Tafuta

Vatican News
Ni kipaumbele cha kutangaza Injili ya Bwana kwa maskini kwa njia ya matendo ya upendo wa dhati Ni kipaumbele cha kutangaza Injili ya Bwana kwa maskini kwa njia ya matendo ya upendo wa dhati 

Bangladesh:Kutangaza Injili kwa maskini ni kipaumbele!

Kardinali D’Rozario, Askofu Mkuu wa Dacca wakati akizungumza katika Mkutano Shirikisho la watawa wa Bangladesh (BCR)tarehe tarehe 21 Desemba wakati wakiadhimisha mwaka wa 40 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kutanganza Injili kwa maskini ndiyo kipaumbele  cha Kanisa kwa upande wa watawa wote na waamini wakristo wote nchini Bangladesh. Amesema hayo Kardinali Patrick D’Rozario, Askofu Mkuu wa Dacca wakati akizungumza katika Mkutano Shirikisho la watawa wa Bangladesh (BCR) ambao tarehe 21 Desemba waliwa wanadhimisha mwaka wa 40 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo.

Kardinali D’Rozario anasema kutangaza Neno habari njema ya Yesu, ni utume wenye thamani ambao kila mmoja, mapadre na watawa wote wanashirikishana katika uwajibu  wao wa kuinjilisha kwa maskini na watu wote wa Bangladesh. Mkutano huo uliwaunganisha wajumbe zaidi ya 500 ambao ni wamisionari katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuhamasisha amani kati ya watu, hadhi na haki za binadamu.

Lengo la Mkutano wa Shirikisho la watawa

Lengo la Mkutano wa Shirikisho la watawa ni kutaka kuongeza mawasiliano zaidi kati yao;kubadilishana mawazo kati ya mashirika ya kitawa na kutafakari kwa pamoja masuala mbalimbali ya mashirika na matatizo yanayo waunganisha kwa pamoja katika nchi ya Bangladesh. Hiyo ni nchi ambayo sehemu kubwa ya wakazi ni waislam na wakati wakristo wanaunda sehemu ndogo tu ya watu wote. Mkutano huo umendaa shughuli za makundi mbalimbali ya wanachama kwa ngazi ya kitaifa na kijimbo kwa kutoa fursa ya watawa wa Bangladesh ili kujipyaisha na kuendelea kwa wote kwa ngazi ya mafunzo  kila maisha yao ya kitawa.

Maelfu ya mapadre, watawa wamejikita katika shughuli za kuendeleza na kusindikiza imani ya wabatizwa wa Bangladesh, kwa namna ya pekee jumuiya za vijijini, ambao kwa kiasi kikubwa wako chini kimaendelea na kiuchumi katika vijijini. Hayo yamethibitishwa na Padre James C. Cruze CSC,Mwenyekiti wa Shrikisho la Watawa nchini Bangladesh (BCR).

Maeneo msingi yanayoongoza kama ufunguo wa shughuli za Kanisa

Maeneo msingi yanayoongoza kama ufunguo wa shughuli za Kanisa nchini Bangladesh ni manne: kwanza uinjilishaji, elimu, afya na maendeleo ya kijamii. “Kama wamisionari wa Bangladesh tunajibidisha kumtangaza Kristo, kwa ujumbe wa Injili ya uhuru, matumaini, upendo na huduma kati ya watu wote tunaokutana nao”. Hayo yamethibitishwa na Sr. Rita Godino CSCk Katibu wa Shirikisho la Watawa Bangladesh. Kanisa Katoliki nchini Bangladesh linahesabu karibia waamini 350,000 walioko katika majimbo katoliki nane yaliyomo nchini humo. Wapo karibia wakristo wa madhehebu mengine 500,0000 nchini Bangladesh yenye kuwa na idada ya watu karibia milioni 160, sehemu kubwa ya watu ikiwa ni waislam.

27 December 2018, 13:33