Baraza la Maaskofu Marekani wametenga karibu dola 800,000 kwa ajili ya misaada saba ya mipango ya ujenzi katika maeneo yaliyoharibiwa na majanga ya asili huko Haiti, Mexico na Peru Baraza la Maaskofu Marekani wametenga karibu dola 800,000 kwa ajili ya misaada saba ya mipango ya ujenzi katika maeneo yaliyoharibiwa na majanga ya asili huko Haiti, Mexico na Peru 

Marekani:Maaskofu watoa msaada kwa ndugu wa Amerika ya Kusini!

Dola milioni 4 za kimarekani zimetengwa na Baraza la Maaskofu Marekani kwa ajili ya shughuli za Kanisa la Amerika ya Kusini ikiwa pia ni fedha kwa ajili ya shughuli ya kichungaji kwa vijana, katekesi na kusaidia kuinua watu katika maeneo yaliyokumbwa na majanga ya asili kama vile Haiti, Peru na Quba

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani (USCCB) wametenga dola milioni 4 za kimarekani kwa ajili ya shughuli za Kanisa la Amerika ya Kusini, hizo ni fedha kwa ajili ya shughuli za kichungaji kwa vijana, katekesi na kusaidia kuinua watu katika maeneo yaliyokumbwa na  majanga ya asili. Kwa mujibu wa taarifa kutoka habari za kimisionari Fides, kamati ndogo ya Baraza la Amerika ya Kusini katika Baraza la Maaskofu wa Marekani (USCCB), katika mkutano wake wa tarehe 10  Novemba 2018 uliofanyika huko Baltimore, imetenga zaidi ya dola milioni 3.2 kwa ajili ya kufadhili  misaada 173 ili kusaidia shughuli za kichungaji katika Kanisa la  Amerika ya Kusini na Caribbean; na karibu dola 800,000 kwa ajili ya misaada saba ya mipango ya ujenzi katika maeneo yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi huko Haiti na Mexico na kwa vimbunga vya Matthew, Maria na Irma.

Fedha kwa ajili ya miradi mingi ya mafunzo, kichungaji na ujinjilishaji huko Amerika ya Kusini

Kadhalikataarifa hiyo inaeleza kuwa wametenga fedha kwa ajili ya miradi ambayo inatakiwa kufanyika katika nchi kadhaa za kanda hilo. Kwa mfano, katika miradi ya Cuba na Equador imefadhiliwa kusaidia kuundwa mradi kwa ajili ya mafunzo ya  watu walei  na viongozi wa Kanisa, wakati  nchini Uruguay na El Salvador, fedha zimepangwa kwa ajili ya mipango ya uinjilishaji na katekesi. Mpango mingine inayotarajiwa ni kusaidia watu wa asili katika nchi ya  Brazil na Venezuela. Kamati ndogo pia imepitisha rasilimali muhimu kwa ajili ya msaada wa vijana katika huduma ya kichungaji na gharama ya usafiri kwa ajili ya washiriki watakaoudhuria Siku ya Vijana Duniani, itakayotarajiwa kufanyika nchini Panama  kuanzia tarehe 22 hadi 27  Januari  2019, kutoka nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini, ikiwa ni pamoja na Haiti, Peru na Quba na ili waungane pamoja na vijana wenzao kufanya maadhimisho hayo muhimu katika maisha yao.

Shukrani kwa wakatoliki wa Marekani kwa sababu ya ukarimu wao

Mkusanyo wa sadaka kwa Kanisa nchini  Amerika unalengo kubwa sana kwa ajili ya watu wa kanda na kwa namna ya pekee katika  mataifa yaliyo athirika. Hayo yamethibitishwa na Askofu Mkuu Paul Dennis Ettinee, wa Jimbo Kuu la  Anchorage ambaye pia ni Rais wa Kamati ya makusanyo ya sadaka Kitaifa ya Baraza la Maaskofu Marekani. Kutokana na hilo, Askofu mkuu anachukua fursa hiyo kuwashukuru kwa dhati Wakatoliki wote nchini  Marekani kwa ukarimu wao na mshikamano kwa ajili ya dada na kaka  hao wa Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean.

Jumapili ya nne ya mwezi Januari na mkusanyo maalum wa USCCB

Sadaka hizo kwa ajili ya huduma ya kichungaji zinapatikana kutokana na mkusanyo wa fedha wa mwaka  kwa ajili ya Kanisa la Amerika ya Kusini na ambao utafanyika katika majimbo mengi katoliki ya Marekani katika  siku ya Jumapili ya nne ya Mwezi Januari na wakati wa kipindi cha dharura na ujenzi, Baraza la Maaskofu wa Amerika (USCCB), uhamasisha makusanyo maalumu kwa ajili hiyo.

14 December 2018, 15:21