Tafuta

Vatican News
Madaktari na Africa Cuamm - Tanzania Madaktari na Africa Cuamm - Tanzania 

Mkutano wa mwaka Cuamm:Vipo vipande vidogo vidogo vya vita duniani!

Askofu Mkuu Matteo Zuppi wa Jimbo Kuu Katoliki Bologna nchini Italia, wakati wa kutoa hutuba yake katika Mkutano wa Mwaka wa Madaktari na Afrika Cuamm, amesema:"Vita nchini Sudan ni moja ya vipande vidogo vidogo vya vita duniani ambavyo vinaendelea na labda ni moja kati ya vita vilivyosahuliwa"

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

"Vita nchini Sudan ni moja ya vipande vidogo vidogo vya vita duniani ambavyo vinaendelea na labda ni moja kati ya vita vilivyosahuliwa". Hayo yamezungumzwa na Askofu Mkuu Matteo Zupi wa Jimbo Kuu Katoliki Bologna nchini Italia, wakati wa kutoa hutuba yake katika Mkutano wa Mwaka wa Madaktari na Afrika Cuamm.

Ulaya inaweka mikono yake kidogo katika mifuko

Hata hivyo Askofu Zuppi ametoa taarifa kuwa hivi karibuni atatembelea nchi ya Afrika na akiwa na Shirika lisilo la Kiserikali kwa ajili ya sababu mbili: kwanza  kuhusiana na vita vilivyosahuliwa yaani matatatizo yasiyoelezeka na sababu ya pili  anasema kwamba: makutano ambayo hufanyika mara nyngi uhanzishwa chochote. Hata hivyo Askofu pia ameonesha kwa mara ya kwanza kuwa, mwaka jana wamewza kuona ongezeko la mchango ambao waliutoa katika shirika hilo, japokuwa ameongeza kusema:“Ulaya inaweka mikono yake kidogo katika mifuko, wakati huo huo ahadi zinakuwa ni nyingi na kumbe inabidi kufanya jambo fulani pamoja, kwa sababu bila hivyo hakuna wakati endelevu wa Ulaya na  bila kuwa na Afrika”.Na kwa mtamzamo wa Bara la Afrika, Askofu amethibitisha kuwa, Afrika kwa bahati mbaya ni tatizo ambalo haliwezi kuwachwa namna hiyo katika utofauti, lakini pia Afrika ni maalum kwa fursa, kwa sababu Ulaya inaweza kuwa na wakati endelevu”.

Katika bala la Afrika ni lazima kuweka kipaumbele zaidi katika uwekezaji

Naye Stefano Menservi, Mkurugenzi wa Migawanyo ya Shirika la Kimataifa na Maendeleo wa Tume ya Ulaya wakati wa hotuba  yake katika Mkutano huo amesema: “Kama Muungano wa Ulaya, tumezungumzia juu ya ulazima wa kujenga mapatano kati ya Ulaya na Afrika kwa sababu ya hatima zake zimeungana.  Na hiyo ni kwa sababu ya kukua kwa Ulaya kunategemea kukua kwa Afrika”. Akiendelea amesema: mara nyingi wanapozungumza juu ya Afrika ni kuomba kuongeza fedha. Na hiyo ndiyo inaweza kuwa suala la dhati, lakini lipo jambo la dhati zaidi, kwa maana ya kujikita katika mtindo mwingine mpya. Kutokana na hili, anakumbuka kuwa ni lazima kuweka kipaumbele kwa sasa na zaidi katika kuwekeza, kwa maana kuna haja ya kuunda nafasi za ajira,  ambazo ni za kudumu barani Afrika, kwa maana ndizo zitachangia kuunda hata nafasi za kazi barani Ulaya. Na ndiyo changamoto ya makubaliano ambayo tunapaswa kujikita nayo, anathibitisha na kwamba  kwa mkataba wa kweli ambao hufanyike kwa kusaidiwa mfuko wa fedha, lakini pia hata utashi wa watu wa kujitolea, wajasiriamali na watu binafsi wa kuwekeza, amehitimisha.

Kwa mujibu wa Cuamm:watoto waliozaliwa  salama kwa mpango wa "Mama na mtoto kwanza"ni 117,541 

Na kwa upande wa Madaktari na Afrika wakati wa kutoa taarifa yao juu ya shughuli zao kwenye Mkutano wao wa mwaka wanasema watoto waliozaliwa  salama kwa mpango wa Mama na mtoto ni 117,541. Lengo la kutangaza ni lile la kuwawezesha watoto 320,000 wanao wasaidia na kufuatilia makuzi ya mtoto 60,000 dhidi ya utapiamlo kufikia miaka 5 ijayo. Na kati ya mambo mengine mapya yaliyotangazwa wakati wa mkutano huo ni juu ya mafunzo kwa wahudumu 1000, waliopo katika vituo vyao mbalimbali barani Afrika kwa mfano mpango wa Kitaifa wa dharura wa huduma ya madaktari nchini Sierra Leone,   pia hata panel za Solar katika Kituo cha Afya cha Wolisso nchini Ethiopia.

13 November 2018, 14:15