea

Tamko hili, limetolewa kwa maandishi muhimu kutokana na vurugu mara baada ya kutokea ugonvi katika kituo cha kuabudu cha Enugu nchini Nigeria kati wa mwanzilishi wake Padre Ejike Mbaka na Peter Obi mgombea kiti cha Urais katika Uchaguzi kwa bendera ya Chama cha kidemokrasi (PDP). Maaskofu wa Nigeria, wanahukumu vikali sura mbaya hiyo na aibu iliyojitokeza katika Kituo cha Kuabudu na mahali ambapo video nyingi zilizorekodiwa zinazidi kuzunguka katika vitandao ya kijamii. Maaskofu wanathibitisha bila kuficha kuwa tukio hili halikubaliki na Baraza la Maaskofu wa Nigeria.

Uchaguzi uwe uhuru, wa haki na usawa

Katika taarifa waliyoiandika Maaskofu wanasema: “Tunasisitiza msimamo wetu: Kanisa Katoliki nchini Nigeria, kama ilivyoelezwa waziwazi katika maelekezo ya tarehe 7 Agosti 2018, linabaki bila kuingilia kati juu ya masuala ya kisiasa na wala kusaidia chama cha aina yoyote cha kisiasa”. Wanaongeza Maaskofu kuandikia kwamba: “Wasiwasi wetu unaobaki ni kwamba kuwepo na mchakato mzuri wa uchaguzi wa amani, huru, usawa, wa kuaminiwa na wenye haki; na kwamba serikali ya kidemokrasia itakayochaguliwa ihakikishe kunakuwapo na amani, haki, usawa, maendeleo na uhuru wa kidini kwa ajili ya manufaa ya wote”.

Hakuna kampeni za uchaguzi katika maadhimisho ya liturujia

Katika hitimisho lao Maaskofu wanaandika kuwa: Wakati Jimbo la Katoliki la Enugu, mahali ambapo Padre Mbaka anatokea, wapo wanachukua hatua zinazofaa kufuatia na ajali hiyo, maaskofu wanasema : “tunaarudia  kuthibitisha kwa makini kwamba, hakuna padre yoyote  mkatoliki  au mtu aliyeweka wakfu anaweza kujihusisha katika sehemu ya mapambano ya kisiasa, kwa kutii Kanuni ya Sheria. Aidha, ni marufuku kutumia maadhimisho ya liturujia katika kutekeleza kampeni za kisiasa.

15 December 2018, 10:13