Wakimbizi wa Venezuela nchini Colombia Wakimbizi wa Venezuela nchini Colombia  

Colombia:Balozi wa Vatican atembelea Cúcuta na kutoa msaada!

Balozi wa Vatican nchini Colombia Askofu Mkuu Luis Mariano Montemayor ametoa msaada wa tani tatu za vyakula katika Jimbo la Cúcuta, wakati wa fursa ya ziara yake ya kitume, jimbo lenye kuwa na idadi kubwa ya makaribisho ya wahamiaji kutoka nchini Venezuela

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Balozi wa Vatican nchini Colombia Askofu Mkuu Luis Mariano Montemayor ametoa msaada wa tani tatu za vyakula katika Jimbo la Cúcuta, wakati wa fursa ya ziara yake ya kitume mwishoni mwa wiki iliyopita, jimbo lenye kuwa na idadi kubwa ya makaribisho ya wahamiaji kutoka nchini Venezuela. Balozi wa kitume ameweza kutembelea vituo mbalimbali vilivyoendeshwa na Jimbo la Cacuta na tarehe 22 Desemba 2018  alitembelea kituo cha nyumba ya Msaada wa Mungu na kukutana na Askofu Víctor Manuel Ochoa Cadavid, pamoja na Askofu Mario del Valle Moronta wa jimbo la Mtakatifu Cristobal nchini Venezuela linalopakana na nchi ya Colombia na kwa maana hivyo vituo hivyo vya wahamiaji, vinapatikana katika mpaka kati ya Venezuela na Colombia.

Hali halisi ya wakimbizi wa venezuela

Maaskofu wote wawili, wamempa taarifa Balozi wa Vatican kuhusu hali halisi ya uhamiaji wa sasa,na Balozi ameweza kuzungumza moja kwa moja na wahamiaji na kutoa huduma ya chakula, ikiwa kama ishara ya kuwa karibu nao. Askofu wa Cristobal ametoa shukrani kubwa kwa namba ya Kanisa la Cacuta, linavyojitahidi kusaidia ndugu wahamiaji kutoka nchini Vanezuela: Ni baraka ya Mungu kuwa na askofu, mapadre na wale wanatambua kusaidia ndugu kaka na dada wa Venezuela kwa namna ya ajabu.

Baba Mtakatifu Francisko anashukuru nchi ya Colombia

Na kwa upende wa Balozi wa Vatican Montemayor amewasihi majimbo yote wasichoke kupeleka msaada kwa ajili ya wahamiaji. Na kwa kusisitiza zaidi amesema: “Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru kwa moyo wote kwa sababu ya juhudi zenu zote mnazoonesh na kushukuru nchi ya Colombia kwa ajili ya kuwa na siasa ya milango wazi… sisi sote ni ndugu kaka na dada. Yeye kama mzaliwa wa Argentina, anapatwa uchungu katika roho yake kuwa na watu wa Amerika ya Kusini wanapatwa na jaribu hili kama hilo la Venezuela”.  Hata hivyo pia  Balozi alipata kutembelea daraja la Kimataifa la Sim Simón Bolívar, ambalo linapakanisha nchi ya Colombia na Venezuela. Vilevile amehitimisha na mikutano yake kwa Misa katika Kanisa kuu na kutembelea vituo mbalimbali vya jimbo na vya upendo kimisionari!

26 December 2018, 13:29