Tafuta

Vatican News
Wakimbizi wa Rohingya wanateseka sana , kwa maana hiyo jumuiya Katoliki nchini Singapore imeanza kujikita katika kusaidia watu hawa kwa njia ya wamisionari wa Kijesuit Wakimbizi wa Rohingya wanateseka sana , kwa maana hiyo jumuiya Katoliki nchini Singapore imeanza kujikita katika kusaidia watu hawa kwa njia ya wamisionari wa Kijesuit  (ANSA)

Singapore:jumuiya ya wakatoliki kusaidia wakimbizi wa Rohingya!

Ni zaidi ya wakimbizi 700.000 wa kabila la Warohingya kutoka Myanmar ambao wako karibu na nchi ya Bangladesh kwa sababu ya kusongwa na wanajeshi. Kutokana na hilo Jumuiya Katoliki nchini Singapore inajikita katika harakati za kuweza kuwasaidia watu hawa wenye kuhitaji

Sr. Angela Rwezaula

Kusaidia waisilam wakimbizi wa Rohingya ili waweze kuwa  na elimu na mafunzo ya utaalam, ndiyo roho ya huduma ya wamisionari Wajesut kwa ajili ya wakimbizi nchini Singapore. Na hiyo inawezekana kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya watu wa kujitolea wa jumuiya katoliki mahalia ambao wametoa mchango kiuchumi, hata kwa upande wa Kanisa zima mahalia.

Zaidi wa wakimbizi 700,000 wa kabila la Warohingya kutoka Myanmar

Habari kutoka katika shirika la habari za kimisionari Fides linasema linaandika kuwa wanajiahidi kwa kila mali ili kusaidia kipeo cha zaidi ya wakimbizi 700.000 wa kabila la Warohingya kutoka Myanmar ambao wako karibu na nchi ya Bangladesh kwa sababu ya kusongwa na wanajeshi. Shughuli na mipango  ilianzishwa ya kukusanya fedha, hata kwa ajili ya kuandaa safari za kimisionari  na kuhamasisha utamaduni zaidi watambue hali halisi ya watu wakimbizi ambao wanazidi kuteseka wapate msaada.

Nchini Singapore kuna maparokia kama vile Mtakatifu Ignatius, la Huruma ya Mungu, Mtakatifu Antoni, na  Kanisa Kuu la Mchungaji mwema aambayo yameweza kujikita kuandaa maonesho ya picha  mbalimbali, sala, na mikutano ya kuwafundisha watu waelewe hali halisi ya wakimbizi hao.

Ushuhuda:kukaribia kambi ya wakimbizi ni kuonesha imani ya dhati

Mmoja wa watu wa kujitolea mkatoliki anathibitisha kuwa, tendo la kwenda kwenye kambi za wakimbuzi, inatoa fursa ya kuwakaribia kaka na dada na wote wenye kuhitaji. Ziara hiyo inaruhusu kwa dhati kuishi uzoefu wa imani ya  kikristo kwa dhati kama wakatoliki.

Kipaumbele cha wamisionari wa Kijesuit ni kufanya kazi hata na wadau wa nchi ya Indonesia, Thailand na ili kuboresha hali halisi ya mafunzo na kutoa msaaada wa kiakili  hata sheria kwa ajili ya wakimbizi wanaoomba hifadhi.

Hata hivyo kwa upande mwingine ni shughuli muhimu  ya kuhamasisha zaidi ili waamini wa Singapore watambue matatizo ambayo wanaishi wakimbizi na kuwafanya atambue kwa dhati dharura hii zaidi na kuwasaidia. Na kati ya shughuli nyingine zilizoanzishwa ni mipang ya mafunzo kwa ajili ya watoto, kusaidia vituo vya afya na shughuli nyingine za kijamii.

 

28 November 2018, 15:00