Tafuta

Vatican News
Kardinali John Njue anasema uwepo uwazi wa upelelezi juu ya kifo cha  Padre John Njoroge Muhia Kardinali John Njue anasema uwepo uwazi wa upelelezi juu ya kifo cha Padre John Njoroge Muhia 

Kard.Njuwe:Uwazi unahitajika kuhusu kifo kwa Pd.John Njoroge

Kardinali John Njue Askofu Mkuu wa Nairobi wakati wa mazishi ya Padre John Njoroge Muhia aliyeuwawa tarehe 10 Desemba 2018 ametaka uwepo uwazi wa upelelezi juu ya kifo hicho ili kuwafanya wazazi ndugu na marafiki kuwa na utulivu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni lazima kufafanua kwa uwazi ya juu ya tukio la kuuwawa kwa Padre. John Njoroge Muhia”. Hayo yametakwa na Kardinali John Njue Askofu Mkuu wa Nairobi wakati wa mazishi ya Padre aliyeuwawa tarehe 10 Desemba 2018 mahali ambapo vyombo vya habari vinasema janga hilo limetokana na wizi wa barabarani.

Kardinali anaomba ufanyike uepelelezi uli wazi

Wakati wa mahubir yake Kardinali Njuwe ya mazishi ya Padre Muhia, ametaka uwazi wa upelelezi ujulikane na kwamba matukio yote  yaweze kuwekwa mbele ya familia yke marehemu na ili wapate faraja. Akiwageukia wazazi na ndugu jamaa wa marehemu aliyeuwawa, Kardinali Njuwe wa Jimbo Kuu katoliki Nairobi, amesema kuwa kumpoteza mtoto kwa mtazamo wa kibinadamu ni moja ya hali nzito na ya uchungu ya kukabiliana nayo kwa namna ya pekee kwa kuzingatia kifo cha Padre Njoroge kilivyotukia, na kuwaacha bumbuazi.

Maisha yake katika huduma ya watu wa Mungu

Hata hivyo kwa muda mfupi, raish wa chama cha Mapadre wa Jimbo Kuu la Nairobo Padre Stephane Mbugua, amethibitisha kuwa kifo cha padre huyo kimeokana na mauaji ya kupangwa na yaliyofanya na kikundi cha watu mbao ahwakuwa wanapendelea uendeshaji wake wa dhati katika parokia yake. Padre Mbugua amaesema kuwa Padre Njoroge alikuwa amesha onesha juu ya kuishi akikabiliana na matatizo mengo katika parokia ya Kinoo.  Wakati wa mkutano ya kima mwezi ya makleri wa Jimbo Kuu Katoliki Nairobi, Padre Njoroge alikuwa amesimulia matatizo ambayo alikuwa anakubiliana nayo na wahusiska wa parokia yake, amethibitisha Padre Mbugua.

Akiongeza amaesema siku moja alisema kuwa yuko tauari kugeuka kondoo aliyechinjwa, lakini hakuwa anaweza kufikiria kuwa muda ungemfikia haraka namna hiyo. Kaka yetu amekutana na kifo cha uchungu sana. Tusali kwa Bwana ili aweze kujaliwa maono matakatifu ya mbingi. Amekufa akihudumia kwa udhati watu wa Mungu.Taarifa kutoka habari za kimisionari, Fides, zinathibitisha kuwa hata hivyo pia kuna padre mwingine ambaye alikuwa ameeleze mashaka yake juu ya kifo cha padre Njoroge.

20 December 2018, 15:28