Tafuta

Vatican News
watu wanasali kwa ajili ya kupinga vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza watu wanasali kwa ajili ya kupinga vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza  (ANSA)

Makombora katika ukanda wa Gaza:mateso ya Waisraeli ni sawa na ya Wapalestina!

Mateso ya waisraeli ni sawa sawa na mateso ya Wapalestina kwa sababu, kuna wamama wa kipalestina na kiisraeli wanaolia kwa ajili ya watoto wao. Mateso na matatizo yanawaunganisha wote sehemu mbili na Kanisa halitazami bendera, bali linajitoa kusali kwa ajili sehemu zote bili

 Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumuiya ndogo katoliki ziko chini ya mashambulizi ya Beersheva na ya Gaza wakiwa wameunganika katika sala ya amani. Ni katika masaa haya ya mivutano, makombora na mabomu  ambayo yameanza kwa upya kusikika sauti katika maeneo yote ya ukanda  wa Gaza. Kadhalika wapo ambao wanaishi katika maeneo hayo wanaungana kwa pamoja kusali na kuomba amani. Katika Mji wa Kiisraeli wa Beersheva ambao ulikuwa tayari umekwisha shambuliwa kunako tarehe 17 Oktoba na karibia waamini katoliki 120 wa Parokia ya Mtakatifu Ibrahimu,kati yao, kuna waisreli na waarabu wanasali kwa pamoja kwa ajili ya amani. Hayo yamesemwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Piotr Zelazko katika Shirika la Habari la Sir.

Wanasali kupitia makundi ya whatsApp kwa ajili ya amani

Padre Piotr Zelazko akiendelea na maelezo yake amethibitisha kuwa, kwa njia ya vikundi vya WhatsApp kila siku wanabadilishana mialiko kwa hekima na mafundisho muhimu, lakini zaidi ni yale  yanayohusu kusali kwa ajili ya amani na kwa ajili ya wadhaifu. Hiyo ni kwa sababu katika migogoro wadhaifu zaidi wapo katika  watu wa makundi mawili. Hili siyo suala la kuweza kupata suluhisho kwa njia ya silaha, hasa nguvu za silaha za waisreli anathibitisha . Kwa maana katika migogoro hiyo watu wa sehemu zote mbili wanateseka. Kuna wamama wa kipalestina na wa Israeli wanaolia kwa ajili ya watoto wao. Mateso na matatizo yanawaunganisha wote sehemu zote mbili. Kanisa halitazami bendera, bali linajitoa kusali kwa ajili ya watu wote hao, kwa maana hiyo anasisistiza: “ tusali hasa kwa ajili ya wale ambao hatima yao iko mikononi mwa vita hivi na ili kuweza kusitisha umwagaji wa damu”.

Wanamapambano wa Palestina wajibu mapigo, vituo vyamiminiwa makombora

Duru za habari zinasema kuwa, hadi sasa zaidi ya makombora na maroketi 400 yamevurumishwa katika vitongoji vya wakimbizi wa Kipalestina. Mashambulizi hayo ya harakati za mapambano ya ukombozi za Palestina ni jibu kwa jinai na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Israeli katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita. Miji na maeneo mengi ya Israeli yalijawa na sauti za ving'ora vya tahadhari, na Wasayuni walionekana wakikimbia huku na kule kutafuta pa kujikinga na makombora na wanaharakati wa Palestina. Awali makundi ya mapambano ya Palestina yalikuwa yametangaza kuwa, yatajibu mashambulizi ya aina yoyote ya Israeli kwa mujibu wa kanuni ya kulipiza kisasi na wajibu wa kujihami. Hali ya sasa ya Palestina inaonesha kuwa, harakati za mapambano za Palestina zimevuka kipindi cha kusubiri kushambuliwa na kujibu mapigo tu na sasa harakati hizo zinalenga maeneo muhimu ya Wasayuni na kuzusha mlingano wa hufa.

Jibu la mamia ya makombora na maroketi ya Wapalestina dhidi ya uchokozi

Jibu la mamia ya makombora na maroketi ya Wapalestina dhidi ya uchokozi wa Israeli ni sawa na kuongeza harakati za mapambano ya Ukanda wa Gaza mbele ya utawala wa Tel Aviv. Harakati hizo sasa zinatumia mikatakati ya mashambulizi dhidi ya mashambulizi. Utawala wa Kisayuni wa Israeli ambao umeshindwa kufikia malengo yake katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na huko Siria, sasa unafanya njama za kutaka kuficha na kufunika kushindwa huko na kuendelea  kuua raia wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. Jinai hizo zimejibiwa na wanamapambano wa Palestina kwa kuvurumisha mamia ya makombora na maroketi dhidi ya vituo vya sakari wa Kisayuni na vitongoji vya wahamiaji wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

 

 

14 November 2018, 11:13