Tafuta

Vatican News
Kanisa la Malaysia, Singapore na Brunei wanajiandaa kuishi Mwaka maalum wa kimisionari, kuanzia sikukuu ya Epifania 2019 hadi mwezi Maalum Oktoba 2019 wa kimisionari Kanisa la Malaysia, Singapore na Brunei wanajiandaa kuishi Mwaka maalum wa kimisionari, kuanzia sikukuu ya Epifania 2019 hadi mwezi Maalum Oktoba 2019 wa kimisionari 

Malaysia:Kanisa linajiandaa kuishi mwaka maalum wa kimisionari!

Kufuatia na tangazo la Baba Mtakatifu kuchagua mwezi Oktoba 2019 kuwa Mwezi Maalum wa Kimisionari, Kanisa Katoliki la Malaysia, Singapore na Brunei, wamependekeza kwamba katika Sikukuu ya Epifania 2019 wanafungua Mwaka Maalum wa Kimisionari ili kuuhitimisha mwaka huo katika mwezi Maalum wa Kimisionari

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa Katoliki la Malaysia, Singapore na Brunei wamependekeza kwamba katika Sikukuu ya Epifania 2019 watazindua Mwaka Maalum wa Kimisionari, ambao utahitimishwa katika maadhimisho ya Mwezi Maalum Oktoba 2019 wa kimisionari uliotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko, ambapo ni matumaini ya Papa kuwa, Jubilei ya miaka 100, tangu kuchapishwa kwa Waraka wa Kitume “Maximum illud, Mwezi Oktoba 2019 unaweza kuwa  ni kipindi cha sala pamoja na shuhuda mbalimbali za watakatifu na wafia dini. Maandalizi ya maadhimisho ya kipindi hiki maalum cha kutangaza na kushuhudia Injili kinaweza kusaidia Kanisa daima kuwa katika mchakato wa kuinjilisha. Askofu Sebastian Francis wa jimbo la Penang na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Malaysia, Singapore na Brunei, amethibitisha  kuzindua mwaka huo katika habari zilizo pokelewa na Shirika la habari za kimisionari Fides. Kama walivyopokea taarifa, ni kwamba katika majimbo ya Malaysia, Singapore na Brunei jumuiya zote za kikristo kwa sasa zimeanza maandalizi ya Mwaka maalum.

Mafunzo kwa wahudumu wa kichungaji katika maandalizi ya mwaka maalum

Taasisi ya Uinjilishiji mpya huko Malaysia, hivi karibuni, imetoa mafunzo maalum ambayo yalikuwa yanawalenga viongozi katoliki, wakiwepo hata maaskofu Sebastian Francis wa Penang na Bernard Paul wa Malacca-Johore. Katika Mafunzo hayo wameudhuria washiriki hamsini, kati yao ni viongozi wahudumu wa kichungaji na wahusika wa jumuiya mbalimbali za Kanisa katoliki.

Kwa asili Kanisa ni la kimisionari

Aliyelisha mada  na kuonesha mantiki msingi ya Mwezi wa Kimisisionari ni Padre Victor Louis, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kipapa ya Shughuli za kimisionari. Mkurugenzi huyo amekumbusha lengo kuu la Maadhimisha hayo kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko.  Hawali ya yote amesema kuwa: Uinjilishaji ni kupokea jibu la kutumwa kwa Yesu aliposema: “Nendeni duniani kote, mkatangaze Injili kwa kila kiumbe (Mk 16,15). Kutii wito huo wa Bwana, siyo kufanya uchaguzi kwa ajili ya Kanisa, bali hiyo ndiyo shughuli yake msingi kwa maana asili ya Kanisa ni la kimisionari na Kanisa lipo kwa ajili ya kuinjilisha. Uinjilishaji kwa hakika ni neema na wito wa dhati wa Kanisa, amesisitiza Mkurugenzi. Katika Kipindi cha mafunzo kwa siku tano, liturujia maalum imewaangazia zaidi na kuwathibitishia kuwa kila mkiristo kwa neema ya ubatizo anaitwa kuinjilisha. Washiriki wa Semina hiyo ya mafunzo pia wameweza kutembelea hata hospitali, katika kituo biashara na katika nyumba za wazee ili kufanya uzoefu wa uinjilishaji wa barabarani.

Mwezi Maalum wa Oktoba 2019

Mwezi maalumu wa Oktoba 2019 unaadhimisha Jubilei ya Miaka 100 tangu kutangazwa kwa Waraka wa Kitume “Maximu Illud” na Papa Benedikto XV(1919 kwa maana hiyo  inaongzwa na kauli mbiu Tuliobatizwa na kutumwa:Kanisa la Kristo katika utume duniani. Lengo lake ni kutaka kuhamaisha kwa kiasi kikubwa uelewa wa Missio ad gentes yaani  utume wa watu wote  na kuwa na upyaisho wenye kuwa na chachu kuu ya kubadilisha shughuli za kimisionaria katika Kanisa. Waraka wa “Maximu Illud” unakazia umuhimu wa maandalizi ya wamisionari na wakleri katika maisha na utume wa Kanisa; umuhimu wa mapadre, watawa na waamini walei kuchuchumilia utakatifu wa maisha na utume wa Kanisa kwa ujumbla. Waamini walei wanashirikishwa kwa namna ya pekee utume wa kimisionari kwa njia ya sala; kwa kusaidia kutegemeza miito mbali mbali ndani ya Kanisa.

 

13 December 2018, 12:51