Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Nigeria wanaomba serikali kufuatilia uhalifu wa biashara ya binadamu na kwamba ni njia madhubuti ya kurejesha hadhi ya waathirika Maaskofu wa Nigeria wanaomba serikali kufuatilia uhalifu wa biashara ya binadamu na kwamba ni njia madhubuti ya kurejesha hadhi ya waathirika 

Nigeria:Maaskofu na serikali wameungana kupambana dhidi ya biashara haramu

Katika mkutano uliofanyika katika mji wa Abuja hivi karibuni, Askofu Mkuu Augustine Obiora Akubeze, ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria, ameiomba serikali kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kurudisha hadhi ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

 Kanisa na serikali huko Nigeria, wanapaswa kushirikiana kwa ajili ya kutoa hadhi ya waathirika wa biashara ya binadamu. Ndicho kinachothibitishwa na Askofu Mkuu Augustine Obiora Akubeze, wa Jimbo Kuu la Benin na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Nigeria katika hotuba yake kwenye mkutano ulioongozwa na mada: “Kanisa na Serikali kufanya kazi ili kuweza kurudisha hadhi ya waathirika wa biashara”; Mkutano huo umefanyika katika mji wa Abuja hivi karibuni.

Kusaidia waathirika na kufuatilia wahusika

Katika hotuba yake, Askofu Mkuu Akubeze ameendelea kusema kuwa, “Ushirikiano wetu na serikali unapaswa kujikita kwa dhati katika kubeba majukumu ya waathirika na kutafuta njia ya kutoa msaada wa kifedha, kimaadili, kiroho na kisheria. Kuchangia, katika mchakato wa kufuatilia uhalifu wa biashara ya binadamu ni  njia muhimu ya kutaka kurejesha hadhi ya waathirika. Vilevile amesema Askofu kwamba: “sheria zetu zinapaswa kuwa na nguvu kwa namna ya kwamba watu ambao wanahusika na biashara haramu ya binadamu waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria moja kwa moja.

Kuboresha uchumi kwa ajili ya kuzuia uhamiaji usio halali

Katika mkutano huo ulioandaliwa na kikundi cha Mtakatifu Marta, Kanda ya Afrika kwa ushirikiano na Chama  Katoliki cha Caritas nchini Nigeria (CCFN) ametoa hotuba hata Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan, Askofu Mkuu wa Abuja, ambaye amekumbusha wahusika wote wa serikali ili kuboresha uchumi wa taifa. Amesisitiza kwamba, "iwapo hali ya maisha ya wanaigeria ingekuwa bora, walio wengi wasingeweza kuwa na kishawishi cha kuanza safari ya uhamiaji usiyo haliali na wakaweza kuishia kuwa waathirika wa uahalifu wa kupangwa".

Janga baya sana la unyanyasaji wa kijisia kwa watoto  

Akiendelea kusisitiza juu ya majanga mbalimbali ya nchi hiyo, Kardinali Onaiyekan amekumbusha juu ya aina za janga baya sana la kutaka faida kwa njia ya biashara ya binadamu na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na vijana. “Shughuli hii ipo chini ya uthibiti wa makundi ya kihalifu yasiyo kuwa na huruma, ambao wanapata faida kubwa kwa kuuza waathirika wasio kuwa na hatia na wala mlinzi” amesema. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kama Askofu Mkuu Matthew Ndagoso wa Jimbo Kuu katoliki la Kaduna  na Rais wa  Chama Katoliki cha Caritas nchini Nigeria (CCFN), na wajumbe wavikosi vya usalama wamethibitisha hali halisi ya uwepo wa  biashara hizi  haramu zinazofanywa na wahalifu wa Kinageria.

30 November 2018, 15:21