Vatican News
Viongozi wa dini ya Korea ya Kaskazini wametuma heri na baraka ya sikukuu ya Noeli kwa ndugu kaka na dada wa Korea ya Kusi Viongozi wa dini ya Korea ya Kaskazini wametuma heri na baraka ya sikukuu ya Noeli kwa ndugu kaka na dada wa Korea ya Kusi 

Korea Kaskazini yatuma matashi mema ya Noeli kwa Korea kusini!

Baraza la Madhehebu ya kidini nchini Korea ya Kaskazini inayounganisha madhehebu matano yaliyokubaliwa na utawala nchini humo limetuma ujumbe kwa njia ya video, ili kuwatakia matashi mema ya amani na matarajio katika sikukuu hizi za Noeli kwa ndugu kaka na dada wa Korea ya Kusini

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wawakilishi wa madhehebu matano ya dini yaliyokubaliwa na Utawala wa Korea ya Kaskazini wametuma ujumbe kwa njia ya video, ili kuwatakia matashi mema ya Noeli wakristo wa Korea ya Kusini. Baraza la majadiliano ya Kidini ya  Korea ya Kaskazini inayounganisha dhehebu la wabudha,waislam watau, wakatoliki na waluteri, wanawatakia amani na matarajio mema ndugu kaka na dada wa Korea ya kusini na kuomba baraka ya Mungu ili waweze  kutembea pamoja  wakiwa wameshikana mkono kuelekea katika umoja wa kweli na amani.

Video inaonesha picha mblimbali za olimpiki

Ujumbe wao kwa njia ya video, unatanguliwa kuonesha kwanza picha mbalimbali za matukio la Olimpiki huko Pyeongchang na Mkutano Mkuu  kati ya viongozi wa korea mbili kwa mwaka 2018. Na baadaye Mkuu wa Baraza la mazungumzo ya kidini, Kang Ji-young anasema “ ninataka kuwatumia ujumbe wa amani wakati wa Noeli, kaka na dada wa Korea ya Kusini. Ni matarajio ya kwamba tunaweza kutembea pamoja na baraka ya Bwana Yesu ili iweze kutupeleka mbele tukiwa tumeshikana mkono kwa mkono kuelekea amani na umoja. Video hiyo imekubaliwa na ofisi kuu ya waziri umoja  huko Seoul na ambayo imetumwa kwa wawakilishi wa madhehebu mengine ya dini nchini Korea ya Kusini.

Sheria za Korea ya Kaskazini kwa upande wa makanisa

Nchini Korea ya kuskazini wanatoa ruhusu ya kuadhimisha ibada ya marehemu kiongozi Kim Jong II na baba yake Kim II Sung. Utawala wa nchi hiyo daima umekuwa ukijaribu kuweka vizingiti vya uwepo wa dini kwa namna ya pekee ya wabudha na wakristo na kuwalazimisha waamini wajiandikishe katika orodha ya mashirika yanayothibitiwa na Chama cha nchi. Adhabu na mateso makali mara nyingi yamekuwapo dhidi ya waamini ambao hawajiandikishi na wale ambao wanajikita hai katika shughuli za kimisionari. Tangu kuanzishwa kwa serikali ya mabavu ya kikomunisti kunako mwaka 1953 wamepoteza wakristo karibia 300,000 na hakuna mapadre na watawa kwa maana waliuwawa wakati wa mateso.

Serikali iliruhusu ujenzi wa Kanisa la Kiorthodox 2006

Katika nchi hiyo kuna aina 51 za maisha ya kijamii iliyotolewa na uamuzi wa serikali, hususani wale ambao hawaamini dini na ambao wanathibitiwa na serikali wako nafasi ya mwisho; hawana fursa ya kujifunza au kuwa na kazi na wala kupokea mahitaji ya chakula na daima ni waathirika wa vurugu na kuonewa. Pyongyang inathibitisha kuwa na uhuru wa dini, lakini inayolindwa na Katiba na  utawala rasmi ambao ni karibia wabudha 10,000, waluteri 10,000 na wakatoliki 4,000. Kwa idadi  hiyo, serikali inasema ni waamini walioandikwa katika mashirika yanayojulikana. Hata hivyo huko Pyongyang walijenga makanisa matatu, moja la wakatoliki na mawili ya waluteri kwenye miaka ya 80. Kutokana na uwepo wa mahusiano mema na ofisi ya balozi wa Urusi nchini Korea ya Kaskazini, serikali pia iliruhusu ujenzi wa Kanisa la Kiorthodox kunako mwaka 2006.

Hata hivyo katika makanisa hayo kwa mujibu wa mashuhuda walioweze kutembelea makanisa waliona kuwa wanafanya propaganda za utawala wa mabavu. Kwa maana ndani ya makanis hayo kiongozi wa kanisa anafikiriwa kuwa rafiki wa Rais Kim Jong II. Katika Kanisa Katoliki hakuna padre yoyote anayefanya kazi, badala yake waamini wanakusanyika katika sala tu ya pamoja mara moja kwa wiki.

28 December 2018, 12:36