Tafuta

Tunapaswa kukumbuka utakatifu wa maisha tunao usherehekea katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana.Ni uzima ambao hauwezekani kufutwa na mikono ya binadamu kwa sababu yoyote Tunapaswa kukumbuka utakatifu wa maisha tunao usherehekea katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana.Ni uzima ambao hauwezekani kufutwa na mikono ya binadamu kwa sababu yoyote  

Kard.Bassetti:Ni utakatifu wa maisha,tunaouadhimisha Siku ya Noeli!

Sikukuu hii ya kikristo kwa dhati ni furaha ya utakatifu wa maisha, Maisha yaliyotolewa na kupokelewa. Maisha maskini na ya unyenyevu. Ni uzima ambao hauwezi kufutwa na mikono ya binadamu kwa sababu yoyote ile na hata kuupunguzia katika mambo mengine ya mali za kidunua

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kamwe haijawahi kutokea kama wakati huu ambapo mashambulizi mabaya yameleta kifo kwenye soko la Sikukuu huko Strasbourg, tunapaswa kukumbuka utakatifu wa maisha tunao usherehekea katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Sikukuu hii ya kikristo kwa dhati ni furaha ya utakatifu wa maisha, Maisha yaliyotolewa na kupokelewa. Maisha maskini na ya unyenyevu. Ni uzima ambao haiwezekani kufutwa na mikono ya binadamu kwa sababu yoyote na hata kuipunguiza katika mambo ya vitu vini vya kidunia.

Soko la krismasi mjini Strasbourg Ufaransa: Hayo yamethibitishwa na Kardinali Gualtiero Bassetti, Askofu Mkuu wa Perugia- Citta della Pieve na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) akigusia juu ya shambulizi la kigaidi lililotokea kwa njia ya mhalifu aliyeshambulia soko la krismasi mjini Strasbourg Ufaransa mapema wiki hii na kuwaua watu watatu, kabla ya kuuuwawa na polisi baada ya kusakwa kwa siku tatu. Hata hivyo namba za waathirika zimeongezeka kifo cha mtu mwengine, mwandishi wa habari wa Italia. Janga hilo limetendwa na mhalifu aliyekuwa wameshitakiwa mara kadhaa nchini Ufaransa.

Katika pembe ya Gazeti la Osservatore Romano, Kardinali Guaritiero anaelezea kuwa, matarajio ya Yesu mwokozi anakuja kutoa maana, leo hii katika dunia uliyojeruhiwa na wenda wazimu wa kutisha wa kigaidi, ambao wanashambulia kwa kushitukiza na kuua bila huruma jirani, kadhalika Yesu anakuja katuka maisha ambayo katika ukawaida wetu wengine wamejazwa na viwanda vya tamaa ya mali na kupenda kutumia hovyo. Matukio yote mawili ya jamii ya sasa, Kardinali anasema yana utofauti kati yao, lakini yanafafana kwa sababu ya kuwa na mzizi mmoja ule wa kupoteza maana ya kina ya maisha ya binadamu, nini maana kuu ya maisha ya binadamu.

 Kardinali Bassetti anasema: Kwa upande mwingine kwa dhati maisha yamapoteza kutokana na wengine kulipa visasi, nna kwa upande mwingine wanatengeneza viwanda vya faida. Kwa manatiki hiyo, Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kinyume chake ni utenzi wa maisha; ni zawadi ambayo unaweza kutambuliwa tu kwa utumilifu kwa njia ya unyenyekevu na imani.

Kardinali akitumia tafakari ya  hivi karibuni ya Baba Mtakatifu Francisko anasema , Yeye anawaalika kuishi kipindi hiki si kwa njia ya kuzungukia pango kwa katika mambo ya kidunia. Pango leo hii linatoa maana ya kuwa na  urahisi wa kiinjili, umaskini na unyenyekevu. Hakuna jingine. Pango leo hii kwa namna moja, linafungua masikio kwa yule aliye msafi wa roho. Ni lazima kukaribia Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa kuonja ule utamu na kuachilia upande mwingine, masuala ya madharau, masengenyo na migawanyiko. Na huo ndiyo upole wa maisha, ambao Yesu alizaliwa katika Holi la Bethlehem na kila mwaka anazaliwa katika mioyo yetu.

Fumbo la Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana kwa maana hiyo inatuuliza, namna gani ya kuwa binadamu kwa sababu binadamu huyo ndiye aliyekuja na kuwa kwetu kama wito. Katuka sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ubinadamu wa Mungu unachukua umbo la nyama na damu ambayo imekuwa sisi wenyewe kwa kujifanya mkate. Mtakatika Francisko wa Assisi alitambua fumbo la Ekaristi ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, na mabayo inajiwakilisha katika pango la Greccio nchini Italia, ikionesha holi la wanyama na ambayo iligeuka kuwa altare amhali ambamo wanafanya maadhimisho ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwama ndiyo moja ya maadhimisho ya kusihi kwa pamoja katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa bwana , kifo na ufufuko wake. Ndilo fumbo la imani na ambalo ni wokovu wetu.

Baba Mtakatifu pia katika tafakari ya maandalizi haya anasema: Kipindi cha Majilio kinatualika katika jitihada za kukesha na kutazama nje yetu binafsi ili kupanua akili na moyo, kujifungulia mahitaji ya watu, ndugu na matashi ya ulimwengu mpya. Ni matashi ya watu wengi wanaosumbuka kwa njaa, ukosefu wa haki na vita; ni ustashi wa maskini, wadhaifu na ambao wameachwa peke yao katika pembezoni mwa jamii. Hiki ni kipindi mwafaka cha kufungua mioyo yetu ili kuweza kujiuliza kwa dhati juu ya jinsi gani tunatumia muda wetu katika maisha.

Mhalifu wa huyo alikuwa tayari anafahamika na vyombo vya madola: Vyombo vya habari vinaripoti kuwa Cherif Chekatt mwenye umri wa miaka 29 amewahi kushitakiwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu ambayo ni pamoja na vurugu na wizi na aliwekwa pia katika orodha ya watu walio na misimamo mikali alipokuwa jela nchini Ufaransa, mwaka 2015 ambapo wakati huo alielezwa na serikali ya nchi hiyo kwamba alikuwa miongoni mwa watu walio na itikadi kali. Kuanzia wakati huo amekuwa akifuatiliwa na idara ya ujasusi ya Ufaransa inayowafuatilia pia maelfu ya washukiwa hao nchini humo. Alishahukumiwa mara 27 Ufaransa na hata nchini Ujerumani, Switzerland na Luxembourg, maeneo yanayofikiwa kwa urahisi kutoka Strasbourg.

Soko la Krismasi lafunguliwa tena baada ya shambulio: Huku hayo yakiarifiwa, soko la Krismasi mjini Strasbourg limefunguliwa tena ambapo siku kadhaa baada ya shambulizi kutokea siku ya Jumanne wiki hii. Tarehe 13 Desemba 2018 Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Christophe Castaner alisema soko hilo litafunguliwa muda mfupi baada ya saa tano mchana. Siku ya Jumanne tarehe 12 Desemba 2018 jioni, Cherif Chekatt aliwamiminia risasi watu waliokuwa katika soko hilo na kuwauwa watu watatu huku wengine 13 wakijeruhiwa. Waendesha mashtaka wa Ufaransa wanalichukulia shambulizi hilo kama shambulizi la kigaidi. Kundi la wanamgambo wa dola la kiislamu wamekiri kuhusika na shambulizi hilo.

15 December 2018, 11:03