Tsunami imeikumba eneo la Sunda mashariki wa  nchi ya  Indonesia Tsunami imeikumba eneo la Sunda mashariki wa nchi ya Indonesia 

Indonesia:wito kutoka mtandao wa Caritas kwa ajili ya mshikamano

Siku chache zilizopita Tsunami iliikumba nchi ya Indonesia kwa mara nyingine tena na kuharibiwa visiwa vya Java na Sumatra. Idadi ya waathirika inazidi kuongezeka hadi kufikia vifo 429 na majeruhi 1400 kwa mujibu wa msemaji mkuu katika shirika la kuthibiti majanga na kwamba waliopotea wanasadikika kuwa watu 128

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika nchi iliyokumbwa na tsunami, siku chache zilizopita na kuharibiwa katika visiwa vya Java na Sumatra, idadi ya waathirika inazidi kuongezeka  hadi kufikia vifo 429 na majeruhi  1400 kwa mujibu wa msemaji mkuu katika shirika la kuthibiti majanga Bwana Sutopo Purwo Nugroho na kwamba waliopotea wanasadikika kuwa  watu 128.

Baba Mtakatifu Francisko Jumapili 23 Desemba 2018, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alionesha maskitiko yake na pia ukaribu wake kwa watu wote ambao wamerundikana na kujaribiwa na mateso ya nchi nzima ya Indonesia. Baba Mtakatifu amewaalika watu wote kusali kwa ajili ya waathirika wa tsunami, wakati huo huo akatoa wito kwa jumuiya nzima ya kimataifa ili watu hawa kaka na dada wasikose mshikamano na msaada kutoka katika jumuiya hii  nzima ya kimataifa. Habari za kila siku zinasikitisha sana, zinazofika kutoka nchini Indonesia mara baada ya Tsunami kutokea tarehe 22 Desemba na kuikumba sehemu inayozunguka Sunda kati ya kisiwa cha Java na Sumatra kutokana na kulipuka kwa volkano Anak Krakatau. Na habari zinaeleza kuwa vulkano hadi sasa bado inaendelea na miripuko yake na inasababisha hofu kubwa katika sehemu ambazo tayari zimekumbukwa na majanga mengi hivi.

Taarifa kutoka Caritas mahali ya Indonesia inatoa wito

Taarifa kutoka Caritas mahalia ya Indonesia inatoa wito kwa ajili ya mshikamano  kuweza kuwasaidia manusuru wa janga kubwa hilo. Tsunami iliyokumba shemu ya Anyer juu ya kisiwa cha Java, mahali ambapo jimbo katoliki la Bogor linatoa huduma yake na sehemu ya Lampung katika kisiwa cha Sumatra mahali ambapo jimbo jingine la Tanjung Karang hutoa huduma yake. Idadi ya waathirika na uharibifu mkubwa unazidi kuongezeka hadi sasa. Hata hivyo mtandao wa Caritas ya Indonesia, wanaendelea kufanya kazi bila kupumzika hasa katika maeneo ambayo hayakushambuliwa ili kuweza kuwasaidia maeneo ambayo hadi dakika hizi ni dharura kubwa na siyo rahisi kupata mawasiliano na Caritas mahalia. Caritas ya Tanjung Karanga huko Sumatra, inajikita tayari kugawa vyakula kwa manusura, anasema hayo Yohannes mhusika wa shughuli za Caritas nchini Indonesia.

Shughuli hiyo imewezekana tu kutokana na watu wa kujitolea wanaosambaza vifurushi 700 na 500 kati yake ni katika maeneo ya hospitali ya mji wa Lampung na 200 katika mpaka wa Kalianda. Tarehe 25 Desemba 2018, vifurushi vingine zaidi ya 1000 vimesambazwa. Na katika kisiwa cha Java, watu wa kujitolea wako katika makambi  kutoka katika jimbo la Jakarta na wanasafiri kwa magari kutoka mji mkuu.  Mhusika wa Caritas ya Indonesia  anasema  Ofisi ya Caritas inaandaa kikundi maalum zaidi cha kusaidia na ambacho kitaendelea kutuma watu wa kujitolea wa Caritas katika maeneo mengine.

Mkurugenzi wa Caritas nchini Indonesia

Naye Mkurugenzi wa Caritas nchini Indonesia, Padre Ignatius Swasono, amesema kuwa katika miezi hii, walikuwa tayari wamesha pata dharura nyingi nchini humo na wakati huu wa kipindi cha Noeli, wameshambuliwa kwa ghafla bila hata ya kujitayarisha mahali pa kukimbilia. Ili waweze kuwasaidia zaidi, Padre, anatoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema huko Italia na nchi nyingine kwa mara nyingine tena katika kupindi hiki kinachokatisha tamaa na hofu kubwa kwani sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana iweze kuleta matumaini kwa watu waliopatwa na janga hili. Padre Swasono anaongeza kusema, watu wengi wa kujitolea wanaendelea kufanya kazi na kuelekea katika eneo lililokumbwa na Tsunami. Hospitali Katoliki za Cilegon Serang iko wazi kwa ajili ya huduma ya jumuiya na kwa ajili ya watu wote wenye kuhitaji msaada.

Caritas nchini Italia inaendelea kusaidia dharura kwa kushirikiana na Caritas Indosia

Caritas nchini Italia inaendelea kusaidia dharura kwa kushirikiana na Caritas nchini Indonesia zaidi ya miaka 15 hivi ambapo hadi sasa wameweza kufanya kazi kubwa ya kusadia dharuda za majanga ya asili ambazo zinaikumba nchi hiyo kila mwaka kama vile (mafuruko, tetemeko la ardhi na moto) lakini hata hivyo na mipango mingine ya maendeleo ili kuongeza juhudi ya jumuiya mahalia.

Wasiwasi umeongezeka kuhusu uwezekano

Kuna hata uwezekano wa kulipuka magonjwa, waathiriwa wakilazimika kuishi katika kambi za muda. Kwa mujibu wa ripoti za madaktari, idadi kubwa ya watoto wanaugua homa na kuumwa kichwa, bila ya kunywa maji wala kula chakula cha kutosha. Tetemeko la ardhi lilofuatiwa na mawimbi makubwa yenye nguvu (Tsunami) iliifunika pwani ya Indonesia na kusababisha uharibifu mkubwa kusini mwa Sumatra na magharibi Java. Makaazi yaliyo karibu na pwani, pamoja na hoteli za watalii ziliharibiwa vibaya. Tukio la Jumamosi 22 Desemba, halikuwa limetabiriwa na wataalam kwa maana hiyo wanaonya kwamba matukio zaidi ya tsunami yanatarajiwa kutokea Indonesia. 

Kadhalika, Idara ya Jiolojia nchini humo imesema tsunami hiyo imesababishwa na mawimbi ya chini ya bahari yaliyolikumba Lango Bahari la Sunda, linalounganisha Bahari Hindi na Java, umbali wa kilomita 200 kusini magharibi mwa mji mkuu, Jakarta. Idara ya Kukabiliana na Majanga imesema watu wengi wameaga dunia huku mamia ya wengine wakijeruhiwa, mbali na makumi ya wengine wakitoweka kutokana na janga hilo la kimaumbile na kwamba maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Pandeglang katika mkoa wa Banten na mji wa Bandar Lampung, kusini mwa eneo la Sumatra. 

 

26 December 2018, 13:19