Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick, Jimbo Kuu Katoliki la  Melbourne huko Australia Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick, Jimbo Kuu Katoliki la Melbourne huko Australia  

Askofu wa Melbourne:Uinjilishaji mpya kwa waamini wa Australia unahitajika!

Moja ya changamoto ya Kanisa la Australia ni utume wa Uinjilishaji kwa waamini wanaokiri ni wakristo, lakini hawashiriki ibada na shughuli hai za Kanisa. Hayo yametamkwa na Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Melbourne, Australia,Askofu Mark Edwards

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Moja ya changamoto ambayo tunaitwa kukabiliana nayo nchini Australia ni utume ambao ni dharura ya kupeleka mbele na ndiyo ya kuweza kufikita watu ambao wanasema ni wakatoliki lakini baadaye hawaendi Kanisani. Hayo yamethibitishwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Melbourne, askofu Mark Edwards ambaye aanathibitisha katika Shirika la Habari za Kimisionari kuwa kwa mujibu wa Takwimu za kitaifa, asilimia 22 % wanajidhihirisha ni wakatoliki. Lakini kesi ya asilimia tisa ya kumi hawajuhi ni kwa jinsi gani ya kuweza kuwafikia,kati yao walio wengi ni vijana. Askofu anasema. “sisi ni taifa la wahamiaji  katika Kanisa letu kuna watu wengi wa mataifa mbalimbali. Lakini swali la kijiuliza kila siku je ni jinsi gani ya kuwafikia wazaliwa wa Australia?

Asilimia ya watoto wanaokwenda parokiani ni watoto wa wahamiaji

Hata watoto na vijana ambao wanakuja kawaida katika Maparokia kwa mujibu wa Askofu Edwards asilimia kubwa ni watoto wa wahamiaji. Daima hawa ni watoto wa wahamiaji wenye asili ya Ufilippini, Indonesia au Vietnam. Katika nchini Australia upo urithi muhimu wa mtandao wa shule katoliki ziliosambaa. Katika Taasisi zao wanaelimisha karibia asilimia 20% ya vijana wenye asili ya nchi ya Austaralia  na ambao wana fursa ya  kutambua vema imani ya kikristo, papa na Kanisa kwa njia ya Shule; lakini Askofu anathibitisha kwamba,  kuwageuza wawe wajumbe hai katika jumuiya katoliki,  hiyo ni historia nyingine.

Wahamiaji wanajitambua madhehebu yao na kuudhuria ibada

Huko Australia, watu wa mataifa na makabila mengine yanajitambua kwa ujumla wali wengi ni wakristo; na watu wanaosema ni wakristo ni asilimia 58% karibia  na asilimia 30% ambao hawamjui Mungu wakati  wengine ni waislam, wayahudi, wahindu, wasikh au wabudha. Hawa kwa kwawaida ni madhehebu madogo na ambayo kwa upande wao wanahishi kwa mazungumzo ya kidini amethibibitisha.

Kristo analeta maana ya maisha ya dhati

Changamoto na utume wa dharura kwa sasa ni ule wa kuweza kuwasiliana na kuwashirikisha katika matendo hai ya kuchungaji watu ambao wanakiri ni wakristo kwa majina, lakini katika maisha ya kila siku hawaonekani, na  kwa kufanya  hivyo wanaweza kwa dhati kujipyausha na kukutana na Kristo ambayo katika imani ya dhati analeta maana ya maisha, Amehitimisha Askofu. Katika nchi ya Australi yapo majimbo katoliki, 33 katika willaya 5 kama vile Sydney, Melbourne, Adelaide, Perth na Brisbaine.

18 December 2018, 14:18