Cerca

Vatican News
Maaskofu nchini Chile katika ujumbe wao wa Noeli unaonesha wasiwasi mkubwa kuhusu wakimbizi, amani na uaminifu wa dhati wa Kanisa Maaskofu nchini Chile katika ujumbe wao wa Noeli unaonesha wasiwasi mkubwa kuhusu wakimbizi, amani na uaminifu wa dhati wa Kanisa  (Vatican Media)

Chile:Ujumbe wa Noeli wa maakofu ni hofu ya wakimbizi!

Maaskofu wa nchini ya Chile wanatoa ujumbe wao wa matashi mema ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, wakiwa na hofu kubwa juu ya wakimbizi na amani ya Araucanía

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maaskofu wa nchi ya Chile wanatoa ujumbe wao wa matashi mema ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, wakiwa na hofu kubwa juu ya wakimbizi na amani  ya Araucanía”. Tunamshukuru Mungu ambaye alichagua ubinadamu kama makao, ndivyo ujumbe wa maaskofu wa Chile unavyoanza kwa njia ya video uliotolewa na Askofu Silva Retamales Rais wa Baraza la Maaskofu wa Chile ambapo anasema kuwa: “ni  kwa njia ya Yesu Kristo Mungu anatupatia maisha tele na kutupatia maana na ukamilifu wa maisha yetu. Kwa kuangazwa na unyenyekevu wa mtoto Yesu pangoni Bethlehemu, sisi maaaskofu wa Chile tunaomb  katika nchi ya Chile, kuwepo na thamani ya amani, haki, upendo na ukweli wa Yesu ambaye anatangazwa na kuishi.

Mtoto Yesu anawaalika kuamka katika usingizi mzito

Katika ujumbe huo kwa njia ya video, Askofu Silva anataja baadhi ya mahangaiko ya nchi, akianzia na suala na ndugu wahamiaji kwa namna ya pekee, wale ambao hawapokelewi, hawatambuliwi na hawakuheshimiwi hadhi yao . Kadhalika wazo na ujumbe huo wa matumaini, unawaendea familia zilizokumbwa na janga la madawa ya kulevya, na hasa hasa kwa watoto na vijana. Na ndiyo wito wao mkuu unasisitiza juu ya kutokusahau, kwamba hayo ndiyo matumaini yaliyomo kwa mtoto Yesu ambaye daima anawaalika kuamka wote na kumwongokea.

Maskofu  wa Chile, wanawatazama kwa karibu, wagonjwa wote hasa wale ambao ni wenye magonjwa sugu. Na pia wazo lao linatazama Mkoa wa Araucani na kwamba, mwanga katika pango na ujumbe wa amani ambao ulitangazwa na malaika, unawaalika watu wote wenye mapenzi wema, waweze kuutimiza huko Aaraucania: “heshima ya maisha na hadhi ya kibinadamu, pamoja na ulazima wa kujikinga katika historia ya watu wa Mapuche, usaidie kwa hakika kutimiza hatua muhimu ambazo zimeanzishwa!

Maaskofu wa Chile wanathibitisha juu ya utambuzi wa hali halisi 

Na mwisho Maaskofu wa Chile wanathibitisha juu ya utambuzi wa hali halisi  na ngumu ambayo Kanisa nchini Chile inaishi, kutokana na kashfa za manyanyaso ya kingono;  kwa maana  hiyo wanatoa mwaliko kuwa,  watu ambao wanatazama Kanisa kwa mbali, basi wajaribu kuligeukia kwa mara nyongine tena kwa  matumaini ya wakati endelevu yenye uhakika na kwa juhudi kubwa zaidi na uongofu.

24 December 2018, 15:50