Cerca

Vatican News
Bi Ana Maria Jorge, mlei ametuliwa kuwa Makamu wa Chuo Kikuu Katoliki katika Kitivo cha Taalimungu nchini Ureno Bi Ana Maria Jorge, mlei ametuliwa kuwa Makamu wa Chuo Kikuu Katoliki katika Kitivo cha Taalimungu nchini Ureno 

Ureno:Mwanamke ateuliwa kuwa makamu wa kitivo cha taalimungu!

Katika Chuo Kikuu Katoliki nchini Ureno, mwanamke amechaguliwa kuwa makamu wa kitivo cha Taalimungu. Huyo ni Bi Ana Maria Jorge, mlei na mwenye umri wa miaka 56. Ni profesa wa chuo kikuu hicho katika somo la historia ya Kanisa, Ukristo, Mbinu za Kufundisha na Mitaala

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kwa mara ya kwanza mwanamke anakuwa kiongozi Makamu Mkuu wa kitivo cha Taalimungu katika Chuo Kikuu Katoliki nchini Ureno. Kwa barua ya utambulisho huo kutoka Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki iliyoandikwa tarehe 26 Oktoba 2018, inathibitishwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mkuu wa kitivo cha Taalimungu cha Chuo hicho, Bi Ana Maria Jorge, mlei na mwenye umri wa miaka 56, ambaye alikuwa tayari ni profesa na msaidizi wa ndani katika kitivo  hicho, mara baada ya Padre Jose Tolento de Mandonca  kuchaguliwa kwenda katika Maktaba na hifadhi za nyaraka za Vatican.

Kitengo cha taalimungu kilianzishwa tangu tarehe 4 Novemba 2018

Bi Jorge ni daktari wa Sayansi za kihistoria katika kitengo cha nyaraka na falsafa, na alijinyakulia shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Lovanio, ni mjumbe wa Kamati ya Masomo ya kihistoria ya jamii nchini Ureno na katika masomo ya miaka ya kati na jamii ya kisayanis katika Chuo Kikuu Katoliki, wakati huo huo anafundisha historia ya Kanisa, Ukristo, Mbinu za Kufundisha na Mikabala.  Licha ya shughuli hizo pia ndiye mwaandaaji wa uzamivu katika mafundisho ya dini kwa watawa katika Taasisi za Kanisa. Shughuli hiyo aliianza mara baada ya kuongoza kituo cha mafunzo ya historia ya dini na gazeti la Lusitania sacra kunako 2007 hadi 2010.

Tangu tarehe 4 Novemba 1968, kuzinduliwa  Kitivo cha taalimungu ambapo kwa hakika ni miaka hamsini iliyopita, pakiwa tayari pameshakuwa na  mzunguko mwingi kwa ujumla wa somo hili. Pamoja na kitivo hicho cha Taalimungu kuwapo, Lisbon pia tangu mwaka 1987 kilizinduliwa kituo kingine cha kitivo hicho huko Braga na Porto nchini Ureno.

Mikakati ya Chuo Kikuu Katoliki nchini Ureno

Mikakati ya Taasisi hiyo kwa ajili ya kipindi tangu 2015-2020 kinatazama kuboresha na kuongeza nguvu zaidi katika muhimili wa maprofesa, kukarabati utafiti wa taalimungu na sayansi ya dini, uundaji wa taasisi ya sayansi ya dini, kushirikishana na taasisi mbalimbali za Kanisa ikiwa ni kitaifa na kimataifa, kushirikiana na Makanisa ya nchi za Afrika wanaozungumza lugha ya kireno.

Katika fursa ya sherehe za maadhimisho ya hivi karibuni ya Chuo hicho, Bi Ana Maria Jorge alithibitisha katika shirika la Kanisa la habari kuwa: muungano kimataifa katika mafunzo, kwa njia ya mzunguko wa maprofesa na walimu, inachukua nafasi mpya na iliyo ya juu. Ni suala lililopo lakini lenye changamoto kubwa. Pia alisisitiza kuwa, ni lazima kuhakikisha  huo muungano wa kimataifa katika Ulaya na kupanua kwa ngazi ya kidunia, ili kuifanya iwe bora kwa wanafunzi, hata kama kikundi chenye maana kubwa cha wanafunzi wa kitengo cha Taalimungu, kinaunganishwa na waseminari ambapo matokeo yake inakuwa vigumu kupendekeza kwao ili waweze kushiriki kozi katika shule nyingine katika nchi nyingine.

Mafanikio ya miaka hamsini ya kitengo cha Taalimungu

Makamu mpya wa kitivo cha Taalimungu akizungumza juu ya historia ya kitengo na shughuli yake katika vituo vingine vitatu vya kitivo cha taalimungu vilivyopo (Lisbon, Porto na Braga, ametoa mtazamo wa jumla kufuatia na miaka hamsini iliyopita tangu kuanzishwa kitengo cha Taalimgungu na kwamba, miaka hii imeweza kutoa uboara wa kizazi cha wanafunzi na leo hii mbele yake upo wakati endelevu, ambapo ni matarajio mema na ya kudumu muda mrefu. Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno ni Patriaki wa Lisbon, Kardinali Manuel Clement na Gombera wa chuo hicho ni mwanamke mwingine anaiyeitwa Isabel Maria de Oliveira Capeloa Gil.

28 November 2018, 15:43