Tafuta

Maandalizi ya Mti wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro Maandalizi ya Mti wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro 

Mti kwa ajili ya mapambo ya Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana uko tayari Vatican!

Mtu wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana umesimikwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. Ni mti uliokatwa kwa ustadi katika msitu wa Cansiglio , na umetolewa kama zawadi kutoka Mkoa wa Friuli Venezia Giulia na Jimbo la Concordia-Pordenone Italia

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mti uliokatwa katika Msitu wa Cansiglio, umetolewa kama zawadi kutoka katika mkoa wa Friuli Venezia Giulia na Jimbo la Concordia-Pordenone Italia, ambapo tayari umesimikwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro kuanza maandalizi ya kuupamba!

Mti  huo una urefu karibia mita 21 na kipeo cha sentimita 50 na mzunguko wa mita 10 kutoka chini. Mti umekatwa na Kikosi maalum cha Mali ya Asili mahalia, katika Wilaya ya Pordenone Italia. Mapambo na taa vitaandaliwa na Kitengo cha huduma ya mafundi wa Serikali kwa ushirikiano na kampuni ya Osram ambayo vitatoa mfumo wa kuwasha taa na mapambo, kwa hali ya juu na ya kisasa, wakati huo huo kwa kuzingatia hali halisi ya utunzanji wa mazingira na utumiaji wa nguvu za umeme!

Ni utamaduni unaopyaishwa kila mwaka

Tangu Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, 1982  wamekuwa wakipyasha mapambo ya Mti wa Sikukuu ya  Kuzali wa kwa Mwokozi kwa kuwakilishwa na Holi, chini ya kitovu cha obelisk mjini Vatican. Katika sehemu ya kulia ya Pango kwa kawaida husimikwa Mti huo mrefu ambapo kila mwaka, mkoa na mkoa katika bara la Ulaya hujitolea kutoa zawadi ya mti wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Mti huo na pango vitabaki hadi siku ya kumalizika kwa Kipindi chote cha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, kwa maana hiyo katika siku Kuu ya Ubatizo wa Bwana, ambapo kwa mwaka 2019, itakuwa ni tarehe 13 Januari.

23 November 2018, 10:56