Tafuta

Vatican News
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imetoa chakula kwa wazee, wahamiaji na wenye matatizo ili kurejesha matumaini ya wakati endelevu kwa ndugu wadhaifu Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imetoa chakula kwa wazee, wahamiaji na wenye matatizo ili kurejesha matumaini ya wakati endelevu kwa ndugu wadhaifu 

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio:Noeli ishara ya mshikamano na ndugu!

Tendo la kusheherekea na kula pamoja sikukuu ni kutoa ujumbe wa matumaini yanayoshinda kila kila aina ya kujifungia binafasi na kurejesha matumaini ya wakati endelevu wa ndugu wadhaifu. Ni kwa mujibu wa maneno ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio tarehe 25 Desemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Watu wa kujitolea, hasa sehemu kubwa ya vijana wameonekana katika vituo 100 vya miji ya Italia katika meza ya watu wasio kuwa na makazi, wazee, wahamiaji waliofika kwa njia ya mkondo wa kibinadamu katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. “Tendo la kusheherekea na kula pamoja sikukuu ni kutoa ujumbe wa matumaini yanayoshinda kila kila aina ya kujifungia binafasi na kurejesha matumaini ya wakati endelevu kwa ndugu hao wadhaifu. Hayo yametamkwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio  wakati wa chakula chakula cha watu wote wenye kuhitaji, ambapo kama jumuiya ya Mtakatifu Egidio wamekuwa wakiandaa karibu duniani kote, mahali popote palipo na wanachama wa jumuiya hiyo. Katika kituo cha chakula kwenye Kanisa Kuu la Bikira Maria Trastevere Roma, tarehe 25 Desemba 2018 Balozi wa Vatican nchini Italia amepeleka salam kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko.

Zaidi ya watu 240,000 katika nchi 77 duniani na kati yao, 60,000

Zaidi ya watu 240,000 katika nchi 77 duniani kote na kati yao, 60,000 ni watu wa nchi ya Italia, wameweza kushiriki  Meza ya Chakula cha Noeli na Maskini wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio tarehe 25 Desemba 2018. Kuanzia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Trastevere Roma, mahali ambapo walianzisha shughuli hii kiutamaduni kunako mwaka 1982 wakiwa na kikundi kidogo cha wazee  na ambapo siku kama hii nzuri zaidi kwa mwaka wangebaki peke yao. Kama  kama kawaida sasa ya jumuia imeweza kuwafanya watu wengi, tofauti kati yao kukaa meza moja. Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo anaendelea kueleza kuwa: “Hawa wote ni watu wasio kuwa na makazi, wakimbizi wengi waliofikia Ulaya kwa njia ya mkondo wa kibinadamu, watoto wa mitaani, watoto wenye matatizo katika miji mikuu ya Afrika na Amerika ya Kusini”.

Vituo vingi nchini Italia vya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuadhimisha miaka 50

Katika mwaka wa 50 wa tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, kwa mara nyingine tena, Jumuiya kwa upande wa Italia imeweza kuhusisha vituo vingi vidogo kama vile: Roma, Napoli, Genova, Messina, Milano, Bari, Firenze, Torino, Novara, Padova, Catania, Palermo, Trieste, Reggio Calabria na vingine vingi. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Bwana Marco Impagliazzo akielezea juu ya tukio kama hili, amesema kuwa ni watu wanaosaidia wanachanganyikana na wale waliosadiwa; ni familia kubwa ambapo kuna nafasi ya kila mmoja. Kuongezeka kwa idadi kubwa  ya watu mwaka huu, inaonesha  wazi kwa jinsi gani inawezekana kujibu utamaduni wa ubinafsi  na na ubaguzi  na ambapo  mara nyingi umetawala na unarudisha nyuma matumaini ya wakati endelevu na wa kuujenga kwa pamoja.

 

26 December 2018, 14:38