Tafuta

Vatican News
Asia Bibi kutoka Pakistani ameachiwa huru! Asia Bibi kutoka Pakistani ameachiwa huru! 

Pakistan: Asia Bibi amefutiwa adhabu ya kifo!

Tarehe 31 Oktoba 2018 majaria ya saa 9:20, asubuhi,na Italia ikiwa ni saa 5,20, Mahakama Kuu imeamuru kuachiwa huru kwa mwanamke mkristo Asia Bibi kufutia kesi yake ambayo imeigawa nchi. Asia Bibi alikamatwa na Polisi kunako 2009 kwa hatia ya kusingiziwa kukashifu wakati wakigombana na majirani zake

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mahakama ya Juu zaidi ya Pakistan imebatilisha hukumu ya kifo kwa mwanamke mmoja wa kikristo aliyekutwa na hatia ya kuikashifu dini ya kiislamu. Ni tarehe 31 Oktoba 2018 saa 9,20 majira ya asubuhi, Italia ikiwa ni saa 5,20 ambapo Mahakama hiyo imeamuru kuachiwa huru kwa mwanamke huyo katika kesi ambayo imeigawa nchi. Asia Bibi alikamatwa na Polisi kuna 2009 na alifungwa mwaka 2010 baada ya kukutwa na hatia ya mashtaka ya kuwa amekashifu mtume Mhamad, wakati wa kulumbana na majirani zake. Mwanamke huyo amekuwa akisisitiza kuwa hana hatia lakini ametumikia kifungo cha miaka nane kwenye chumba cha peke yake jela.

“Bwana amesikiliza sauti sala zetu kwa ajili ya Asia na wote ambao walikuwa karibu naye. Leo ni siku ya furaha kubwa ya kukumbuka katika maisha yote. Haki imeshinda na asiye na hatia hatimaye yuko huru”. Hayo yamesema katika vyombo vya habari vya Vatican Insider na Joespg Nadeem, mtu ambaye kwa miaka hii mingi amekuwa akihamasisha haki, shukrani kwa Chama cha Elimu ya kuzaliwa kwa Upya anacho kiongoza yeye huko Lahore na kinaelimisha na kuitunza Familia ya Asia BiBi, ambaye alikamatwa kunako 2009 na polisi katika kijiji chake cha Ittanwali, katika Wilaya ya Punjab.

Familia ya Asia Bibi ilipokelewa na Papa Francisko: Ikumbukwe mwezi Februari mwaka huu, Familia ya Asia Bibi, ikiwa ni Mtoto wake wa kike Eisham na mme wake Ashiq walifika Roma wakiwa wageni wa Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji (Acs) pamoja na Rebeca msichana mkristo wa Nigeria mwathirika wa Boko haram walikutana na Papa Francisko. Katika Mkutano wa faragha na Papa, Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji lilisema  kuwa ulikuwa  mkutano wao ulikuwa wenye mguso wa ajabu kutokana na historia yao  na kwamba, Papa alisema kuwa: Ushuhuda wa Rebeca na ule wa Asia Bibi, unawakilisha mtindo wa jamii ya sasa ambayo daima inazidi kuogopa uchungu. Hawa ni mashahidi alithibitisha hayo mara  baada ya kusikiliza historia yao ya kutisha. Hata hivyo mtoto wa Asia Bibi alimwambia Papa juu ya kukutana na mama yake kabla ya kuanza safari na jinsi gani Asia Bibi, alituma ampatie sala zake na kuomba sala zake,  pia mme wake,aliomba Papa sala kwa ajili ya mke wake na kwa ajili ya wakristo wote wanaoteseka

Mapigano ya waandamanaji hao na polisi yaliripotiwaTukirudi katika suala la Asia Bibi na hasa hukumu hiyo ya kihistoria tayari imesababisha maandamano yenye ghasia kutoka kwa makundi ya kisiasa yanayounga mkono sheria ya kukashifu dini. Maandamano dhidi ya maamuzi ya mahakama yalifanyika katika miji ya Karachi, Lahore, Peshawar na Multan.

Nje ya mahakama hiyo katika mji mkuu wa Islamabad kulikuwa na  kizuizi cha polisi na wanajeshi ambao walijipanga kuwazuia waandamanaji hao kuingia ndani. Jaji Mkuu Saqib Nisar, ambaye alisoma hukumu hiyo alisema “Asia Bibi anaweza kuachiwa huru kutoka gereza la Sheikupura, lililokuwa karibu na Lahore, ikiwa hatahusishwa na kesi nyingine yeyote”. Mwanamke huyo hakuwepo mahakamani kusikiliza hukumu yake lakini hakuamini maamuzi hayo yaliyotolewa dhidi yake alipoelezwa akiwa gerezani. "Siamini ninachokisikia kuwa nitaweza kutoka sasa. Kweli kabisa wataniachia huru?" Ni Shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema hayo kupitia njia ya simu.

Historia ya kisa cha Asia Bibi kushutumiwa: Kesi ya Asia Bibi ambaye jina lake halisi ni Asia Noreen ilianzia kwenye malumbano na kikundi cha wanawake mwezi Juni 2009. Wanawake hao walikuwa wanavuna matunda na ugomvi ulizuka kuhusu ndoo ya maji. Wanawake wa Kiisilamu walisema kuwa alikuwa ametumia kikombe ambacho wasingeweza kukishika tena kwa sababu imani yake imekifanya kikombe hicho kutokuwa safi. Mwendesha mashtaka alidai kuwa malumbano hayo yalikuwa yanamtaka Asia Bibi kubadili dini yake na kuwa muislamu ndio sababu iliyompelekea kutoa kauli za matusi dhidi ya mtume Muhammad katika majibu yake. Baadaye alipigwa mpaka nyumbani kwake wakati waliomshtaki wakidai kuwa alikiri kukashifu dini. Alifungwa baada ya polisi kufanya uchunguzi.

Kukashifu dini kuna maana gani Pakistan: Sheria ambazo ziliwekwa na Waingereza mwaka 1860 waliifanya kuwa ni kosa la jinai kwa mtu kusumbua mikutano ya dini, kupita makaburini, kukashifu imani ya mtu kwa maksudi mtu kuharibu chombo kinachotumika kuabudia na hukumu yake kwa hayo yote ni kifungo cha miaka 10. Majaji walisema kuwa mashtaka yaliyotolewa hayajajitosheleza kuthibitisha suala hilo. Kesi hiyo ilikuwa ina ushahidi mdogo, walisema kuwa hakukufuatwa utaratibu katika kufuatilia kesi hiyo. Inasemekana tu kuwa mshtakiwa alikiri mbele ya kundi la watu wengi waliotaka kumuua. Hukumu hii ambayo imeangalia Koran na historia ya dini ya kiislamu ilimalizika na nukuu kutoka kwa hadithi ,inayosema kuwa mtume Muhammad alitaka usawa kwa hata wale ambao sio waislamu .

Kwa nini kesi hii imezua makundi: Uisilamu ndiyo dini ya taifa la Pakistan na umeathiri pakubwa mfumo wa kisheria wa nchi hiyo. Uungwaji mkono wa sharia za kudhibiti kukashifu dini ni mkubwa. Baadhi ya wanasiasa wenye msimamo mkali wamekuwa wakipigia chapuo adhabu kali zitolewazo kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukashifu dini kama njia ya kujinufaisha kisiasa. Wakosoaji wengi wanasema sharia hizo mara kadhaa zimekuwa zikitumika kulipiza kisasi baada ya malumbano binafsi, na hukumu zimekuwa zikitolewa kwa kutegemea ushahidi finyu. Hata hivyo jamii ndogo ya Wakristo imekuwa ikilengwa na kushambuliwa kwa tuhuma za kukashifu uislamu. Na Wakristo wengi wamekuwa wakilalama na kuishi kwa hofu ya kubambikiwa kesi. Hakuna mtu ambaye amenyongwa na serikali kwa kutumia sharia hizo, lakini baadhi ya watu wameuawa mitaani na watu waliojichukulia sharia mkononi baada ya kutuhumiwa kuukashifu uisilamu. Asia Bibi ambaye ni mzaliwa wa mwaka 1971 na mwenye watoto wanne ndio mwanamke wa kwanza kuhukumiwa kifo kwa mashtaka hayo nchini Pakistan. Hukumu yake ya wali ilipingwa vikali kimataifa kuwa ni kinyume cha haki za binadamu.

Hofu iliyopo: Kuna hofu kubwa kuwa Asia Bibi na familia yake wanaweza kushambuliwa na watu wenye hasira kali baada ya kuachiwa huru. Tayari kuna nchi kadhaa ambazo zimejitolea kumpa hifadhi yeye na familia yake na inategemewa kuwa watakubali kuihama nchi yao.

01 November 2018, 14:54