Tafuta

Vatican News
Watawa wajitayarishe katika ufahamu wa masomo maalum hasa ya kitaalimungu, liturujia na Biblia wakiwa pamoja na waseminari Watawa wajitayarishe katika ufahamu wa masomo maalum hasa ya kitaalimungu, liturujia na Biblia wakiwa pamoja na waseminari  (Vatican Media)

Zambia:ushiriki wa watawa katika mafunzo ya kikuhani seminarini!

Kushiriki katika sehemu ya mafunzo ya kikuhani katika seminari. Anathibitisha kwamba hatua hiyo hasa ya kuendelea kujitayarisha katika ufahamu wa masomo maalum hasa ya kitaalimungu, liturujia na Biblia si tu kwa ukuaji wa kiroho na kidini, lakini pia hata kushiriki katika malezi na mafunzo ya kikuhani wakina na makuhani

Sr. Angela - Rwezaula

Askofu, Patrick Chisanga wa Zambia, amewahimiza watawa  nchini Zambia kushiriki katika sehemu ya mafunzo ya kikuhani seminarini. Anathibitisha kwamba katika hatua hiyo hasa ya kuendelea kujitayarisha katika ufahamu zaidi wa masomo maalum hasa ya kitaalimungu, kiliturujia na Biblia si tu kwa ukuaji wa kiroho na kidini, lakini pia hata kushiriki katika malezi na mafunzo ya kikuhani pamoja na makuhani, kwa maana hiyo amezidi kuhimiza kwamba uwepo wa watawa katika mafunzo ya makuhani katika seminari ni muhimu.

Chama cha watawa Katoliki Zambia kilianzishwa kunako 1958

Askofu Chisanga amezungumza hayo tarehe 17 Novemba 2018 wakati wa maadhimisho Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzisha kwa Shirikisho la watawa (ZAS) sherehe iliyofanyika katika Parokia ya Roma Jimbo Kuu Katoliki Lusaka. ZAS ni mwavuli unaounganisha pamoja wakuu wa Mashirika ya kitawa nchini Zambia. Shirikisho la Chama hicho  kilianzishwa kunako mwaka 1958 na kina wajumbe wanachama wa mashirika 45 mahalia na wa kimataifa, ambao wanafanya idadi zaidi ya jumla ya watawa 1,500 nchini Zambia.

Askofu ameomba Chama cha watawa katoliki Zambia (ZAS) kufanya kazi na  Baraza la Maaskofu Zambia (ZCCB) ili kuhakikisha kuwa watawa wanapata maandalizi mazuri ya kitawa na ili waweze kujikita katika utume wao kwa kusaidiana na maaskofu kuwaandaa mapadre endelevu. Askofu huyo ambaye pia ni Msamamizi wa utume mashirika ya kitawa na vyama vya Kitume wa Baraza la Maaskofu Zambia, amewataka watawa waendelee kuimarisha kwa kina na ushirikiano hasa katika kuwafunda vema katika mafunzo ya watawa wao vijana. Kwa kusisitiza zidi amesema, kuendelea na mafunzo haina maanaya mafunzo ya kitaaluma tu katika sayansi ya kidunia, lakini pia ni kuongeza uelewa wa kina wa mwito binafisi kwa ajili ya utakatifu. Kadhalika Askofu pia amehimiza Serikali ya Zambia kutoa msaada muhimu kwa kile ambacho kinatendeka na chama hicho katika sehemu zote nchini, hasa katika utoaji wa huduma za afya na elimu katika maeneo yaliyo pembezoni mwa nchi.

Askofu akifafanua zaidi amesema, “katika kutekeleza shughuli hizo, Kanisa halishindani na mtu yeyote; Kanisa halina tamaa ya kitu chochote zaidi ya kutaka kufanya mapenzi ya Mungu na kuendeleza utume wa Kristo. Kutokana na hilo ameongeza, “Tunatoa wito kwa Wizara zote za Serikali husika kusaidia hasa kwa utoaji wa motisha muhimu ili watawa wetu waweze kuendelea kufanya utume wao kwa ufanisi”, amesema.

 Mwaliko wa kusoma ishara za nyakati kwa ajili ya vijana

Kadhalika Askofu wa Jimbo la Mansa, amewashauri wanachama hao, kusoma ishara za nyakati na kungalia mahitaji ya vijana kwani amesema, “mwaka huu Kanisa limejikita kuweka Sinodi nzima iliyokuwa inawahusu vijana. Na kwa maana hiyo kulikuwa na haja kubwa kwa Chama cha Watawa Katoliki Zambia kufuatilia kile kilichojadiliwa katika Sinodi hiyo na ili kuweza  kutafsiri matokeo ya Sinodi hiyo  kwa kutumia uzoefu huo wa hali halisi katika maeneo ambayo wao wanatumikia. Ametaja pia eneo jingine muhimu ambalo kama mashirika wanapaswa kujijita na eneo hilo  ni kuhusu huduma ya uchungaji katika familia.

Katika kusisitiza amesema: “Kuna vitisho vingi vinavyotishia uaminifu wa familia” na hiyo ina maana  kwamba mkristo ni pamoja na maadili ya jadi ya familia, kwa njia hiyo Askofu amethibitisha: “Tunahimiza ninyi kama  chama cha watawa katoliki Zambia (ZAS), ambao ni pamoja na taasisi watawa kike na kiume kufanya kazi pamoja katika utume wa kurejesha na kuhifadhi maadili ya familia za kikristo na jadi zake za Zambia” pia ameongeza kusema, “hebu tuwe na umoja na tusaidie maono  na juhudi za  chama cha Watawa Zambia (ZAS) katika kukuza ubora wa maisha”.

29 November 2018, 15:30